Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Biashara ya bodaboda na suzuki cary kwa kusubiria hela ya wiki...

Bodaboda zilikiwa tano, kila moja ilikuwa inaleta 50,000/- kwa wiki. Hela ya service ilitoka hapo hapo, wastani wa 8,000/- kwa wiki EXCLUDING major breakdown.

Sasa uswahili wa madereva mara mtu alete 30,000/- na maelezo ya 20,000/-.... kingine wizi... baadhi ziliibiwa ila kwa vile niliziwekea bima kubwa nikalipwa na bima. Mwishi niliziuza zote zilizobaki

Suzuki cary nazo mbwembwe na longo longo za madereva zilokuwa ishu. Unfortunately moja iliibiwa baada ya dereva kuuwawa. Bima kubwa ilinisaidia kulipwa.

Risk ni nyingi. Hivyo vi-cary hubebeshwa mizigo kuliko uwezo wake.
Matrafiki nao barabarani wakiona cary ni kama wanaona hela inayotembea... hawavichi vikafanya kazi zake kwa uhuru.. kilichobaki nikakiuzilia mbali

By the way, kwa mtu anayetaka kufanya biashara ya bodaboda, ni bora afanye kwa mkataba. Unanunua bodaboda 2M, unachukua 10,000/- kila siku kwa miezi kumi au zaidi kutegemeana na makubaliano mnayoandikishana. Muda ukifika inakuwa ya uliyeandikishana naye
 
Ngalikihinja,
Ila Suzuki carry vinaonewa sana.
Mwaka flani nikiwa Dar jamaa yangu flani alikuwa anakimiliki na kuendesha mwenyewe ila kashkash za trafiki zilikuwa kubwa sana
 
mi ni biashara ya kuuza nguo za mtumba mnadani, aise yan baro la jeans unanunua laki sita, kilo mia lkn jeans unazozkuta ndani ni kichekesho ilinikata mtaji nikaamua nilime nyanya tu. na ctaman tena mambo za mtumba hela yake n ya moto ata yamoto band haifkii.
Katika hustle za maisha huwa watu tunajaribu Biashara mbalimbali ili kuweza kufanikisha malengo yetu lakini wengi wetu huweka mitaji mikubwa pengine pesa za kukopa na mwisho wa siku changamoto zikiwa nyingi tunakata tamaa na kuacha.

Mimi binafsi nakumbuka nilianza biashara ya kuuza saa na viatu vya kike lakini changamoto kubwa ikawa ubora wa zile bidhaa. Aisee nilipata malalamiko mengi sana nikaamua kuacha. Laiti ningejua ningeboresha ubora wa zile bidhaa tu pengine leo ningekuwa na mtaji mkubwa sana.

Karibuni tushirikishane kuhusu biashara gani ulianzisha, changamoto ulizopitia na ulizitatua vipi au uliacha?

Uzi huu unaweza kuwa mwanga kwa watu wengine pia.
 
*OFFICE/KIGOLI INAUZWA WAPENDWA IPO MTAA WA MAFIA NA SKUKUU NI KIGOLI CHA PEMPARS NA VITU VYA WATOTO INAUZWA NA KILA KITU KILICHOMO MWENYEWE KAHAMISHWA KIKAZI HIVYO WANAHAMA NDO AKAAMUA AUZE KWA MAELEZO ZAIDI 0688008799 NO YA MUHUSIKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[QUOTE="kapunika,
Umesema kweli tupu. Halafu kuna kitu kingine watu wanaona ni kidogo kumbe kinachangia sana: kuamini ushirikina. Kuna mdau anajiita mtena amesema kuwa sababu ya kunaguka kwenye biashara za Mpesa etc ni pamoja na ''chuma ulete''! Hili ni tatizo kubwa kwa wafanya biashara wengi.

Mtu anaanzisha biashara anaacha kuwekeza nguvu kwenye kanuni za biashara na badala yake anafanya ushirikina uwe ndiyo mwongozo wake! Mtu wa aina hii ataacha kufeli? Unakuta wengine kwa mfano anafungua Bar, badala ya kuboresha huduma na kufanya ubunifu zaidi ya wengine yeye anakimbilia kuzika kondoo au wanyama wengine kwenye eneo la biashara.

Matokeo ni kuwa anakuwa amejiridhisha kuwa sasa atapata wateja na mambo kama huduma nzuri anayasahau.
Mkuu biashara ya Mpesa inachangamoto nyingi sana ila hii ya kupoteza pesa ni jambo la kawaida mno. Nimeifanya kwa muda mrefu sana. Unafunga hesabu jioni kukuta laki 3 hakuna ni jambo la kawaida mno. Unameza mate machungu unasubiri commission ije kufidia hasara.
 
[QUOTE="kapunika,
Umesema kweli tupu. Halafu kuna kitu kingine watu wanaona ni kidogo kumbe kinachangia sana: kuamini ushirikina. Kuna mdau anajiita mtena amesema kuwa sababu ya kunaguka kwenye biashara za Mpesa etc ni pamoja na ''chuma ulete''! Hili ni tatizo kubwa kwa wafanya biashara wengi.

Mtu anaanzisha biashara anaacha kuwekeza nguvu kwenye kanuni za biashara na badala yake anafanya ushirikina uwe ndiyo mwongozo wake! Mtu wa aina hii ataacha kufeli? Unakuta wengine kwa mfano anafungua Bar, badala ya kuboresha huduma na kufanya ubunifu zaidi ya wengine yeye anakimbilia kuzika kondoo au wanyama wengine kwenye eneo la biashara.

Matokeo ni kuwa anakuwa amejiridhisha kuwa sasa atapata wateja na mambo kama huduma nzuri anayasahau.
Mkuu kwenye biashara ya mpesa,Tigo pesa lazima utapigwa tu Nina uzoefu na hiyo biashara 6 yrs now so I am talking from my experience sio chanjanja Wa kijiweni tu mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom