Tuombeane wakuu huyu Corona analeta wenge hatari

Uko sahihi mkuu sasa sijui itakuaje kwa hyo ukisikia hata kichwa kinauma inabid ujifungie ndani..? Wengine ukijifungia unakufa na njaa badala ya Futa
Huko unakotembea tembea,utaua wengine. Fikiria sawa na kuwachinja. Fikiria kuanzia pale ulipojitambua tu usingeenda bar,ungejifungia. Huku ukiletewa unachohitaji humo kwa tahadhari,yakiwemo hayo malimao na tangawizi. Mazoezi fanyia ndani. Fikiria umesema unaenda sauna. Huko nako utakutana na wengine ambao hawana uwezo wa kinga kama zako siku kadhaa mbele utamsikia amekufa. Muda mwingine utakuja kuhisi kuhisi kabisa ni wewe ulimwambukiza siku uliyoenda pale,itabaki milele kwenye kumbukumbuku yako. Huu ugonjwa ukijitambua ni vizuri sana uwalinde na wengine kwa kujitenga nao. Kibaya zaidi utakaemwambukiza hana kinga kama yako,yeye anaweza akafariki

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuna sehem nimesema apa nilipo nimelala kitandani niko hoi...! Nimepost ili ku share nilichopitia na ninachokipitia mpka nimepost ujue bado uzima upo..! Sauna ipo ndio na ndo naelekea mda huu

Sent using Jamii Forums mobile app
On a serious note, hizo zote ni dalili mkuu don't take it lightly,endelea kukaza na hizo malimao, tangawizi, vitamin c na makorokoro mengine utakayoshauriwa na wadau walio pitia. Why bother kwenda sauna while unaweza kamata mentho vicks ukapiga sauna yako home. Kila la kheri mkuu,uwe mzima.
 
Uko sahihi mkuu sasa sijui itakuaje kwa hyo ukisikia hata kichwa kinauma inabid ujifungie ndani..? Wengine ukijifungia unakufa na njaa badala ya Futa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna namna mbili tu ya kufanya. Ukijisikia dalili mojawapo kati ya zile za (FUTA kwa sauti yako). Moja nenda hosp moja kwa moja na kule unawaeleza unavyojisikia huku ukiwalinda wasikukaribie. Kule watakupa ushauri namna ya kufanya. Kupelekwa amana mimi mwenyewe siungi mkono,huko kataa. Mbili ukijitambua una dalili kama uko kwako,chukua chumba kimoja kwa ajili ya wewe,waambie unayojisikia. Kama umepanga na nafasi ni ndogo,hapo ujue wewe na mkeo lazima mkubaliane jambo,lazima akuachie chumbani ili usimwambukize,msije mkaumwa wote asiwepo wa kumhudumia mwenzie. Sasa hapo unasema unaenda sauna,huoni utawaambukiza wengine?. Kwa nini usifukize tu mwenyewe na mwarobaini nyumbani ili kuwalinda wengine. Huu ugonjwa ajabu yake ni moja,yule utakaemwambukiza anaweza akafa,halafu wewe ukapona. Pole,utapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naitafuta wiki ya pili sasa sijui ni huyu mdudu Futa amebisha hodi kwangu au ni nini ilianza kama homa hvi ya jion nikawa naipuuzia nikidhani ni uchovu tu.

Jumapili iliyopita siku hyo nilikua nimeshinda garage nikatoka nimechelewa ikabid nipite Bar nimalizie wkend ila mwili nikawa bado siuelewi vizuri ikanibid nijisogeze tu home.

Usiku nimelala nilishikwa na homa Kali sana ila dalili zote ni kama malaria nilikaza mpka asubuhi ila niko hoi sana nikaenda duka la dawa nikanunua single dose ya malaria malafin baada ya kuinywa mpka imefika jion nikahis mwili unakua sawa ila usku homa ikajirudia na mafua juu.

Aisee hlo wenge nikajua hii ni Futa ina fuatilia maisha yangu ndani nilikua na Dr cold nikapiga moja usku huo nikatoboa ... Rasmi nika anza kupiga dozi ya malimau mixer tangawizi nika anza kufanya na mazoezi tangu juzi nimepoteza uwezo wa kunusa kabisa lakin ladha mdomoni bado ipo Jana nimejifukiza kidogo nasikia mwili unapata nafuu na Leo nataka niende sauna nipigwe mvuke.

Nina maswali najiuliza hizi ndo dalili za mwanzo za covid au? Je kila Mtu ana dalili zake kulingana na uimara wa kinga mwili yake? Mimi viungo vya mwili haviumi ...na kifua hakijabana kwenye upumuaji sijapata shida japo kuna mda pua zinabana na kuachia homa inakuja ila haina nguvu sana..ila chafya kama zote.

Nina uncle yangu alipata huyu mdudu Futa alilazwa siku tano badae akakaa sawa ananihimiza sana niende kupima ananiambia hizi elimu za mtaani kuhusu huu ugonjwa kama kujifukiza matumizi ya limau na tangawizi ni hatari kwa afya zetu anasema suluhisho lipo hospital...!

Tupeane updates wanaopitia dalili mbalimbali za mdudu Futa Korie.
Muulize uncle yeye hospital alitumia /alipewa dawa gani ya FUTA!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mrembo hebu nichanganyie huo mseto halafu unipe
Mimi nimetengeneza leo.
20200514_151356.jpg
 
Back
Top Bottom