Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 284
- 442
Msingi wa biashara yoyote ni Mauzo. Bila mauzo basi hakuna Biashara.
Hata hivyo changamoto ambayo inawakumba wafanyabiashara wengi ni kupata wateja.
Kuwa na bidhaa au huduma ni jambo moja na kujua kuuza bidhaa hiyo ni jambo jingine.
Unaweza kutumia mbinu hizi kuongeza wateja.
1. Kutumia mitandao ya kijamii /internet.
Zaidi ya Watanzania 27M kufikia April walikua wanatumia internet.
Watanzania wengi hutumia wastami wa masaa mawili mtandaoni kwa siku.
Ukitumia mitandao ya kijamii kibiashara unaweza ongeza mauzo yako sana.
Unaweza kutumia matangazo ya kulipia (Sponsored ads) kufikia watu wengi zaidi kama huna wafuasi wengi mtandaoni.
Pia unaweza tumia watu wenye ushawishi mtandaoni kujitangaza ,hapa inabidi kuwa mwangalifu na kujua watu hao wana aina gani ya wafuasi na je wanaendana na biashara yako?.
Naweza kukusaidia kwenye hili.
2.Tumia watu wakutafutie wateja na uwalipe kwa commission.
Mfano Unauza Kiwanja Milioni 8. Mtu alikuletea mteja una mlipa asilimia kadhaa 5_10.
Au kama Bidhaa Unauza laki moja unaweza mwambia mtu auze kwa kuongeza bei kidogo ambayo itakua faida yake. (inategemea aina ya bidhaa pia kuwa makini ili usiharibu image ya biashara yako)
Unaweza kutumia pia mfumo wa Network marketing.
Kwangu mimi hii ni njia nzuri kwa mfanyabiashara ikifanywa kitaalamu.
Wapo watu wengi hawana kazi, wengine wanatamani kuanzisha biashara lakini hawana mitaji.
Kupitia njia hii utaongeza mauzo lakini pia utakua umesaidia watu wengine kupata riziki .
3. Tengeneza Brand (Jina)
Hii ni njia ya kuuza bila kutumia msuli.
Hii ni njia nzuri kwa wenye biashara za huduma au wenye maono ya kukuza biashara kwa muda mrefu.
Brand hiangalii leo tu, ni maono ya muda mrefu.
Unaweza tengeneza brand yako kwa matangazo, Huduma nzuri, Kuonekana na kusikika na kujenga taswira ya biashara yako ( image)
4.Patikana haraka na kwa wepesi.
Ukiserch kitu Google huwa ni option gani unawahi kuiclick na kuangalia, za mwanzo, mwisho au page zinazofuata?
Ni zile zinazopatikana mwanzo.
Hakikisha biashara yako inaonekana kwa haraka na inafikika
Watanzania wengi hatupendi complications, hakikisha unapunguza process kwa mteja ili apate bidhaa yako kiurahisi.
Huoni njia za kutuma pesa kwenye simu watu wanazipenda kuliko kutumia Benki ambako kuna process nyingi?
Haya ni machache tu.
Kelvin Kibenje
Mtaalamu wa mauzo na masoko
Kama unapata changamoto kwenye mauzo Tuwasiliane tukusaidie.