Tunduma: Mbunge Frank Mwakajoka akamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya

Kawapiga picha madiwani waliojiunga na CCM kisha kusambaza kwenye mitandao na kuhamasisha siasa chafu
Nieleze kuna siasa gani chafu kuonyesha watu ambao siyo madiwani tena, lakini wanahudhuria vikao vya madiwani vya kibajeti. Elimu ni ufunguo wa maisha ebu nipe shule kidogo kwenye hilo.
 
bdce08ddffd45403c320455d1994f923.jpg


Mbunge wa CHADEMA katika jimbo la Tunduma, mkoani Songwe, Frank Mwakajoka amekamatwa na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa amri ya mkuu wa wilaya Juma Said.

Mwakajoka ameswekwa rumande baada ya kuwapiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, madiwani watatu wa Chama hicho waliojiengua na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanadaiwa kupigwa picha na Mwakajoka, ni Ayob Mlimba ambaye alikuwa diwani wa Kata ya (mwaka kati), Simon Mbukwa (Kaloleni), na Amos Nzunda (Mpemba).

Taarifa zinasema, tukio hilo lilitokea wakati madiwani hao walipoitwa na serikali kuhudhuria kikao cha bajeti cha Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, leo Jumatano.

"Hawa watatu wa nyuma ndio waliokuwa madiwani wetu wa CHADEMA na ambao wamejiuzulu nafasi zao. Lakini leo wameitwa kwenye kikao cha bajeti ya Mji, huku wakiwa wamehama chama na kujiuzulu nafasi zao za udiwani", ameeleza Mwakajoka katika moja ya ujumbe wake kwa wabunge wenzake.

Muda mfupi baadaye, mbunge huyo anaandika " Na sasa nawekwa chini ya ulinzi na pia nakaa ndani kwa saa 48 kwa amri ya (DC mkuu wa wilaya)", aliandika mbunge huyo Mwakajoka.
Mkuu kwa ajili ya kumbukumbu naomba uweke vizuri majina yote matatu ya huyo DC .
 
Nieleze kuna siasa gani chafu kuonyesha watu ambao siyo madiwani tena, lakini wanahudhuria vikao vya madiwani vya kibajeti. Elimu ni ufunguo wa maisha ebu nipe shule kidogo kwenye hilo.
DC wa Tunduma ambaye pia ni Mungu wa eneo hilo kaamua , hii nchi inatia aibu sana ! Yaani Madiwani wamenunuliwa wamejivua nyadhifa zao , halafu leo wanahudhuria vikao ambavyo waliviacha , unawapiga picha halafu unakamatwa !

Hii amani si tu inachezewa kwenye tundu la choo , bali ilishatumbukia chooni , nchi imefika patamu sana !
 
Masaa 48! Picha!Mbunge! Kuna watu wanatafuta mkuki wa makalioni wawape watu lawama
 
Back
Top Bottom