Uchaguzi 2020 Tupeane mikakati ya mwisho ya kuifuta CCM

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
276
1,000
kura yangu inakwenda kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, mnapiga sana kelele kuongoza nchi sio suala la mzaha mzaha. Kuna mtu chama chake kimeshindwa hata kujenga ofisi ya chama licha ya ruzuku kedekede leo anaomba ridhaa tumpe uongozi aijenge Tanzania? Hizi ni dharau za waziwazi na majibu atayapata tarehe 28 Oct. Hizi thread zote tutazifukua maana watu wa hulka kama ya mleta mada wana kumbukumbu ndogo sana. Amesahau kama 2015 alideki barabara .
Huijui CCM wewe, kaa kimyaa.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,893
2,000
Kila siku nawaambia Tundu Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sio 2020 tu bali kamwe(NEVER). Kwa anayejua system ya Tanzania inafanyaje kazi peke yake ndio atanielewa. Kwa wengine mliojaa kelele za kijipa matumaini za "NI YEYE", hamuwezi kunielewa. Ila nina uhakika hata Lissu mwenyewe na Mbowe wanajua. Tanzania ni zaidi ya mnavyoijua na kuijadili mitandaoni. Mpaka tarehe 30 mwezi huu ndo mtaelewa ninachomaanisha hapa.
 

Enlightening

Senior Member
Oct 14, 2020
170
250
Enyi watia nia 7000 wa CCM mlionyimwa mishahara.

Enyi wagombea wa CCM mlioshinda kura za maoni na kutoteuliwa.

Enyi wafanyabiashara mliofirisiwa mitaji yenu kwa kodi za TRA.

Enyi watumishi mlionyimwa haki yenu ya nyongeza ya mshahara wa kila mwaka.

Enyi wakulima ambao mmekopwa mazao yenu na mazao yenu kupata bei hafifu.

Enyi wanavyuo mliokosa mikopo ya elimu ya juu.

Enyi watumishi wa umma na binafsi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao mmepandishiwa riba kutoka asilimia 3 baadae 8 na kufika 15.

Enyi mama ntilie, machinga, na wafanya biashara wadogo wadogo mliouziwa vitambulisho vya mjasiliamali kwa elfu 20.

Enyi ndugu za waathirika wa kesi za kubambikia na vifungo vya uonevu.

Enyi ndugu za waathirika wa utekaji, utesaji, na mauaji ya wasiojulikana.

Enyi watumishi mlioacha au kuachishwa kazi na mnaathirika na kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwenye mifuko ya pensheni.

Enyi wastaafu watarajiwa kuanzia mwaka 2022 ambao mtakumbana na kikokotoo kandamizi cha mafao yenu ya kustaafu

Enyi watumishi wa umma mlioitwa "watumishi hewa na vyeti feki" mliofukuzwa kikatili.

Enyi maafisa, wakurugenzi, wakuu wa idara, makatibu wakuu, mawaziri na maafisa wengine wote, mlioathirika na tumbuatumbua na tenguatengua zisizo na haki.

Enyi watanzania wote mliopata madhara katika utawala wa miaka mitano ya serikali ya CCM ya Magufuli.

MIMI MWANA CCM NINAWAOMBA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA:

Tumia dakika mbili kila siku, kwa siku zilizobaki kabla ya tarehe 28/10/2020, kuwapigia simu ndugu, jamaa, na marafiki wa mijini na vijijini kuwaelimisha jinsi ya kujinasua kwenye makucha ya CCM ya Magufuli, kwa kumpigia kura TUNDU LISSU, kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Watanzania mpoooooooo!

#Haki Huinua Taifa#
Umesahau kututaja tulio maliza vyuo miaka 4 sasa ajira hakuna saizi tunaoneka wasomi ni wapumbavu flani ,kura yangu ni Lisu
 

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,243
2,000
Kinachosikitisha lakini ni ukweli, NEC na CCM wamejipanga sana kudhurumu uchaguzi na Magufuli atatangazwa mshindi.

Kamanda usikate tamaa mapema... Hata ikipita wiki baada ya matokeo ya uchaguzi... Wengi wapo tayari kuingia barabarani kudai haki sehemu mbalimbali nchini... Nguvu ya umma itaonekana na haitoweza kuzuiwa..

Amin
 

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
276
1,000
2015 nilifanya ujinga ambao umenitesa kwa miaka 5 tena nirudie kosa ? Never ever
Makosa ya 2015 watanzania wengi tunajutia. Lakini sio kosa letu, alijivisha vazi la malaika kwa nje, wakati ni shetani kwa ndani. Alijifanya malaika wa nuru hivyo ilitakiwa macho ya rohoni kumuona. Gwajima na watumishi wengi wa Mungu waliona lakini....
 

Enlightening

Senior Member
Oct 14, 2020
170
250
Makosa ya 2015 watanzania wengi tunajutia. Lakini sio kosa letu, alijivisha vazi la malaika kwa nje, wakati ni shetani kwa ndani. Alijifanya malaika wa nuru hivyo ilitakiwa macho ya rohoni kumuona. Gwajima na watumishi wengi wa Mungu waliona lakini....
Tumkatae tuwaambie na ndugu zetu tumkatae ametutesa sana nafsi zetu
 

Nakukunda

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
725
1,000
Kinachosikitisha lakini ni ukweli, NEC na CCM wamejipanga sana kudhurumu uchaguzi na Magufuli atatangazwa mshindi.
Kutangazwa atatangazwa kama jamaa wa Malawi....ila guarantee ya kuongoza itategemea reaction ya watanzania...CDM...vyombo vya kimataifa nk....

Na hali iliyopo hata system inaweza kumbetray....CCM kapandikiza chuki sana na hakuwaheshimu wazee ambao wengi ni wazee wa system...kumbuka kauli yake kuwa waache kiherehere.....

Pia angalia support waliyompa katika kampeni...refer maneno ya mama Maria Nyerere....

Magu ana wakati mgumu sana
 

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,157
2,000
1.Nenda kapige kura,

2.Jitoe kulinda kura au wawezeshe Mawakala

3.Shinikiza mshindi atangazwe,

Tutakuwa tumeifuta Ccm.
 

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
930
1,000
1. Tushikamane sote kuthibiti wizi wa kura vituoni na udanganyifu unaofanywa na wasimamizi wanaonunuliwa na ccm
2.Tusaidiane kuvielimisha vyombao vya dola kuwa watwndaji wake ni waajiriwa wa serikali, hivyo hata kikingia madarakani chama kingine ajira zao bado zitakuwa palepale
3.Tuwaelimishe wataz wote kujitokeza kumpigia kura mgombea wa upinzani mwenye maono mbadala wa ccm
4.Tuzidishe sala na maombi ili Mwenyezi Mungu awanyongonyeze wote waliopanga njama na hila za kujipatia uongozi isivyo halali
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,557
2,000
Wahutu wa Mpanda na Tabora wamtosa Magufuli Huu ulikuwa mtaji mkubwa wa CCM huko mishamo.

Lissu ni Ushindi mkubwa ambao haijawahi kuonekana
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,566
2,000
Hahahaha! Jamani CCM siyo TLP au NCCR mageuzi ya mbatia, CCM Ni mfumo na umejisimika kwa mikakati thabiti,

Tatizo nyie wapinzani hamjitambui, mnakubalije kuingia kwenye uchaguzi kwa tume mnayoamini Ni ya CCM?

Mimi upinzani naupenda ila approach zenu hazifai na hazina madhara yoyote kwa CCM.

Hata hivyo tusipepese macho, Lissu hawezi na Hana uwezo wa kuwa Rais wa JMT.
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,513
2,000
Mkakati mkuu ni kulinda kura zetu.

Sana sana kiti cha Urais.
Huko mita 200 kutoka kituoni,wakala wa chama chako ametia sahihi ya kukubali matokeo.
Unacholinda ni nini wakati wewe huoni kilicho mezani?
Kuna haja gani ya kuwa na wakala?
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
2,192
2,000
CCM itaendelea kuwepo hapa mpaka TADEA watakapokuwa chama kikuu cha upinzani..sasa hesabu itoke Chadema,ACT,NCCR,TLP,UDP,CHAUMA.......TADEA...Safari ni ndefu Makamanda hii syndicate ishakuwa ngumu kutafuta rudini ngome mkajipange.


October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM
JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom