naomba nami niunge hukoVLOOKUP nimeizungumzia Kwa clip fupi kule Telegram Sijajua kama upo kule..
Kiufupi sana.. VLOOKUP Hukuwezesha kutafuta kitu chochote katika Sheet Vertically ndani ya sekunde tu...
=VLOOKUP (D10,A1:F10,4,FALSE)
D10 hii ni CELL ambayo utakuwa ukiandika jina la hiyo item unayoitafuta so inategemea Unataka ionekane wapi katika Sheet yako
A1:F10 ni data zote ambazo Unataka ziwe considered ukiangalia vizuri nimeanza na A1 hadi F10 so lazima I select data zako zote
4 hii ni Column.. Je hiyo value au price ipo katika colum ya ngapi kutoka mwanzo?
FALSE ni kuwa jina utakalo liandika li match sawasawa na unachokitafuta ukiandika TRUE inaamana ikutafutie Value yeyote ambayo inakaribiana
Bonyeza Enter na Anza ku search items katika Cell D10
Hakikisha umeandika formula pale ambapo Unataka Jumla itokee... Andika kama inavoonekana Kwenye picha halafu bonyeza enter..
Rudia mara mbili Tatu utazoea.. Usisahau kuingia Kwenye Telegram nitakuwa naweka video fupi ili ieleweke vizuri
Asante Kwa Swali Lako Zuri.. Nimekuandalia Video fupi.. Nimeiweka Kwenye Group kule hakikisha umeingia... Nimejifunza swali lako lote.. Iangalie na fanya mazoezi na kama utakuwa na swali usisite kurudi hapa kuuliza
JINSI YA KUWEKA DROP DOWN LIST
Unaweza ukataka kuweka list ambayo mtumiaji anataka achague kitu fulani na ajaze kadiri ya matumizi yako...
Kitu cha kwanza andika list ya hizo items au majina katika sehemu yeyote katika Sheet yako
Nenda Kwenye Data >>> Data Validation kitatokea kibox kidogo... Bonyeza settings halafu nenda chini Kwenye Allow chagua list kama inavoonekana hapo chini
Baada ya hapo Kwenye source andika range ambayo hizo items ulizoziandika zipo.. Kwa Sheet yangu ni =$F$2:$F$6
Halafu bonyeza OK
mwisho sheet yako inatakiwa ionekane hivi
View attachment 436363
Kama data umezipanga vizuri tumia Vlookup functionJaman wataalamu kuna tatizo moja naomba msaada.
Nina mafaili mawili; yote yamekosewa
Faili la kwanza nimechanganya watu waliopo na wasio kuwepo na namba zao za simu.
Faili la pili lina watu waliopo tu ila hakuna namba zao za simu nawezaje kurekebisha kwa haraka badala ya kupitia kila jina?
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukatuma screen shot nikusaidie? hapa au PM?Jaman wataalamu kuna tatizo moja naomba msaada.
Nina mafaili mawili; yote yamekosewa
Faili la kwanza nimechanganya watu waliopo na wasio kuwepo na namba zao za simu.
Faili la pili lina watu waliopo tu ila hakuna namba zao za simu nawezaje kurekebisha kwa haraka badala ya kupitia kila jina?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nina kitambo mkuu sijapata notification yoyote telegram kwenye group kule. Ama ni mimi tu!?