Tundu Lissu: Spika Ndugai na watu wake wamelipa mshahara wangu wa tangu Januari hadi Machi waliokuwa wameuzuia kiharamia

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
HABARI NJEMA KUTOKA KWA HON. TUNDU LISSU

Hello bandugu wapendwa,

Nawasalimuni kwa upendo tele na heshima kubwa. Natumaini Mungu wa Haki amewajalia afya na kila lililo jema. Ni stahili yenu.

Naomba nianze kwa kuwatakia kila la kheri katika wakati huu wa Wikiendi ya Pasaka.

Pili naomba niwape mrejesho kuhusu 'ugomvi' wangu na Spika Ndugai na watu wake juu ya mshahara wangu.

Pamoja na kwamba Spika Ndugai amesikika akisema kuwa mambo ya mshahara ni siri ya Bunge na Mbunge husika, na yanatakiwa kujadiliwa 'chumbani' na sio 'sebuleni', nadhani ni vizuri tukafunga mjadala huu kama ulivyoanza: hadharani!!!

Kwa kifupi ni kwamba Spika Ndugai na watu wake wamelipa mshahara wangu wa tangu Januari hadi Machi waliokuwa wameuzuia kiharamia tu.

Kwa maoni yangu, kilichowafanya wakubali yaishe ni ujasiri wenu, na wa watu wengine wengi, mlioamua kunichangia, sio tu gharama za matibabu yangu, bali hata huo mshahara uliozuiliwa kinyume na Sheria na Kanuni za Bunge.

Kama walivyotaka nife kwa kukosa matibabu, watu hawa walitaka nife njaa kimya kimya kwa kuninyang'anya mshahara wangu.

Sikukubali kufa kimya kimya na ninyi ndugu zangu hamkukubali. Walipoona sokomoko la mshahara wangu limekuwa kubwa na sasa limebebwa na wananchi wakakubali yaishe. Nawapongezeni sana kwa ushindi huu.

Hili ni funzo kubwa sana kwa kila mmoja wetu. Tusikubali kukaa kimya tunapoonewa. Hakuna fedheha yoyote katika kupiga kelele za kudai haki. Tupaze sauti zetu na kupiga kelele, watu wema watasikia kilio chetu na tutapata msaada.

Hakuna busara yoyote ile katika kukubali kunyongwa kimya kimya na wasio na haki. Christopher Okigbo, mshairi maarufu wa Nigeria ya wakati wa Vita ya Biafra, aliandika: "The man died who keeps silent in the face of oppression."

La tatu linahusu afya yangu. Na kwenye hili habari ni njema sana. Tarehe 2 ya mwezi huu nilikutana na madaktari wangu kwa appointment ya kwanza tangu operesheni za tarehe 20 Februari.

Taarifa yao ni kwamba mfupa wote wa mguu wa kulia umepona vizuri. Sehemu iliyowekewa 'kiraka' cha mfupa na kupigwa 'ribiti' ya chuma juu kidogo ya goti; na sehemu ya kwenye paja iliyotakiwa kuota mfupa mpya, zote ziko vizuri.

Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kukunja goti na kujifunza kutembea tena. Naomba mniamini nikisema kujifunza kutembea tena, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kulala kitandani, ni kazi ngumu sana!!!!

Nafikiri sina tofauti sana na mtoto mdogo anayejifunza kupiga hatua zake za kwanza. Lakini pole pole nitafika inshaallah.

Tarehe 14 ya mwezi ujao nitapimwa urefu wa miguu ili nitengenezewe kiatu au soli maalum kwa ajili ya mguu wa kulia.

Kwa sababu ya majeraha makubwa niliyopata, mguu huo ni mfupi kwa sentimita kadhaa. Bila kiatu au soli maalum nitakuwa 'langara' sana na madaktari wamesema hiyo sio sawa sawa.

Kwa kumalizia, sasa nina tarehe ambayo madaktari wangu wamesema nitakuwa 'fiti' kurudi nyumbani.

Msiniambie niiseme kwa wakati huu. Tunahitaji kushauriana na wadau mbali mbali kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwangu nyumbani.

Tukumbuke tu kwamba waliotaka kuniua mchana kweupe katikati ya mji wa Dodoma bado wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Itabidi tupate 'security guarantees' kutoka kwa wahusika, Serikali ya Magufuli na Jeshi la Polisi, kwamba nitakuwa salama nikirudi.

Kwa hiyo, wakati muafaka utakapofika, hopefully sio mbali sana, nitawaeleza tarehe kamili ya kurudi nyumbani na, kwa mlioko Dar, nitawaomba mniandalie supu ya utumbo wa mbuzi Rose Garden kwa Mzee Assey!!!

Wasalaam
TL

SHARE ZAIDI DUNIA IJUE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado anaichambua ripoti ya CAG kimyakimya bila shaka atakuja na uchambuzi yakinifu bila kusahau udhaifu wa Bunge letu tukufu utapata tafsiri sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh. Lissu atakuwa hayupo sawa kisaikolojia, aidha ana matatizo ya kisaikolojia. Hivi alivyokuwa anatembeza bakuli mbona alisema hahitaji mshahara?

Then alivyoona michango haitoshi akawatishia bunge, then busara zikatumika kumhurumia huyu mharifu Lissu then leo anasema eti wameogopa, hahahaha, kweli wapinzani wana uelewa mdogo sana
 
HABARI NJEMA KUTOKA KWA HON. TUNDU LISSU

Hello bandugu wapendwa,

Nawasalimuni kwa upendo tele na heshima kubwa. Natumaini Mungu wa Haki amewajalia afya na kila lililo jema. Ni stahili yenu.

Naomba nianze kwa kuwatakia kila la kheri katika wakati huu wa Wikiendi ya Pasaka.

Pili naomba niwape mrejesho kuhusu 'ugomvi' wangu na Spika Ndugai na watu wake juu ya mshahara wangu.

Pamoja na kwamba Spika Ndugai amesikika akisema kuwa mambo ya mshahara ni siri ya Bunge na Mbunge husika, na yanatakiwa kujadiliwa 'chumbani' na sio 'sebuleni', nadhani ni vizuri tukafunga mjadala huu kama ulivyoanza: hadharani!!!

Kwa kifupi ni kwamba Spika Ndugai na watu wake wamelipa mshahara wangu wa tangu Januari hadi Machi waliokuwa wameuzuia kiharamia tu.

Kwa maoni yangu, kilichowafanya wakubali yaishe ni ujasiri wenu, na wa watu wengine wengi, mlioamua kunichangia, sio tu gharama za matibabu yangu, bali hata huo mshahara uliozuiliwa kinyume na Sheria na Kanuni za Bunge.

Kama walivyotaka nife kwa kukosa matibabu, watu hawa walitaka nife njaa kimya kimya kwa kuninyang'anya mshahara wangu.

Sikukubali kufa kimya kimya na ninyi ndugu zangu hamkukubali. Walipoona sokomoko la mshahara wangu limekuwa kubwa na sasa limebebwa na wananchi wakakubali yaishe. Nawapongezeni sana kwa ushindi huu.

Hili ni funzo kubwa sana kwa kila mmoja wetu. Tusikubali kukaa kimya tunapoonewa. Hakuna fedheha yoyote katika kupiga kelele za kudai haki. Tupaze sauti zetu na kupiga kelele, watu wema watasikia kilio chetu na tutapata msaada.

Hakuna busara yoyote ile katika kukubali kunyongwa kimya kimya na wasio na haki. Christopher Okigbo, mshairi maarufu wa Nigeria ya wakati wa Vita ya Biafra, aliandika: "The man died who keeps silent in the face of oppression."

La tatu linahusu afya yangu. Na kwenye hili habari ni njema sana. Tarehe 2 ya mwezi huu nilikutana na madaktari wangu kwa appointment ya kwanza tangu operesheni za tarehe 20 Februari.

Taarifa yao ni kwamba mfupa wote wa mguu wa kulia umepona vizuri. Sehemu iliyowekewa 'kiraka' cha mfupa na kupigwa 'ribiti' ya chuma juu kidogo ya goti; na sehemu ya kwenye paja iliyotakiwa kuota mfupa mpya, zote ziko vizuri.

Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kukunja goti na kujifunza kutembea tena. Naomba mniamini nikisema kujifunza kutembea tena, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kulala kitandani, ni kazi ngumu sana!!!!

Nafikiri sina tofauti sana na mtoto mdogo anayejifunza kupiga hatua zake za kwanza. Lakini pole pole nitafika inshaallah.

Tarehe 14 ya mwezi ujao nitapimwa urefu wa miguu ili nitengenezewe kiatu au soli maalum kwa ajili ya mguu wa kulia.

Kwa sababu ya majeraha makubwa niliyopata, mguu huo ni mfupi kwa sentimita kadhaa. Bila kiatu au soli maalum nitakuwa 'langara' sana na madaktari wamesema hiyo sio sawa sawa.

Kwa kumalizia, sasa nina tarehe ambayo madaktari wangu wamesema nitakuwa 'fiti' kurudi nyumbani.

Msiniambie niiseme kwa wakati huu. Tunahitaji kushauriana na wadau mbali mbali kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwangu nyumbani.

Tukumbuke tu kwamba waliotaka kuniua mchana kweupe katikati ya mji wa Dodoma bado wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Itabidi tupate 'security guarantees' kutoka kwa wahusika, Serikali ya Magufuli na Jeshi la Polisi, kwamba nitakuwa salama nikirudi.

Kwa hiyo, wakati muafaka utakapofika, hopefully sio mbali sana, nitawaeleza tarehe kamili ya kurudi nyumbani na, kwa mlioko Dar, nitawaomba mniandalie supu ya utumbo wa mbuzi Rose Garden kwa Mzee Assey!!!

Wasalaam
TL

SHARE ZAIDI DUNIA IJUE.

Sent using Jamii Forums mobile app
cc: Wakudadavuwa
 
Mh. Lissu atakuwa hayupo sawa kisaikolojia, aidha ana matatizo ya kisaikolojia. Hivi alivyokuwa anatembeza bakuli mbona alisema hahitaji mshahara? Then alivyoona michango haitoshi akawatishia bunge, then busara zikatumika kumhurumia huyu mharifu Lissu then leo anasema eti wameogopa, hahahaha, kweli wapinzani wana uelewa mdogo sana
Kwahiyo ulitaka malipo yalivyoingia bila kumtaarifu kuwa tunakulipa maana kelele zimezidi.. wewe ulitaka azirudishe etiee... SHWAIN KABISAA!!!
 
Mh. Lissu atakuwa hayupo sawa kisaikolojia, aidha ana matatizo ya kisaikolojia. Hivi alivyokuwa anatembeza bakuli mbona alisema hahitaji mshahara? Then alivyoona michango haitoshi akawatishia bunge, then busara zikatumika kumhurumia huyu mharifu Lissu then leo anasema eti wameogopa, hahahaha, kweli wapinzani wana uelewa mdogo sana
Screenshot_20190415-103200.jpeg
 
Back
Top Bottom