Uchaguzi 2020 Tundu Lissu sio Mzee Lowassa, asipuuzwe!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
TUNDU LISU SIYO MZEE LOWASA, ASIPUUZWE.

Na, Robert Heriel.

Moja ya sifa ya Mpumbavu ni kuishi kwa Dharau na mazoea. Tabia ya mazoea imeangusha watu wengi mashuhuri. Maisha hayana mazoea, maisha yanabadilika. Hivyo hata siasa haina mazoea, siasa zinabadilika, dakika moja inatosha kabisa kubadili mwelekeo wa siasa.

Hata katika michezo, timu zinazocheza kwa mazoea, ati mwaka fulani nilikufunga hivyo mwaka huu nitakufunga pia, bila kufanya jitihada huko ni kujidanganya.

Kuna watu wanafikiri kama watu wajinga, mtu mjinga huishi ulimwengu wa zamani, mtu mjinga anadhani dunia ya zamani niyasasa. Mtu mjinga hafikiri dunia inaenda mbele. Yeye anafikiri jana ni leo, na leo itakuwa kesho. Jambo ambalo sio kweli.

Hata katika Siasa, hasa katika bara letu la Afrika. Wanasiasa wengi wanatabia ya kufikiri kijinga jinga tuu. Yaani kama alishinda zamani basi anadhani kila siku atashinda, kama ni mbunge wa jimbo fulani anafikiri atabaki kuwa mbunge, kama chama chake ni chama tawala anafikiri kitaendelea kuwa tawala milele. Hivyo wengi huishi kwa mazoea na dharau, hali inayopelekea kutofanya jitihada za kusaidia wananchi.

Hili nimeliona katika siku chache tangu Lisu aanze harakati zake za kutafuta wadhamini.

Wapo watu wanaakili za kijinga, wanatumia jana katika siku ya leo.

Utasikia mjinga mmoja akisema; Hata Lowasa alikuwa anajaza watu hivyo hivyo, tena lowasa alikuwa ananguvu. Mwingine utasikia, Mbona huyu hajamfikia Dr. Slaa, mwingine atakuambia mbona hajafika hata nusu ya nyomi za Mzee Mrema. Mtu yeyote awazaye hivi huwaza kama mtu mjinga. Nimeshatoa sababu kuwa, moja ya mtu mjinga ni kudhani kila siku ni jumapili, pia ni kudhani kuwa kama alimshinda fulani basi hata huyu atamshinda. Wazo hili aliliwaza Mtu aitwaye Goliath, ati kwa vile yeye ni jemadari na ananguvu basi alivyomuona Daudi kakijana kadogo akakadharau, akatumia mazoea, wote tunajua, Goliath alikatwa kichwa na Daudi.

Tunafahamu hata kule Marekani, hakuna ambaye alijua Donald Trump angemshinda Hillary Clinton. Lakini Dharau za wapiga kura wa Hillary zilimpa ushindi Trump kwani hawakwenda kupiga kura .

Mzee Kinana aliongea jambo lenye hekima kubwa kuwa, hakuna uchaguzi rahisi. Hivyo watu wasichukulie mambo ni kama kawaida. Hata Mhe Rais ambaye anatetea kiti chake. Mhe. Magufuli mara kadhaa nimemsikia akiwaambia wanachama wake kuwa, wasichukulie rahisi, wasidhani wameshinda, ushindi bado, hivyo siku ya kura waende kupiga kura.

Hao ni watu wazima wenye akili. Watu wasioishi siku ya jana.

CCM kumshinda Lowasa sio kusmhinda Tundu Lisu
CCM kumshinda Dr Slaa sio kumshinda Lisu
CMM kumshinda Lipumba sio kumshinda Lisu
CCM kumshinda Mrema Sio kumshinda Lisu.

Kwanza ni watu tofauti kabisa, kitabia, kihaiba, kitaaluma, kinyakati.

MAMBO YANAYOMTOFAUTISHA Lisu na Lowasa

1. ASILI YA ITIKADI ZAO
Lisu hakuwahi kuwa CCM. Lakini hao wengine wote walishawahi kuwa Ccm. Hii ni moja ya Sababu kuu ya kwa nini Lisu asipuuzwe. Lisu ni Mpinzani OG.
Kubadili Itikadi ni sawa na kubadili jinsia, yaani ni sawa na mwanamke ajibadili awe mwanaume Bado atabaki kuwa mwanamke tuu. halikadhalika na kwa mwanaume. Mtu kama Mrema, Lipumba, Dr. Slaa, Lowasa hao ni CCM na watabaki kuwa hivyo.

2. UJASIRI
Lisu ni jasiri, haogopi kusema kile anachokiamini bila kujali matokeo, Lisu hamung'unyi maneno.Lakini Lowasa ni mtu wa kumung'unya maneno, Ujasiri wake ni mdogo ukilinganisha na wa Lisu. Kidogo Dr Slaaa anaweza kumkaribia Lisu lakini sio kumfikia Lisu.

Lowasa hakuwa na ujasiri wowote, pengine nikijaribu kumtetea, nitatoa sababu labda umri unachangia. Inasemekana umri unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo ujasiri unavyozidi kupungua.

3. USHAWISHI
Lisu anaushawishi Mkubwa kuliko Lowasa. Kuna watu wanadhani Lowasa alikuwa na ushawishi, lakini sio kweli, Lowasa hakuwa na ushawishi wowote. Lowasa ni mtu wa mitego. Lowasa alikuwa anachambo ambacho ni pesa, waliokuwa wanamshabikia ni kutokana na kuvizia pesa zake. Yaani mtego wake ni kuwa Rais lakini chambo alichokitumia ni pesa. Watu walikuwa wanavizia pesa zake.

Lowasa ni sawa na mwanaume mwenye pesa anayeenda kuposa mwanamke. Kitakachomshawishi huyo mwanamke ni pesa zake na wala sio Lowasa.Hii ni tofauti na Lisu. Lisu ni kama mwanaume masikini anapoenda kumchumbia mwanamke. Hana pesa lakini anakubaliwa kutokana na maneno yake.

Lisu anajua kujenga hoja zenye ushawishi, na hii ni watu wachache wanayo. Lisu kamuacha mbali sana Lowasa kwenye kujenga hoja.

Kama Lowasa angekuwa anajua kuongea vizuri basi mwaka 2015 angeukwaa Urais. Lakini alizidiwa vilivyo na Magufuli. Wote tunajua kuwa Magufuli naye hajambo kwa mdomo, anajua kujenga hoja, Magufuli hata umpe masaa matatu hapo azungumze ataongea na hutatamani aache kuzungumza. Hiko ndicho kilimfanya Magufuli amshinde Lowasa mbali na sababu zingine.

Lisu asipuuzwe kwa maana mdomo anao, anajua kuongea, hashindwi kuongea siku nzima na ukatamani aendelee kuongea. Sifa ya watu wanaojua kushawishi pia wanachanganya na chumvi nyingi. Hilo lizingatiwe, wanautani, wanadata nyingi, wana mikwala, wanaswaga.

Lisu siku zinavyozidi kwenda anazidi kupata nguvu ya ushawishi kwa watu.Siku 60 ni nyingi sana kwa Mtu kama Lisu.


4. NYAKATI
Wakati wa Lowasa na Lisu ni tofauti kabisa. Japo tofauti ni miaka mitano lakini ni miaka mingi sana kisiasa, kiuchumi na kimtazamo.

Lowasa alikuwa kipindi ambacho changamoto za ajira zilikuwa ni ndogo. Vijana wasomi walikuwa wanaajiriwa kwa sehemu kubwa na serikali. Lakini Lisu kipindi hiki Vijana wengi wamesota kwa miaka mitano bila ajira za kueleweka. Sidhani kama kuna kijana msomi ambaye hatamuelewa Lisu wakati amesota miaka mitano, wengine mitatu kwa kadiri ya mwaka aliomaliza. Ni kijana mjinga tuu ambaye amesoma alafu hana muelekeo wa maisha ambaye hatamuelewa Lisu.

Kipindi cha Lowasa Watumishi wa Umma walikuwa wanaongezwa mishahara pia na kupandishwa madaraja. Lakini kipindi hiki cha Lisu, wafanyakazi wengi wanalia na kusaga meno kwa mishahara yao kudumaa huku gharama za maisha zikiendelea kupanda. Ni wafanyakazi wachache ambao hawatamuelewa Lisu, kwa maana wameguswa moja kwa moja.

Ongezeko la Kundi kubwa la vijana wenye umri kuanzia 18 Kuendelea linaweza likawa sababu pia ya kuwatofautisha Lisu na Lowasa.


5. HALI YA UTEGEMEZI IMEBADILIKA
Siku hizi hali ya utegemezi inazidi kubadilika.

Kura nyingi wanazo wanawake, CCM inavuna kura nyingi kwa wanawake hasa wategemezi ambao wanasubiri mume alete pesa nyumbani. Wanawake hawa ni moja ya mitaji ya CCM kwani wao hawajui pesa inatafutwaje. Wao ni Goalkeeper. Wanawake tegemezi wao lawama huwapa waume zao pale mume anaposhindwa kutoa matumizi. Mume yeye ndiye anajua anakutana na changamoto gani huko mtaani.

Hali ya sasa imebadilika kidogo, wanawake nao wanatoka kwenda kutafuta riziki. Sio kwamba 2015 kurudi nyuma hapakuwa na wanawake waliokuwa watafutaji, hasha! Ila zama hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wanaotafuta pesa. Hivyo nao wanajua ugumu wa kuipata pesa, wanaona vikwazo.

Nachelea kusema, mikoa yenye wanawake watafutaji wengi wao hawaichagui CCM, angalia Mkoa wa Mbeya, njoo Iringa, Twende Kigoma, Nenda Mkoa wa Mara, Shuka Arusha, kisha Kilimanjaro, fika Dar es Salaam. Mikoa hiyo wanawake wengi nao wanajishugulisha, hivyo wanaona ni kwa namna gani serikali iliyokuwa chini ya CCM inavyowapa wakati mgumu katika utafutaji wa Riziki.

Utegemezi kwa vijana, vijana wa siku hizi wengi wameamka. Wanajishughulisha wengine kwenye kilimo, bodaboda, saluni, ujasiriamali n.k. Mikoa yenye vijana wachapakazi, watafutaji wengi ni rahisi kusombwa na upepo wa Lisu.

Mbinu kubwa ambayo itawafanya wanawake kuelewa hoja za Lisu, ni kuwaambia nao waingie mtaani watafute hela. Sio asubiri chakula ndani ya nyumba yeye kazi yake kula na kunenepa. Mwambie mkeo toka nawe tusaidiane kutafuta, hapo hata siku akimsikia Lisu anaweza kuelewa.

Lisu na Lowasa ni mbingu na Ardhi.


6. KUKUA KWA MITANDAO YA KIJAMII NA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO.
Idadi ya vijana wanaomiliki simu janja wakati wa Lowasa na sasa ni mbali mno. Kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana wanaotumia simu janja ambapo wengi wanajiunga na mitandao ya kijamii. Wewe mwenyewe unaweza kufanya utafiti mdogo kuwa ndugu zako wangapi au hapo mtaani kwenu ni watu wnagapi mwaka 2015 hawakuwa na simu janja na sasa hivi wanazo. Ni watu wangapi unawafahamu ambao 2015 hawakuwa wamejiunga na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, Jamiiforum n.k na sasa wamejiunga. Utakuta ni wengi.

Ongezeko la watumiaji wa simu janja na wanamitandao ya kijamii linaathari kubwa katika siasa. Kwani siku hizi sio rahisi kudanganya, ukimsingizia mtu, muda huo huo hata bila vyombo vikuu vya habari kama ITV, TBC, StarTv n.k mtu anakanusa, na anatoa ushahidi.

Watu siku hizi hawasubiri habari za magazetini au kwenye Televisheni


Kumfananisha Lisu na Lowasa ni kutotumia akili vizuri. Lisu ananafasi kubwa ya kushinda ukilinganisha na Lowasa ambaye hata kuongea dakika kumi zilikuwa ni shida kabisa.

Mimi ningekuwa ndio CCM, ningehakikisha Tundu Lisu hapitishwi na NEC, pengine hiyo ndio ingekuwa Figisu figisu ya kumuondoa Mchezoni, najua sio haki lakini ni bora ningepambana naye kwenye masuala ya NEC, Kuliko kukimbizana naye kwenye kampeni.

Hii ni kutokana na upande wa Pili wa Zanzibar ambapo nako hapatoshi.

Ningekuwa mimi, mgombea mmoja kati ya Lisu au Maalimu Seif ningemuengua NEC ili abaki mmoja. Lakini kuwa na wote wawili kwa wakati mmoja, hakika sijui.

CCM wasipuuzie, siku 60 kwa mtu anayejua kushawishi ni siku nyingi mno. Msimfananishe Lisu na Mzee Lowasa. Hamtaamini.

Narudia, siku 60 ni siku nyingi sana. Siku 60 zinamtosha Lisu kugeuza akili za Watanzania.

Tuipende nchi yetu.
Tupendane
Tulinde amani kwa kutenda haki.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Good analysis
Unfortunately, our presidential election has got a pre-determined winner 😂😂😂😂


Kuwa na wagombea wawili moto wenye misimamo kama ya Lisu kwa Zanzibar na Bara hakika ningekuwa mimi mmoja ningemuengua kwa figisu figisu.

Aidha Nichague Nipambane na Lisu au Seif. Wote wawili hapana, kuna hatari ya kupoteza kote, au sehemu moja.

Ili nipate Bara na visiwani sharti nimuengue mmoja ili nguvu yao ipungue.
 
Kuwa na wagombea wawili moto wenye misimamo kama ya Lisu kwa Zanzibar na Bara hakika ningekuwa mimi mmoja ningemuengua kwa figisu figisu.

Aidha Nichague Nipambane na Lisu au Seif. Wote wawili hapana, kuna hatari ya kupoteza kote, au sehemu moja.

Ili nipate Bara na visiwani sharti nimuengue mmoja ili nguvu yao ipungue.
Hapa watasababisha balaa ambalo hawataweza kulizuia, hii issue ni kama maji, ukishayavulia nguo sharti uyaoge, there is no plan B there.
 
Analysis yako ya leo kweli imekaa kuihalisia na umetendea haki dhana ya Jamii Forums, Home of Great thinkers.

Nilikuwa naongea na bwana mmoja jana na ni mtu mkubwa serikalini akaniambia kuwa hakuna uchaguzi mgumu kwa Tanzania Kama wa mwaka huu. Maneno yake machache aliyoniambia hayatofautiani sana na hoja zako hapa!

Nirudi kwenye kumuengua Lissu! Hapo ndugu Nina uhakika, hakuna sehemu CCM watafeli kama hapo. Hilo likitokea, amini maneno yangu hapatatosha. Watanzania wengi wamefika a point of no return na Nina uhakika hali itakuwa mbaya sana na sidhani Kama kutakuwa na uchaguzi.

Wewe fikiria umati wa Jana Tunduma uamue kwenda mbele zile gari tatu za polisi zitaweza kuwasimamisha?????

Pili Naona hata Tanzania tutakuwa tumejiwekea mazingira ya kuwekewa vilwazo. Tamko la juzi la kamati ya mambo ya nje ya bunge la marekani inaonesha kuwa tunafuatiliwa sana. Usisahau mambo ya Wakili wa kimataifa Amsterdam!


Mimi nilikuwa CCM ndugu, ukweli ni kuwa CCM tulijisahau sana. Naona ili CCM iwe Chama bora kwa sasa kinachojitegemea kutokana na Sera bora na ushawishi bila kutegemea vyombo vya dola ni vizuri kikapumzishwa na watanzania kwa hata miaka 5 - 10 ili wajifunze.

Dunia inakimbia sana kwenda mbele ila CCM imekuwa ikiwarudisha nyuma watanzania miaka 100 nyuma. Hili sio sahihi hata kidogo.

Ni vizuri Lissu ashinde mwaka huu ni vizuri Tanzania tujifunze kuwa kuna maisha nje ya CCM. Ni vizuri pia Tanzania ijaribu Sera mbadala nje ya sera za kijamaa za CCM kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya watu na vitu!
 
Back
Top Bottom