Tuombeane wakuu huyu Corona analeta wenge hatari

Mzee Shirimaa

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
1,539
3,440
Naitafuta wiki ya pili sasa sijui ni huyu mdudu Futa amebisha hodi kwangu au ni nini ilianza kama homa hvi ya jion nikawa naipuuzia nikidhani ni uchovu tu.

Jumapili iliyopita siku hyo nilikua nimeshinda garage nikatoka nimechelewa ikabid nipite Bar nimalizie wkend ila mwili nikawa bado siuelewi vizuri ikanibid nijisogeze tu home.

Usiku nimelala nilishikwa na homa Kali sana ila dalili zote ni kama malaria nilikaza mpka asubuhi ila niko hoi sana nikaenda duka la dawa nikanunua single dose ya malaria malafin baada ya kuinywa mpka imefika jion nikahis mwili unakua sawa ila usku homa ikajirudia na mafua juu.

Aisee hlo wenge nikajua hii ni Futa ina fuatilia maisha yangu ndani nilikua na Dr cold nikapiga moja usku huo nikatoboa ... Rasmi nika anza kupiga dozi ya malimau mixer tangawizi nika anza kufanya na mazoezi tangu juzi nimepoteza uwezo wa kunusa kabisa lakin ladha mdomoni bado ipo Jana nimejifukiza kidogo nasikia mwili unapata nafuu na Leo nataka niende sauna nipigwe mvuke.

Nina maswali najiuliza hizi ndo dalili za mwanzo za covid au? Je kila Mtu ana dalili zake kulingana na uimara wa kinga mwili yake? Mimi viungo vya mwili haviumi ...na kifua hakijabana kwenye upumuaji sijapata shida japo kuna mda pua zinabana na kuachia homa inakuja ila haina nguvu sana..ila chafya kama zote.

Nina uncle yangu alipata huyu mdudu Futa alilazwa siku tano badae akakaa sawa ananihimiza sana niende kupima ananiambia hizi elimu za mtaani kuhusu huu ugonjwa kama kujifukiza matumizi ya limau na tangawizi ni hatari kwa afya zetu anasema suluhisho lipo hospital...!

Tupeane updates wanaopitia dalili mbalimbali za mdudu Futa Korie.
 
Tuache hayo yote ungeumwa usingepata nguvu ya kupost.....nikuulize hv bongo kuna sauna?
 
....
_joy__joy__joy__joy_mna%20wafahamu%20-%20WAJUMBE%20%20hawa__!%20vipi%20TUENDELEE%20NAO%20au%20...jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuache hayo yote ungeumwa usingepata nguvu ya kupost.....nikuulize hv bongo kuna sauna?
Kwani kuna sehem nimesema apa nilipo nimelala kitandani niko hoi...! Nimepost ili ku share nilichopitia na ninachokipitia mpka nimepost ujue bado uzima upo..! Sauna ipo ndio na ndo naelekea mda huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
P

Poa mzee ila ungefanya poa ka ungemsikiliza mjomba mzee kuliko kutegemea majibu ya jf..koz tayari anaexperience
 
Naitafuta wiki ya pili sasa sijui ni huyu mdudu Futa amebisha hodi kwangu au ni nini ilianza kama homa hvi ya jion nikawa naipuuzia nikidhani ni uchovu tu.

Jumapili iliyopita siku hyo nilikua nimeshinda garage nikatoka nimechelewa ikabid nipite Bar nimalizie wkend ila mwili nikawa bado siuelewi vizuri ikanibid nijisogeze tu home.

Usiku nimelala nilishikwa na homa Kali sana ila dalili zote ni kama malaria nilikaza mpka asubuhi ila niko hoi sana nikaenda duka la dawa nikanunua single dose ya malaria malafin baada ya kuinywa mpka imefika jion nikahis mwili unakua sawa ila usku homa ikajirudia na mafua juu.

Aisee hlo wenge nikajua hii ni Futa ina fuatilia maisha yangu ndani nilikua na Dr cold nikapiga moja usku huo nikatoboa ... Rasmi nika anza kupiga dozi ya malimau mixer tangawizi nika anza kufanya na mazoezi tangu juzi nimepoteza uwezo wa kunusa kabisa lakin ladha mdomoni bado ipo Jana nimejifukiza kidogo nasikia mwili unapata nafuu na Leo nataka niende sauna nipigwe mvuke.

Nina maswali najiuliza hizi ndo dalili za mwanzo za covid au? Je kila Mtu ana dalili zake kulingana na uimara wa kinga mwili yake? Mimi viungo vya mwili haviumi ...na kifua hakijabana kwenye upumuaji sijapata shida japo kuna mda pua zinabana na kuachia homa inakuja ila haina nguvu sana..ila chafya kama zote.

Nina uncle yangu alipata huyu mdudu Futa alilazwa siku tano badae akakaa sawa ananihimiza sana niende kupima ananiambia hizi elimu za mtaani kuhusu huu ugonjwa kama kujifukiza matumizi ya limau na tangawizi ni hatari kwa afya zetu anasema suluhisho lipo hospital...!

Tupeane updates wanaopitia dalili mbalimbali za mdudu Futa Korie.
Duuuh Mkuu kwa maelezo yako hayo ni FUTA hilo.....Pole sana ila kunywa dawa kiholela ni hatari sana usijaribu tena.kuna dawa nyingine zinaleta reaction kama ukiwa na ugonjwa mwingineambayo ni hatari(life threatening).

Kwa mfano kama una sukari ukaja kupigwa dripu ya quinine lazima ung'ate shuka.
 
Kubana kifua inaweza kutokea siku saba mpaka kumi tangu uanze kuona dalili za mwanzo. So anza kufanya mazoezi ya kupumua ili kuweka sawa mapafu pamoja na mbavu. Ingia YouTube utaona jinsi ya kufanya zoezi la kupumua kwa wagonjwa wa covid 19.
 
Huko unakotembea tembea,utaua wengine. Fikiria sawa na kuwachinja. Fikiria kuanzia pale ulipojitambua tu usingeenda bar,ungejifungia. Huku ukiletewa unachohitaji humo kwa tahadhari,yakiwemo hayo malimao na tangawizi. Mazoezi fanyia ndani. Fikiria umesema unaenda sauna. Huko nako utakutana na wengine ambao hawana uwezo wa kinga kama zako siku kadhaa mbele utamsikia amekufa. Muda mwingine utakuja kuhisi kuhisi kabisa ni wewe ulimwambukiza siku uliyoenda pale,itabaki milele kwenye kumbukumbuku yako. Huu ugonjwa ukijitambua ni vizuri sana uwalinde na wengine kwa kujitenga nao. Kibaya zaidi utakaemwambukiza hana kinga kama yako,yeye anaweza akafariki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom