TUONGEE KIUME: Ndoa ingekuwa mtu ingefanana hivi

TUONGEE KIUME: Ndoa ingekuwa mtu ingefanana hivi

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,536
Reaction score
3,885
Watafute watu kadhaa walio kwenye ndoa, mathalani watu 10 hivi.

Kisha waambie unataka kuumba mtu mwenye taswira ya kufanana na ndoa, hivyo wakusaidie kupata picha kwamba mtu anayefanana na ndoa anaweza kuwa anaonekanaje?

Niamini mimi, utaumba mtu mbaya kiasi kwamba kama marehemu, gwiji wa muziki wa Tanzania Dk Remy Ongala angekuwa hai, angesimama mbele ya vyombo vya habari na kutangaza kuacha kujinasibu kuwa ana sura mbaya kuliko wote.

Kwa nini? Kwa sababu leo hii tunaishi katika dunia ambayo kila mtu anayeongea kuhusu ndoa anaizungumzia kwa taswira za kutisha.

Mama, bintiye anapoolewa atamwambia; mwanangu, ndoa si lelemama, ina changamoto nyingi sana, misukosuko, ugomvi, purukushani na makorokoro ya kila namna, kwa hiyo inahitaji uvumilivu wa kiwango kikubwa sana.

Baba naye, wakati kijana wake anaoa atamuelezea ya kufanana na hayo. Mwanangu ndoa ngumu, wanawake wana matatizo mengi, kuishi nao kunahitaji moyo wa kustahimili na akili kubwa sana, changamoto ni nyingi.

Watu hawa wawili wakikutana ndani ya nyumba ni kama Chadema na CCM kama sio Simba na Yanga, upinzani wa kufa mtu. Kila mtu kwa nafasi yake akili yake imejazwa habari hasi kuhusu ndoa.

Habari hasi ambazo kimsingi zinaweza kuwa za kweli, lakini zinasemwa sana, kiasi kwamba ndoa inaonekana lazima iwe hivyo tu. Kwamba kuwa na furaha ndani ya ndoa.Mungu wangu, huo ni muujiza.

Lakini ni kweli iko hivyo? Au labda kwa misingi ya kidini tuseme Mungu aliamuru tuoane ili iwe kama adhabu kwa Adamu na msaidizi wake Hawa ya kuyapinga maagizo pale Edeni, sitaki kuamini.

Imani yangu ni kwamba ndoa inastahili kuwa tulizo kubwa kuliko kawaida, inastahili kuwa kimbilio kuu kwa mwanandoa mmoja anapopata matatizo mazito.

Mke akikumbwa na janga akimbilie kwa mumewe, akumbatiwe vizuri tu na kwa upole apewe maneno ya kutia nguvu na kuibua upya imani yake.

Na ni hivyo kwa mume pia, purukushani anazokumbana nazo siku nzima ziyayushwe kama barafu juani kwa upendo wa daraja la juu sana kutoka kwa mkewe.

Ndoa haistahili kabisa kuwa namna ambayo watu wengi wanaifikiria kwamba ni ngumu. Labda tuamue, tuseme sisi ndiyo wagumu. Tusiipake matope ndoa.

Hata nakumbuka kuna kichekesho kimoja kuhusu ndoa, tuliwahi kukiongelea hapa hapa. Kwamba mwanaume akifa, akiwa mbinguni, kitu cha kwanza kuulizwa kabla ya kupimiwa dhambi zake ni kwamba Je duniani ulikuwa umeoa?

Jibu likiwa ndio, Mungu atasema “mpelekeni peponi moja kwa moja mtu huyu. Moto alishaupata huko huko duniani.
Hapana, ndoa haistahili kuwa moto bali kinyume chake. Yaani pepo.
 
Wanandoa kujeni uku mtuambie ukweli wa maneno yanayosemwa juu ya ndoa.
 
Unasema Dr Ongalla alikuwa mbaya kwa vigezo gani..?

Acha dharau kwa marehemu, ameacha legacy kuliko wewe na ‘uzuri’ wako. tumia mfano halisi kuelezea huo ubaya wa ndoa ulioukusudia.
 
Unasema Dr Ongalla alikuwa mbaya kwa vigezo gani..?

Acha dharau kwa marehemu, ameacha legacy kuliko wewe na ‘uzuri’ wako.... tumia mfano halisi kuelezea huo ubaya wa ndoa ulioukusudia.
Kama ungejua maneno ya nyimbo yake mojawapo, wala usingeuliza kigezo gani.
 
Kha! Kwa staili hii nitaoa kweli!! Yani ndoa inasura mbaya kushinda ya naniliu!.. duh!
 
Ndoa haijabadilika ila wanandoa ndio hubadilika. Mume haridhiki na mkewe na hapo ndio uchokozi huanzia. Kama sote tungelikuwa bikira yaani mimi simjui mwanamke mwingine yeyote na mke wangu hamjui mwanamume mwingine yeyote yule nadhani tunge heshimiana sana.
Tatizo letu; Huyu mke wangu sijui ni wa ngapi katika orodha niliyo wahi kutembea nao. Sasa mimi nikatamini nimkute akiwa bikira. Wadhani hiyo ni haki?? Hao niliwatenza wao hawakuwa watu?? Basi nikakubali kuwa; Nalipa nilichofanyia wengine.
Nilipomleta ndani, nikaanza kukutana na ma X wangu. Kila mtaa, kila mji na wote wanataka tupashe kiporo. Nami nikashindwa kusema"Sili kiporo". Uaminifu nikavunja. Sasa siwezi muamini hata huyu mke wangu.
All in all, sisi warume ndo wabadirifu wakubwa wa ndoa. Tusilaumu ndoa bali tujilaumu sisi warume
 
Wanaume bana anataka yeye awe anapasha viporo na kuchovya nje
Nyumbani anarudi kachoka anatoa show ya kichovu afu bado ategemee mke utulie?..tuliii?...
 
Wanaume bana anataka yeye awe anapasha viporo na kuchovya nje
Nyumbani anarudi kachoka anatoa show ya kichovu afu bado ategemee mke utulie?..tuliii?...
Nimesema; Sisi warume tunatamani hata yule wa miaka 47 iliyopita, nikikutana naye, aniheshimu na kutoa nguo hapo hapo hata barabarani. Ndivyo tulivyo. Ila weye bibiye, nisikuone unapita hata umepanda boda mbele yangu na jamaa yako anayekulisha. Huo ndo wivu wa virume. We tulia hapo chumbani tu uombe mechi yako asubuhi kabla ya wenzako.
 
Nimesema; Sisi warume tunatamani hata yule wa miaka 47 iliyopita, nikikutana naye, aniheshimu na kutoa ngua hapo hapo hata barabarani. Ndivyo tulivyo. Ila weye bibiye, nisikuone unapita hata umepanda boda mbele yangu na jamaa yako anayekulisha. Huo ndo wivu wa virume. We tulia hapo chumbani tu uombe mechi yako asubuhi kabla ya wenzako.
Zama hizi mtalia sana
Unavoenda kushughulikia wa mwenzako mchana wako pia anashughulikiwa na mwingine

Jioni kila mtu no stress
 
Zama hizi mtalia sana
Unavoenda kushughulikia wa mwenzako mchana wako pia anashughulikiwa na mwingine

Jioni kila mtu no stress
Ila samahani kwa neno hili kuwa; Miye namwagia kwako unabaki nayo , huoni vibaya kuileta nyumbani kwetu uliyo mwagiwa huko?? Mwanamke, kabla hujaamua kumkomesha mumeo kwa kwenda nje, jitambue kuwa mwenye kuleta balaa ni weye
 
Kuna kumwaga nje na hainaga makombo hata kama imemwagwa ndani...
Balaa mnalianzisha wanaume yanini kujifia wkt hata mi natongozwa
 
Ndoa Ina raha yake kama utamfanya mke wako ndio mtu wako wa karibu zaidi
Ishi kwa furaha zote hiyo hela unayoitumia kwa mambo yako ya anasa peke yako ichange na mwisho wa mwaka nendeni holiday hata Mombasa au nchi yoyote ile mkale bata

Pata ushauri kwake kwani kuna mengi binadamu hatuyajui lakini wengine wanayajua, na kuwa faida kwenu pamoja
Tumia mda wako baada ya kazi kwa kukaa pamoja na kubadilishana mawazo
Furaha itawale kila wakati
Kama utakuwa una double life huo ni mtihani mkubwa sana na daima hiyo itakuwa ndoa ya matatizo kwani utakuwa na wasiwasi tu kila wakati
Kupanga ni kuchagua

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
ndoa ni nzuri kama familia hazitaingilia. Kama tukiwachukulia wanawake kama wanadamu wenzetu kuwa wana hisia, wanachoka pia, wana mahitaji etc.
Uchumi pia husababisha ndoa nyingi kuyumba, huwa hakuna uvumilivu kama uchumi ukiyumba.
Hakuna uvumilivu kama familia moja wapo inaiona nyingine haifai
Hakuna ndoa kama Mungu hayupo kati ya wana ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom