Tuongelee Njaa, hivi imeisha?

Tuongelee Njaa, hivi imeisha?

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,693
Kila kona unakuta post za Makonda na Madawa. Sasa hizi zimetukinai bahna. Hebu tuongelee ile mada yetu pendwa ya mlo. Hivi njaa imeisha? Leo nimenunua debe kwa 25000. Nyie uko mlipo bei ya mahindi imepanda imepungua?

Mchele bei imepaa hadi 2400. Vip uko nyie?


Na bei ya gesi imepanda. Mtungi wa 18000 sasa ni 22000. Haya yote yametokea hiki kipindi cha mziki wa makonda ukiwa umeshika chat.
 
Uko sahihi. Hii ya Makonda imeletwa kuzima ajenda za kitaifa za njaa na elimu.

Ila na wewe usije ukabambwa kwa uchokozi na uchochezi
 
Kila kona unakuta post za Makonda na Madawa. Sasa hizi zimetukinai bahna. Hebu tuongelee ile mada yetu pendwa ya mlo. Hivi njaa imeisha? Leo nimenunua debe kwa 25000. Nyie uko mlipo bei ya mahindi imepanda imepungua?

Mchele bei imepaa hadi 2400. Vip uko nyie?
unazungumzia njaa au bei za vyakula?
 
Ebwana njaa ipo, labda tu haijakolea ndo maana viongozi wanakanusha kirahisirahisi. Juzi nimesafiri toka DSM kwenda Musoma aisee hali niliyoiona hapo njiani kuanzia Singida, Shinyanga huko, Mwanza, Bunda ndo kabisaaaa. Vitu vimeota na mvua zikakata vikiwa katikati na vingine vichanga kabisa. Viongozi wanabisha bure tu, bora kukiri uwepo wa tatizo ili tuanze mapema mikakati ya kkukabiloan nalo kabla watu hawajaanza kufa. Njaa ipo, tena ipo Mubashara
 
We mbona mbishi.

Msukuma kishasema hakuna njaa.
 
Supply bana sio bei.
The higher supply,the lower prices and vice versa
Hivi nyie izo shule ndzo zinawafunza ujinga au. Unashindwa hata kurelate laws of demand and supply kudetermine price?

Mwaka jana kuna kipind kulikuwa na mafuriko ya nyanya mpaka tenga lilifika mia tano. Leo hii tenga ni 50,000. Ni kwanini inakuwa hivi.

Ishu ni kuwa sasa nyanya zimepanda bei. Kama ulikuwa unatumia nyanya 5 leo utatumia mbili ili kuendana na hali ilivyo.

Hivyo hivyo kwenye bei ya nafaka. Bei inapopanda sio kuwa walaji wameongezeka ni kuwa supply imeshuka. Sababu ya soko huria bei hupanda ili kubalane. Kama ulikuwa unafamilia wanakula debe kwa wiki leo watakuwa wanakula debe kwa siku kumi. Huu ni uhaba wa chakula. Maana yake ni njaa. Sio lazma mpaka watu wafe ndyo mseme kuna njaa
 
Watanzania kwa mbwembwe ni hataree.
Hivi hata kubaini kama kuna njaa au la kunahitaji mabishano ya kutumia elimu za kwenye vitabu, mara demand, mara sijui supply?
Halafu hao wanaobishana utakuta hakuna hata mmoja mweye shamba la kuzalisha chakula cha kula walau yeye na familia yake kwa mwaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom