Tunza chupi wewe dada

DR SANTOS

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
10,513
21,404
ITUNZE CHUPI YAKO IMEBEBA MAANA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YA NDOA

IMEANDALIWA NA SANTOS AMAN MWAKOMO

Pole na majukumu ya hapa na pale, natumai u mzima wa afya nami vivyo hivyo.
Leo nimependa kulizungumzia hili, kwani suala la ndoa kwa sasa limekua ni kama, uhusiano uliopo kati ya pilipili na macho, yaani asilimia kubwa ya watu huona ndoa ni chungu, na wengi hawafurahiii maisha ya ndoa kabisa. Unajua kwanini?

Hivi ulishawahi fikiria mwanaume anajifikiriaje pale anapokutana na wewe kimwili kwa mara ya kwanza, na kukuta umeshatumika?
Basi jibu ni hili;
Mwanaume humshusha thamani moja kwa moja na kumuona mwanamke ni wa kawaida sana
Mwanaume hupoteza imani na mwanamke aiamini anaweza kupigwa muda wowote na Yule aliyefungua njia.
Mwanaume huumia sana na kuamua kutafuta faraja nje ya ndoa, na hapo ndipo suala la michepuko huanza.
Hivi jaribu kufikiri, mwanaume aliyekuhangaikia kwa miaka takribani miwili na umekua ukionesha ugumu hasa pale anapokuomba mshiriki tendo la ndoa katika kipindi cha uchumba wenu lakini yeye amekua akikujali kwa kila kitu ikiwemo kukutimizia mahitaji ambayo umekua ukimuomba mfano nguo pesa nk
Licha ya hivyo akakulipia na mahali, akakutoa kwenu na kukupeleka kwake, na kukufanya ujisikie furaha na ujione una thamani kuliko wanawake wote, duniani kwani si wote wanakamilisha maandiko
Ya kwamba
”mwanaume atawaacha wazazi wake na ataongozana na mwanamke kwenda kuanza maisha yake”.( Namaanisha ndoa)

Leo hii anakuja kuona umesha tumika, leo hii anakuja kuona umeshindwa kuitunza chupi yako kwa kumpa mtu mwingine kabla ya ndoa
Kwanza atajiuliza, hivi ni kitu gani alichokua ananibania kabla?
Na mara nyingi maswali hayo hukosa majibu pia hutengeneza jeraha lamoyo ambalo halitakaa lifutike kwani atakua akikumbuka kila anapokuona na hapo matatizo huanza katika ndoa
Mfano
Ugomvi usio na sababu
Ulevi
Pamoja na dharau

Umewahi kujiuliza ni furaha anayoipata mwanaume pindi anapofanya mapenzi na wewe na kukukuta ukiwa bikira?
Kwanza inamjengea uaminifu mwanaume, kuamini kwa asilimia 200, kwani takwimu zinaonesha
“mwanamke uliyemtoa bikira ana asilimia 89% za kutoka nje ya ndoa mkikutana, hata iwe umemtoa miaka kumi iliyopita”.

Jamani hebu tuzitunze chupi zetu, sasa unakuta dada wa miaka ishirini amezaa na aliyezaa nae tayari ameoa, hebu ifike wakati tujionee huruma, pia tukionee huruma kizazi chetu

Nimalize nikisema hebu tuzitunze chupi zetu wakati wake utafika tu wa kuzivua na ikiwezekana kulala bila nguo.

Santos aman mwakomo
 
Back
Top Bottom