Tundu Lissu: Ninaendelea vizuri na matibabu

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,289
Anaandika Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.

Wapendwa wangu,

Naomba niwape taarifa ya maendeleo yangu ya kiafya. Ninaendelea vizuri na matibabu. Mguu wa kulia unaendelea kupata nguvu na sasa ninaweza kusimama kwa miguu yote bila msaada wa magongo. .

Hata hivyo, timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana. .

Madaktari wangu wamesema kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, kwanza, itachukua muda mrefu sana kuunga; na pili, hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. .

Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia. .

Hivyo, siku ya Jumatano ijayo ya tarehe 14 March, 2018, nitarudi Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, kwa ajili ya kufanyiwa operesheni hiyo. .

Niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Madaktari wangu, Prof. Dr. Stefa Nijs na Prof. Dr. Willem-Jan Mertsemakers, ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya kwa utaalamu wao katika fani hiyo. Hivyo, msiwe na hofu. Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza yake kupitia kwa madaktari bingwa hawa.
.
Nitaendelea kuwataarifu maendeleo ya matibabu yangu kadri itakavyokuwa lazima na muhimu kufanya hivyo. .

Kama kawaida, nawaombeni muendelee kutuunga mkono mimi na familia yangu kwa maombi na misaada ya kibinadamu ya hali na mali kwa kadri ya Mungu alivyowajalia. .

Mungu awabariki sana.
0e2608781b6859205f40c6f7daf0dae9.jpg

IMG_20180311_073605.jpg

IMG_20180311_073601.jpg
 
View attachment 710857
Wakiona hivi akili zinawaruka kabisa
 
Hata Yesu alisulubiwa msalabani na wanadamu japo hakuwa na kosa lolote.Usijali Mungu atakuwa nawe siku zote kama ambavyo hakumuacha mwanae mpendwa Yesu Kristo ambae nae hakuwa na hatia yoyote kama ulivyo wewe leo hii.

Tukumbuke hata Pilato hakuona kosa lililostahili Yesu asulubiwe hivyo nawe haya yatapita tu kama yalivyopita kwa Kristo.

Duniani hakuna haki!
 
Iv' mutaelimika lini wacheza cinema???
Maana mwavuja damu pasina jeraha kuliona!
[HASHTAG]#UPUUUUUUUUUUUUUUUUZZZy[/HASHTAG]
 
Nguvu ya Mungu i pamoja nasi. Mwenyezi Mungu na akujaalie upone upesi urudi kuokoa jahazi ambalo tangu uondoke linazama kwa kasi ya 32G
 
Back
Top Bottom