Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
TUNDU LISSU mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Rais wa Chama cha wanasheria TLS, mwanasheria Mkuu wa Chadema, Wakili wa kujitegemea hana uwezo wa kuhamasisha maendeleo ndani ya Jimbo Lake hata ujenzi wa Choo kimoja, Mara zote wajibu wa kiongozi ni kuonyesha njia kwa Wale unawaongoza, kuonyesha njia na kuifuata njia hiyo kwa kushirikiana na wananchi wako kujiletea maendeleo.
Kwa Wale wanaofutilia kwa karibu siasa za Wilaya ya Ikungi yenye Majimbo mawili yaani Singida Mashariki na Singida Magharibi wanaujua huu ukweli, Lissu amezidiwa mbali na Elibariki Kingu Mbunge wa Singida Magharibi kwenye suala la Maendeleo ya wananchi, Lissu ni tajiri na Mwenye Mapato makubwa na umaarufu mkubwa lakini yote hayo hayana faida kwa wapiga kura wake, Yeye ni mtetezi wa chama, mfia chama, mnazi wa chama na mtumwa kwa chama chake tu.
Tangu aingie Bungeni 2010 hadi leo hakuna la Maana alilofanya Jimboni au alilololianzisha kwa ajili ya Maendeleo Jimboni kwake, hayuko karibu na wananchi, hatembelei jimbo Lake na kukaa na wananchi kupanga mipango ya Maendeleo, yeye huwa anaenda Ikungi anafanya mkutano analalamika weee anaondoka kurudi Dar es salaam. Hata darasa likiezuliwa na upepo yeye anaamini Serikali itafanya hana mpango wa kufanya wala kuhangaisha kichwa chake kuhakikisha darasa lililoezuliwa na upepo linarekebishwa.
Huyo ndio Rais Tundu Lissu , vyeo kibao lakini havina msaada kwa wapiga kura wake.