Tupunguze marafiki feki...

Tupunguze marafiki feki...

Mimi sijui hata kama nina marafiki!

Nadhani nina watu tu ambao tunakutana katika matukio, nyakati, na kazi rasmi peke yake.

Tofauti na hapo hapana na sihitaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao utakao wadelete kwa kisingizio dhaifu cha kutowasiliana nao mara kwa mara ipo siku utawakumbuka
Inategemea mkuu,namba miaka 5 huna mawasiliano nayo unategemea ipo siku itatokea miujiza
 
Mkuu sio watu wote waliopo kwenye simu lazima uwe unawasiliana nao kila siku, wengine una wasiliana nao wakati unahitaji jambo fulani mfano unahitaji msaada fulani na anaeweza kukusaidia hilo jambo ni mtu uliefuta namba yake inakua tabu kuanza kutafuta namba ya huyo mhusika upya
Nakubaliana na wewe,kama mawasiliano yenu yana gap ya miaka 5 na zaidi,kuna umuhimu wa kuitunza hiyo namba?
 
Kuna watu mnapenda tu kulalamika na kuweka lawama kwa binadamu wenzenu... Jiulize wewe uko kwenye list ya watu wangapi? Wote huwa unawapigia?

Mtu anaishi kwa basics hawezi kulalamika ovyo eti fake friends hamuwasiliani... Binafsi Mimi huwezi kuwa unawasiliana na mimi kwa maswala yasiyoeleweka kila siku, tutasalimiana na kujuliana hali.. Kwenye contact list yako haiwezekani watu wote 200 wawe wanakupigia wewe..

Futa hzo namba baadae usumbue watu, Mimi naheshimu nafasi ya kila mtu... Kuna mtu unayedhani huna haja na namba yake, siku moja unajikuta unahitaji hata kuulizia mashamba huko kwao, au hata dawa aliyowahi kukwambia alimpa mwanae ikamsaidia na wewe ndo unaitaka halafu ulijimwambafai eti 2020 goals nadelete Namba..

Tuache kulalama hovyo

Ulimwengu umebadilika mkuu kutokana na teknolojia, sasa hivi ukiwa na shida yoyote...weka mezani utapata suluhisho.Kuliko kuwa na list ndefu ambayo una zaidi ya miaka 5 hakuna mawasiliano.
 
Nakubaliana na wewe,kama mawasiliano yenu yana gap ya miaka 5 na zaidi,kuna umuhimu wa kuitunza hiyo namba?
Umuhimu ni je huyo mtu anaweza kukusaidia kwenye jambi gani kwa wakati husika...
 
Unakuta kwenye simu yako una list ya marafiki 1000+; ambao umewasiliana nao mwaka mzima na mawasiliano yao na wewe yako active ni wanne (4) tu; Sasa hao wengine uliowaweka kwenye simu yako wana tija gani kwa maisha yako. Kwa mtazamo wangu, ni bora uwe na idadi ya watu wachache kwenye simu yako ambao kweli unaona wana tija. Kuwa na list ndefu ya majina ni kuichosha simu yako na kujipa faraja kwa marafiki feki ulionao. Kwa maoni yangu tubadilike
 
Attachments

  • 5CAA63F4-05E4-4992-8173-2F3809F23FF5.jpeg
    5CAA63F4-05E4-4992-8173-2F3809F23FF5.jpeg
    34.9 KB · Views: 13
Back
Top Bottom