Tupatiwe Kanuni za bunge

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
974
Waheshimiwa,

Kesi ya Zitto Kabwe mwaka juzi ilileta ubishi pale aliposimamishwa kwa kanuni za bunge. Pamoja kwamba tulibishana nchi nzima lakini Anna Makinda kama naibu spika alitetea kwamba kanuni za bunge zilifuatwa kumsimaisha Zitto.

Anna Makinda wakati ule alisisitiza kwamba inabidi wananchi waonyeshwe kanuni za bunge zinasemaje. Statement ambayo ameirudia juzi kwamba atahakikisha tunazielewa kanuni za bunge ili kusiwe na ulalamishi.

Sisi kutokuwa nazo, ni kwa sababu wengi hatutegemei kuwa wabunge na hivyo ikaonekana kama zinawahusu wabunge tu wala hazituhusu sisi.

Kwa mfano kanuni zitatufungua macho kwamba, je, spika akiamua kutumia ubabe kuwanyima baadhi ya wabunge uhuru wa kuuliza anawajibishwa vipi au nini kifuate baada hapo?

Je, spika akiamua binafsi kuzuia hoja binafsi ya mbunge isijadiliwe bungeni awajibishwa na kanuni ipi?
Hayo ni baadhi tu ya yaliyo gizani mwangu. Wengine mnaweza kuchangia kudhihirisha ni giza gani tulilomo bila kuwa na kanuni hizo.

Hata wabunge wakijua kwamba wananchi tumeanza kuzidai na kisha tukaziimba kanuni zao vilivyo basi hata waliodhani kuondoka kwa Samwel Sitta kuna unafuu kwao basi wamenula wa chuya.

Hivyo anayeweza kutusaidia kanuni hizo basi aziweke hapa wazi wengine tuanze kuzitumia. Wengine tunaweza kuzisoma mradi tu tukiziona na si lazima Anna Makinda au yoyote atufundishe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom