Turejee kwenye mambo ya ndoa: Mapenzi Vs Maslahi wakati wa kuchagua mwenzi!

Nakubaliana na wewe Babu DC, tatizo vijana wengi siku hizi wanaangalia mvuto wa kimwili, wanasahau kwamba kwenye ndoa vigezo ivyo vinachukua tu part ndogo sana
 
Du naona ile kauli ya 'Love conquers all' imebadilika na kuwa 'maslahi conquers all'.
Eiyer uko wapi?
Nakubaliana na dhana hii 'mpya' lkn iongezewe na hata kijiattraction fulani ndipo ndoa ifanye kazi. Mfano, ninataka kuanzisha familia, kwa vigezo vyangu ninataka msomi (upeo wa uelewa mkubwa), aliye financial stable, dhehebu langu, kabila langu etc. Sasa hivyo vyote ni vigezo basic, ili kusiwe na shida sana kwenye ndoa, lkn kuna aina ya watu ambao navutiwa nao, mfano napenda mwanaume mrefu, mtundu ambaye atanifanya nicheke etc. So nikimpata mwenye basic sifa zile juu, na bado l am atracted to him kwa hizo extra qualities sioni jinsi gani sintampenda.

Lkn pia, bado wale wenye upendo strong sana, ambao hauangalii hayo mambo yote; (it has to be two way though), wanaishi vizuri tu tena pengine kushinda lile kundi la kwanza. At one point mmoja anaweza akateleza, na nguvu ya kumrudisha ni upendo wake mkubwa, kama yule atakavyorudishwa na 'maslahi'. Sema couple ambao wote wana true love ni ndogo sana ukilinganisha na kundi kubwa ambalo ni maslahi+attraction driven relationship.

Sasa wewe Kaunga, si umekiri mwenyewe kuwa, watu wenye ndoa za mapenzi ya kweli (tena both sides) ni wachache sana! Ndio maana nikasema kuwa wengi wetu tunaogelea kwenye maslahi zaidi. Which is fair even biologically. Ulishaona mnyama gani anayependa kuzaa na lofa?
 
Last edited by a moderator:
Ngoja niwape kisa kidogo,
kuna rafiki yangu (university graduate) alimpenda sana dada mmoja ambaye alikuwa mdogo sana kiumri, walipishana kama miaka 10 au zaidi, isitoshe dada huyo alikuwa na elimu ya Darasa la saba. Yaani huyu rafiki yangu alikuwa akinieleza mapenzi yake, he was seriously crazy about her.

Lakini nilijaribu kumshauri kuhusu gap iliyopo kati yao kielimu na kiumri, yeye hakutaka kabisa kuelewa. nilimtolea mifano ambayo nimeshuhudia ktk familia, unajua maisha hubadirika inawezekana baadae ukamuona huyo dada hakufai may be kwasababu anashindwa kuwaentertain wageni wako (yaani wa level yako) kutokana na uelewa wake mdogo.

anyway nilikuja kukutana nae ivi karibuni analalamika kuhusu yale yale niliyojaribu kumshauri. Yaani mwanamke anashindwa kukope na maisha anayatoka yeye waishi, analalamika kwamba she is boring kwa sababu hata maongezi yao hayaendani.

kwahiyo ebu tujaribu kutafuta watu ambao you have something in common, otherwise mapenzi ufifi after sometime.
 
Yeah, you have said it all! tena sasa nimekumbuka kwani kuna siku nilitoa comment kuwashauri bachelors wa humu kwamba inabidi kujenga mahusiano na mwenzi wako kiasi kwamba ifikie mahali uone kwamba huwezi kuishi bile yeye

Hapa sasa tunaongea lugha moja. Lengo la uchumba nadhani ni kuwasaidia wahusika kujiridhisha kuwa watarajiwa wao wanakidhi vigezo muhimu vya kimaslahi na kwamba kuna chembe chembe za kemia!!
 
Ngoja niwape kisa kidogo,
kuna rafiki yangu (university graduate) alimpenda sana dada mmoja ambaye alikuwa mdogo sana kiumri, walipishana kama miaka 10 au zaidi, isitoshe dada huyo alikuwa na elimu ya Darasa la saba. Yaani huyu rafiki yangu alikuwa akinieleza mapenzi yake, he was seriously crazy about her.

Lakini nilijaribu kumshauri kuhusu gap iliyopo kati yao kielimu na kiumri, yeye hakutaka kabisa kuelewa. nilimtolea mifano ambayo nimeshuhudia ktk familia, unajua maisha hubadirika inawezekana baadae ukamuona huyo dada hakufai may be kwasababu anashindwa kuwaentertain wageni wako (yaani wa level yako) kutokana na uelewa wake mdogo.

anyway nilikuja kukutana nae ivi karibuni analalamika kuhusu yale yale niliyojaribu kumshauri. Yaani mwanamke anashindwa kukope na maisha anayatoka yeye waishi, analalamika kwamba she is boring kwa sababu hata maongezi yao hayaendani.

kwahiyo ebu tujaribu kutafuta watu ambao you have something in common, otherwise mapenzi ufifi after sometime.

Sina cha kuongeza.

Kupenda ni jambo zuri sana but unfortunately very rare!

Ni vizuri watu wajue kuwa hata limbwata linafika mahali linaexpire!!
 
Nakubaliana na wewe Babu DC, tatizo vijana wengi siku hizi wanaangalia mvuto wa kimwili, wanasahau kwamba kwenye ndoa vigezo ivyo vinachukua tu part ndogo sana

Hao wanahitaji msaada haraka na tusijidanganye eti tuwaombee tu bila kuchukua hatua.
 
Unajua ni vigumu sana kumshauri mtu mzima, hasa pale anapokuwa kapenda. wanasema eti tusiwachagulie, wanasahau kuwa sisi wapembeni lakini wenye mapenzi mema tunaona zaidi ya wao walio blinded na love.

inachokera wanapoanza ugomvi hawaishi kuwaletea kesi. ukiangalia ugonvi wenyewe unahusisha yale yale uliyoshauri yakapuuziwa, its such a waste of time.

Hao wanahitaji msaada haraka na tusijidanganye eti tuwaombee tu bila kuchukua hatua.
 
Mapenzi hayana mwalimu. Kila mtu huingia kichwa kichwa, na baadaye hujuta kivyake vyake, katika suala hili, walimu wamefeli, wanafunzi wamefaulu, and the viceversa also can be true.
 
Mapenzi hayana mwalimu. Kila mtu huingia kichwa kichwa, na baadaye hujuta kivyake vyake, katika suala hili, walimu wamefeli, wanafunzi wamefaulu, and the viceversa also can be true.

Uko sahihi kabisa. Ila unadhani mijadala kama hii haiwezi kusaidia kitu?
 
Just being in love is not enough for two people to decide to spend the rest of their lives together. It is not even enough to start a relationship! It is important, it is essential but BY NO MEAN enough!

Kwa nini tunaichukulia Love kama kitu kinacho 'exist' independently?
Ain't love a combination of lots of things?
 
.. nilimweleza kuwa katika maandalizi ya kuingia kwenye ndoa, kuna vitu vingi ambavyo ni muhimu sana kuvipa kipaumbele cha aina yake. Miongoni mwa vitu hivyo ni mapenzi/upendo na maslahi (uzuri, elimu, kiwango cha ustaarabu, utanashati, urembo na sifa nyingine za ndani na nje ambazo mhusika anazo).

Dark City hebu fafanua kidogo hapo kwenye red..
Mimi nadhani ni ngumu kutenganisha mapenzi na maslahi..kwa maoni yangu maslahi ndio yanapelekea mtu aseme nampenda flani!
 
Last edited by a moderator:
Uko sahihi kabisa. Ila unadhani mijadala kama hii haiwezi kusaidia kitu?
Nakushukuru kwa kuliona hilo, ingawa napenda kuwasihi vijana wasipende mijadala ambayo mwisho wa siku yaweza kuwapotosha. Wapo wengi wameoa nje ya makabila yao, wana enjoy na ndoa zao, wakati huo huo wapo wengi walio oa makabila yao na wanajuta, and the viceversa can also be true.
Kitu kikubwa ninachoweza kukusaidia, ni kwamba ndoa inaunganisha watu wawili wenye tabia tofauti, mila tofauti na desturi tofauti. Mara tu baada ya muungano huo, upo muda wa tabia, mila na desturi hizo kugongana. Wazoefu wanasema inaweza kuchukua miaka hadi 7, kabla watu hawa hawajakubaliana tabia, mila na desturi ipi iongoze nyumba yao. Hii haijalishi Kabila wala dini. Hivyo kwa ushauri wangu wa bure, kuoa ni just a game. nobody knows who will win. Mungu akubariki.
 
Kwa nini tunaichukulia Love kama kitu kinacho 'exist' independently?
Ain't love a combination of lots of things?

Uko sahihi ila ukiwasikiliza baadhi ya wadau unaweza kupata hisia kuwa hivi ni vitu tofauti. Hata hivyo, watu wengi huweka mkazo kwenye maslahi zaidi wakati wa kutafuta wenzi na hilo ndilo tunalojadili.
 
Nakushukuru kwa kuliona hilo, ingawa napenda kuwasihi vijana wasipende mijadala ambayo mwisho wa siku yaweza kuwapotosha. Wapo wengi wameoa nje ya makabila yao, wana enjoy na ndoa zao, wakati huo huo wapo wengi walio oa makabila yao na wanajuta, and the viceversa can also be true.
Kitu kikubwa ninachoweza kukusaidia, ni kwamba ndoa inaunganisha watu wawili wenye tabia tofauti, mila tofauti na desturi tofauti. Mara tu baada ya muungano huo, upo muda wa tabia, mila na desturi hizo kugongana. Wazoefu wanasema inaweza kuchukua miaka hadi 7, kabla watu hawa hawajakubaliana tabia, mila na desturi ipi iongoze nyumba yao. Hii haijalishi Kabila wala dini. Hivyo kwa ushauri wangu wa bure, kuoa ni just a game. nobody knows who will win. Mungu akubariki.

Ahsante sana kwa mchango wako.

Hata hivyo, naomba nikiri kuwa sijaelewa perspective yako katika mjadala huu.
 
Dark City hebu fafanua kidogo hapo kwenye red..
Mimi nadhani ni ngumu kutenganisha mapenzi na maslahi..kwa maoni yangu maslahi ndio yanapelekea mtu aseme nampenda flani!

Hivi vitu vinatenganishwa tena sana. Hivi hujagundua hadi sasa kwamba mabinti wenye kazi nzuri wanasumbuliwa sana na wanaume matapeli wa mapenzi? Na pia hujasikia mitaani wakisema kuwa kijana mwenye usafiri ana chance zaidi ya kujipatia wachumba?
 
Last edited by a moderator:
Dark City , tuko busy na shopping ya sikukuu si unajua wajukuu zako bila nguo mpya hapakaliki.

Mada ni nzuri na kweli nimekufahamu, mapenzi peke yako hayatoshi kuwa na long lasting relationship, hayo maslahi unayoyazungumzia kwa watu wa siku hizi wanaangalia kipata zaidi ambacho nacho kipo leo kesha hakipo, lakini vitu kama sifa na tabia za mtu ni muhimu hata family ya mtu anapotekea lina umuhimu fulani. Ni vipi ambavyo hatuvipi umakini lakini hivi huwa ndio vinaweka mapenzi. Sisemi kuwa mapenzi sio lazima lakini to my context sio lazima umpende mtu kupindukia ndio kujua ndio mwenza. Muhimu kuwa kuna some common ground or some likes its enough to be together.

Ubarikiwe
 
Ahsante sana. Sina cha kuongeza.
 
Last edited by a moderator:
Kaunga, hiyo la love conquers all anayeiamini na kuiishi ni MwanajamiiOne peke yake.

Nakubaliana na Babu DC, love peke yake haitoshi, nafasi ya maslah katika mahusiano ya kudumu ni kubwa.

Kuna ndugu yangu aliolewa na 'love of her life' wote tulikuwa tunapinga ndoa hiyo lakini halueleewa kabisa.

Waliamua kufunga ndoa 2006, na sasa navyoongea wako kwenye mchakato wa kuachana kisheria.

Kisa cha kuachana baba mwenye nyumba hakuwa anasaidia lolote wala kujihusisha na lolote ndani ya familia zaidi ya amri ya sita.

Ada za watoto, chakula, malazi yote ni huyu dada alikuwa anafanya mwenyewe, sasa huwa najiuliza lile 'PENZI kali la KIHINDI' limeenda wapi?
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli Dark City, ni rahisi sana kusema mbele za watu mara mambo yanapoharibika kuliko before.
lakini tukiangalia kwa karibu kabisa, sijui logic ya ndugu wa huyo mjukuu wako kumwambia akaoe mdada wa kabila lao. kama kuna mdada wa kabila lao ambao wameshamwona na wanaona anafaa kuwa mke wa ndugu yao ni sawa, lakini kama hakuna ambaye wamem-identify, ila wanataka yeye ndo aanze kutafuta wanampa kazi kubwa sana, sipati picha anaanzia wapi........... kila akikutana na mdada ambaye anamvutia swali la kwanza liwe "kabila lako" lol!

Hata mimi nimepawaza sana hapa Fixed Point, kulazimishwa kuoa mtu wa kabila lako ilhali huna mahusiano bado na mtu wa jinsi hiyo. Ni kazi ngumu sana ameepewa huyu mjukuu wa babu yetu Dark City.

Mkasa huu ulimtokea kijana mmoja wa kwetu, maana miongoni mwa makabla yenye kasumba hii ni wakwetu huko. Alileta mchumba mrugulu, very beautiful, decent, mpole nakadhalika. Wazazi wakataa kabisaaa kwa nguvu zote wakidai wanataka wa kabila lao, otherwize aoe huyo mrugulu but asahau kuwa ana baba, mama na ndugu. Ilikuwa hot and serious.
Aliamua kufuata ya ukoo akiogopa laana, akatafuta wakwao tena kujijini kabisaa, na alikuwa 7yrs older than him. but after marriage life was living hell. Yule mkaka alianza tabia ambazo hakuwa nazo, alianza ulevi, uhuni na akawa mtu wa kutanga tanga tanga, simply because yule aliye nao si wa chaguo lake na hampi vile alivyovizoea na hana furaha nae na amejitahidi kumkubali imeshindikana.

Mwisho wa siku kaka yangu yule alifariki kwa HIV/AIDS akiacha mjane na mtoto wa 5yrs, na hadi anakata roho alilaumu ukoo wake wote esp mama yake ambaye ndo alishika bango kweli kweli.

So nashauri pamoja na mslahi mengi mengi katika mahusiano na ndoa, wazazi/ndugu hebu tuwaachie watu wachague wenzi wao wanaotaka kuoa au kuolewa nao tusije tukawa wakulaumiwa baadae mambo yanayofanana na haya yakitokea.
Ahsanteee

I
 
ni kweli kwamba tuingiapo ktk ndoa ule upendo wa awali na hamshahamsha la kimahaba tulokua nalo kabla ya kuhalalishana kwa pingu laisha na tunageukia ktk maslahi...?? Na je ni kwa wote.!? Dark City ? et.al

Babu data
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom