Tupendane: Matukio 08 wakristo,wayahudi na waislamu waliyookoana ktk mazingira usiyotarajia

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Tusibaguane

JIFUNZE HAPA

1:WAISLAM WA SYRIA na WAALMENIA WA UTURUKI
Armenians_marched_by_Turkish_soldiers_1915.jpg

Chini ya utawala dhalimu wa OTTOMAN uturuki waliamua nchi nzima iwe ya waturuki na ya kiislamu na kufyeka makabila yote na wakristo. Waalmenia zaidi ya million 2.5 wengi wao wakristo walikuwa wahanga wa kwanza. wengi walikimbilia syria nchi ambayo wayahudi,wakristo na waislamu waliishi kwa upendo. Waislamu waliwapokea wakristo hawa na kuwahifadhi hadi syria ikaitwa MBINGU SALAMA/Safe heaven. Fadhila zinalipwa leo maana waislamu wa syria wakikimbia vita dhidi ya ISIS wanapokelewa na jamii ya WAALMENIA waliopo ULAYA, CANANDA na US wakikumbuka wema waliwafanyia.

2:KIJANA WA KIISLAMU REFIK (17) ALIYOOKOA FAMILIA ZA KIYAHUDI
iStock_000032313968_Small.jpg

Kabla ya msako wa kuwauwa wayahudi. Albania wakristo,wayahudi na waislamu waliishi kwa upendo. Myahudi mmoja Moshe Mandil alikuwa amemuajiri kijana huyu wa kiislamu. baada ya msako wa HItler kuwaua wayahudi. Kijana huyu aliichukua familia hii na kuificha nyumbani kwao milimani. Sio huyu tu wayahudi wengi walihifadhiwa na waislamu na kuwaokoa maisha.

3:MAKASISI WA KIGIRIKI
iStock_000091235591_Small.jpg

Hapa wakristo na wayahudi waliishi vizuri kabisa. Wanazi walioingia waliomba list ya Wayahudi wote ili wawaue. Kadrinari aliyaandikia makanisa yote na makasisi barua kuwa Wawatengenezee Wayahudi VYETI FEKI VYA UBATIZO ili waonekane ni wakristo ili wasiuwawe. Kuna kisiwa kimoja nchini hapo kilikuwa na wayahudi 257 aliwaadaa wanazi kuwa kuna wayahudi wawili tu. Msako mkali wa SHOOTING SQUARD haukuwaona hata mmoja wote walifichwa na wananchi.

FAIDA: Mwaka 1953 lilipotokea tetemeko ugiriki Taifa la kwanza kutoa msaada tena haraka lilikuwa ni ISRAEL.

4:UOKOAJI WA WAYAHUDI DENMARK
iStock_000007460704_Medium.jpg

Hapa SHOOTING SQUARD ya WANAZI ilimuhitaji mfalme atoe tangazo kuwa wayahudi wote wavae ngue zenye alama kama nyota hapo juu ya njano(david star) ili wawatambue kirahisi maana wakristo/warutheli na wayahudi walikuwa karibu mno. Cha ajabu wa kwanza kuvaa hivyo alikuwa Mfalme mwenyewe na kuwataka watu wote wavae hivyo. Hii iliwachanganya wanazi. Walipokuja kwa kasi kuua walichelewesha huku maelfu ya wayahudi wakitoroshwa na meli za wavuvi. Ikiwa ni idadi kubwa kabisa. Hadi leo matajiri wakubwa na wanaoifanya denmark iwe juu kitechnolojia na kiuchumi ni hawa jamaa.

5:MSIKITINI PARIS PALIPO GEUZWA MBINGU SALAMA KWA WAYAHUDI
640px-Grande_Mosqu%C3%A9e_de_Paris.jpg

Wanazi walipoichukua PARIS 1940. Msako wa wayahudi ulianza na maelfu wakubwa kwa watoto walikamatwa na kupelekwa kambi za mateso Ujerumani. Ni huu msikiti uliowaficha kwa kuwapa chakula,malazi na hata fursa ya kuoga mamia ya wayahudi wenye asili ya Afrika kaskazini na kuwaokoa.

6:Tahrir Square
800px-Tahrir_Square_-_February_9_2011.jpg

Katika hali ambayo haikutarajiwa Wakristo waliweka tofauti zao pembeni wakaungana na waislamu kumuondoa madarakani Mubarack. Hii ilithibitishwa zaidi siku ya kuondoka baada ya ushindi Ijumaa February 2011, Waislamu walitoa mikeka yao na kuanza kuswali huku wakristo wamewazunguka kuwalinda. Hata baadae wakristo walipoanza kuvamiwa na wachache wenye nia mbaya waliibuka waislamu kuwalinda.

7:SHOMRIM - ASKARI MAALUMU WA KIYAHUDI WALIOJITOLEA KUWALINDA WAISLAMU
Stamford_hill.jpg

Baada ya jamaa mmoja kuchomwa kisu LONDON (MWANAJESHI) na ikasemekana Alichomwa na waislam. Ilizuka vurugu kubwa huku misikiti ikichomwa moto, makundi ya vijana yakiwachoma visu waislamu kama kisasi. Kikundi kimoja cha Wayahudi SHOMRIM kilijitolea kuwalinda waislamu na kuwasaidia polisi. Polisi haya jamii pamoja na waislamu wachache walishirikiana kushika doria usiku na mchan kuwalinda waislamu wasiuwawe huko. Kikundi hiki cha WAYAHUDI kimekuwa MACHO na MASIKIO ya polisi na kimekuwa msaada kwa watu wa imani zote hasa waislam.

8:HII YA WAKRISTO WA NA WAISLAM WA CAMEROON ITAKUSHANGAZA ZAIDI
726px-LamidoGrandMosque.jpg

BOKO HARAM wanaojiita waislam ila cha ajabu huko wanashambulia MISIKITI na MAKANISA. Hii imewafanya waislam na wakristo cameroon kuwa wamoja na kuweka tofauti zao kidini. Sasa WAKRISTO wakiwa wanasali waislamu wanawalinda nje hadi ibada iishe, Waislamu wakiwa wanaswali basii wakristo nao wanapeana zamu ya kuwalinda waislamu hadi ibada iishe. Mfano huo msikiti unaitwa lamido Grand hicho kitu hufanyika.

MODS: Hii sio ya kidini isipelekwe jukwaa la dini hii ni mada ya KIJAMII.

karibuni: Sema chochote
 
Kumbe tunaweza kuwa wamoja licha ya tofauti zetu za kidini sasa je huu utofauti chanzo chake ni nini???maana kuna jamii ambazo hawapendani sababu ni dini
Wana siasa mkuu. hao ndio wanaleta fitina ili wajipatie maslahi yao. Angalia vyanzo vingi vya mizozo ya dini utakuta mikono ya wanasiasa ndani yake. Na wakisha washa moto basi kuuzima ni taabu
 
Wana siasa mkuu. hao ndio wanaleta fitina ili wajipatie maslahi yao. Angalia vyanzo vingi vya mizozo ya dini utakuta mikono ya wanasiasa ndani yake. Na wakisha washa moto basi kuuzima ni taabu
kweli utasikia zamu hii ni ya mtu wa dini flani, au kiongozi akifanya maamuzi utasikia ni kwa sababu huyo jamaa ni dini flani hata kama umeelezewa kila kosa aliliofanya.
 
Wana siasa mkuu. hao ndio wanaleta fitina ili wajipatie maslahi yao. Angalia vyanzo vingi vya mizozo ya dini utakuta mikono ya wanasiasa ndani yake. Na wakisha washa moto basi kuuzima ni taabu
Daaa kweli aisee siasa inasababisha mizozo sana katka jamii zetu
 
tofauti za kidini tuziweke pembeni tuwe wamoja kwani tumetoka na tunatunzwa na Baba mmoja, tuna utu na haki sawa! mafundisho tofauti ya kidini hayambadilishi Mungu vile alivyo na wala hayataweza kumfanya abadilishe sheria na kanuni zake. tuwe wapole na wanyenyekevu tumuamini na tupendane!
uko vzr
 
Udini hauwez kuisha as long as u
dini zipo, na ubaya wa dini hupelekea makundi mawili, kwenye kila arguement
Sisi wasafi ,wao wachafu
Sisi waamini mungu, wao wana kosea.
Halaf hakuna hata mtu anaye jua usahih au kutokuwa sahihi kwa dini

Naamini Mungu yupo, ila naamin some tymes dini hu harib image ya Mungu na huwatenganisha binadam kuanzia ki hisia, hadi kijamii
ili umwelewe wa dini nyingine usiwe extreme sana kwenye dini yako
 
wanasiasa na mabepar ndio wabaya sana wana2mia migogoro ya kdni kujiimarsha kisiasa na kiuchum. 2we wa moja mkristo, mpagan, din za asil, muislam nk
 
Safi sana...Basically muislamu ni uzao wa mtoto mkubwa wa kwanza wa Ibrahim (Ishmael) na Wakristo ni uzao wa mdogo(Isaka), mi huwa nashangaa sana wanaoshadadia chuki za dini...ni ukosefu wa elimu tu na roho mbaya...
 
Great topic! "Na hapo ndipo siri ya 'tunda la uzima wa milele" or "fumbo la siri"....ilipo!

The day human beings understand the truth and reality of Humanity it's the day "Eternal Life, Real Life" will be given to us! Siku ambayo wote kwa pamoja tutakubali kwamba yupo Mungu mmoja tu na Hana mshirika, hakuzaa wala hakuzaliwa, alituumba ili tumtumikie na tumtukuze yeye tu maana ndie ajuaye ya hadharani na sirini, basi tutakua tumejua na tumetambua "dhambi" waliyoitenda "wazazi wetu, Adam / Eva/Hawa" na kuitubu/kuungama kwa wote kwa wakati mmoja mbele ya Muumba mmoja na ndiyo siku Ibilisi atakosa mfuasi hata mmoja zaidi ya waliotangulia/kusudiwa (Mola anajua zaidi) na mamlaka ya Muumba wa Mbingu na Ardhi itarudi katika mikono yake "at one whole/complete piece".........duh!!

***My opinion tu jamani.....was kinda imagining the bliss/peace around the world!!
 
Back
Top Bottom