Tupeane maujanja ya Excel

Mkuu kwa hiyo unanishauri nitumie program/application gani ili niweze kutuma meseji nyingi kutoka kwenye excel file?
Almost program zote huwa zinafanana majina (Bulk sms) tofauti ipo kwenye mmiliki wa software. India wapo vizuri sana kwenye haya mambo ila sometimes wanaboa kuwa na limitation ya nchi za kutumia program zao
 
Wewe unafanyaje mkuu??...
Hakuna trick yoyote, yani kiufupi Ms office kutokuwa activated sio issue na asilimia kubwa huwa wanatumia hivyo hivyo mana kila baada ya muda flani huwa inahitaji uiactivate tena na tena, sasa wengi tunapuuzia tu kwa sababu program inaendelea kutumika tu hivyo hivyo bila shida
 
Sasa kwa kesi yangu ya kushindwa kutype na kufanya changes mkuu ndio changamoto
 
Sasa kwa kesi yangu ya kushindwa kutype na kufanya changes mkuu ndio changamoto
Kama unatumia microsoft office ambayo haijawa activated unaweza ukaiactivate kwa kufata hizi hatua

This PC>>Local disc C>>program files (86)>>Common files>> Microsoft shared>>Officesoftwareprotectionplatform>>ospprearm.exe (right click, then run as an administrator). Baada ya hapo fungua file lolote la Microsoft office iwe ni Ms Word, Excel n.k utaona yale maandishi ya Activation Failed yamepotea, hapo itakuwa tayari iko activated
 
Shukrani mkuu, ngoja nijaribu hii alternative
 
Mkuu naona inaishia hapo, haifiki kwenye ospprearm.exe
 
Hiyo channel ya telegram mbona siioni?
 
Itakuwa umeclick mara moja, click mara mbili kama unaifungua
Nilijaribu kila namna lakini wapi!!!, Lakini Mungu ni mwema nikarestart computer (Restart & Update) baada ta masaa matatu hali ikatengamaa...Sahii nafanya tu kazi zangu....but still nahitaji kuijua hiyo njia just in case
 
Kama Kuna pdf nzuri zaidi ya kujifunzia hii excel pia from beginner to expect naomba nisaidiwe
 
Wakuu samahani Nina data zangu nimeweka za receipts Sasa tarehe niliyoweka hazijapangana kwa mpangilio nataka njia ya kufanya zijipange kutokana na tarehe na mwezi husika.
 
Wakuu samahani Nina data zangu nimeweka za receipts Sasa tarehe niliyoweka hazijapangana kwa mpangilio nataka njia ya kufanya zijipange kutokana na tarehe na mwezi husika.View attachment 2590648
Kwanza hakikisha tarehe zipo ktk format moja,select hiyo column ya tarehe yote,nenda Home>Format>Date, alafu chagua format ya tarehe unayoipenda,baada ya hayo ziarrange hizo tarehe kwa kusort,nenda Data kisha sort either kutoka tarehe kubwa kwenda ndogo au viceversa
 
Wakuu samahani Nina data zangu nimeweka za receipts Sasa tarehe niliyoweka hazijapangana kwa mpangilio nataka njia ya kufanya zijipange kutokana na tarehe na mwezi husika.View attachment 2590648
Select columns zote, then click Data tab hapo juu, then hapo kwenye Sort click hiyo A to Z
Hiyo ni incase kama date column ndio first column ktk table yako, next time unaweza ukawa unataka kusort the whole table lakini date column au column yoyote unayotaka kuitumia kufanya sorting ipo katikati au mwishoni so for this case utaclick hilo neno Sort, utaona kibox, utachagua column yako hapo kwenye "Sort by" (eg date column), then kwenye "Sort On" utaselect Values na kwenye "Order" utaselect "Oldest to Newest"
 
Nimejaribu naona inapanga only tarehe tu Hai consider mwezi
 
Kwa hiyo inachanganya za mwezi wa tatu na wa nne kisa zote ni tarehe the same au zinafatana ila mwezi imechanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…