Tundu Lissu: Napendekeza kutafakari mambo yafuatayo ya kufikirisha katika kujaribu kuelewa maana halisi ya hii hama hama

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Anaandika Wakili Msomi #TunduLissu wa CHADEMA, leo October 8, 2018 akitokea nchini Ubelgiji.

Huu mjadala wa hama hama ya Wabunge wa CHADEMA ni muhimu sana. Unahitaji kujadiliwa kwa tahadhari na kwa umakini, vitu ambavyo ni adimu katikati yann kelele na vumbi kubwa vilivyotokana na hama hama hii.

Napendekeza kutafakari mambo yafuatayo ya kufikirisha katika kujaribu kuelewa maana halisi ya hii hama hama:

(1) Kuhama kwa viongozi wa kisiasa kutokana na migogoro na tofauti za kisiasa ndani ya vyama vya siasa sio jambo geni katika historia ya vyama vingi nchi yetu. Hata hivyo, kuhama kwa Wabunge na Madiwani wa upinzani kwenda CCM ni jambo geni.

(a) Kati ya 1995, CHADEMA ilipopata Wabunge wake wa kwanza (walikuwa wanne), na 2015 ilipopata Wabunge 35 wa majimbo na 37 wa Viti Maalum, hakuna Mbunge au diwani hata mmoja aliyejiuzulu ubunge na kujiunga na CCM kwa sababu yoyote ile.

(b) Katika kipindi hicho cha '95 - '15, Wabunge na Madiwani walioondoka CHADEMA na vyama vingine vya upinzani na kuhamia CCM:

(i) ama walifukuzwa kwenye vyama vyao (mfano madiwani 5 wa CHADEMA Arusha, akina Danhi Makanga na Teddy Kasela Bantu wa UDP, n.k.),

(ii) ama walipoteza ubunge wao mahakamani (mfano Makongoro Nyerere, Dr. Lamwai, Kifu Gullamhussein Kifu wa NCCR-Mageuzi, n.k.)

(iii) au walisubiri washindwe ubunge ndio wakahamia CCM (mfano Dr. Amani Walid Kabourou, Saidi Arfi wa CHADEMA na wengineo wengi)

(c) Katika kipindi hicho hicho, waliokuwa wanahama chama wakiwa wabunge na kujiunga na vyama vingine walikuwa wanaCCM (mfano Freddie Mpendazoe).

(2) Katika kipindi hicho chote, licha ya matatizo mengi, hakukuwa na ukandamizaji wa haki za kisiasa na haki za binadamu kwa ujumla kama ilivyo sasa.

(a) Vyama vya siasa vilikuwa vinaendesha mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa.

(i) Leo shughuli za kawaida za kisiasa, kama mikutano ya hadhara, maandamano na hata vikao au semina za ndani, zimepigwa marufuku kabisa.

(b) Viongozi wa vyama vya upinzani hawakuwa walengwa wa moja kwa moja wa ukandamizaji unaoendeshwa na vyombo vya usalama.

(i) Leo karibu viongozi wote wa CHADEMA wa ngazi za juu, wakiwemo Wabunge wengi, na wa ngazi za kati na hata za chini wanakabiliwa na kesi za jinai mahakamani.

(ii) Wengi wa wale ambao bado hawana kesi angalau wameonja mahabusu au kipigo cha polisi kwa kufanya shughuli za kawaida za kisiasa zinazoruhusiwa na sheria zetu.

(iii) Wapo viongozi wameuawa kinyama lakini mauaji yao hayajachunguzwa wala hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

(iv) Wengine wamejeruhiwa vibaya katika mazingira hayo hayo ya kulenga kuwaua au kuwadhuru viongozi wa upinzani.

(c) Haki, hadhi na heshima ya Bunge na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge au katika shughuli za kibunge, zilikuwa zinaheshimiwa. Leo kuwa Mbunge, au diwani au hata Mwenyekiti wa Kijiji au Mtaa wa upinzani, hasa wa CHADEMA, ni adha kubwa.

(i) Leo Wabunge wa upinzani wanapigwa na kudhalilishwa na askari wenye sare za polisi ndani ya Ukumbi wa Bunge.

(ii) Wakitoka nje ya Bunge Wabunge wa upinzani wanatekwa nyara na mapolisi na kusafirishwa usiku kupelekwa Dar Es Salaam au Arusha au Morogoro au kwingineko.

(iii) Leo Wabunge wa upinzani wanakamatwa na kuwekwa mahabusu na baadae kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa kushiriki kwenye mikutano ya hadhara kwenye majimbo yasiyokuwa yao, ambalo halijawahi kuwa kosa la jinai katika nchi yetu.

(3) Ambao wanajiuzulu ubunge na udiwani na kuhamia CCM ni wanaCHADEMA wa aina gani hasa???

(a) Wabunge wote wa CHADEMA ambao wamejiuzulu ubunge na kuhamia CCM ni wanaCHADEMA na Wabunge wapya.

(i) Baadhi, kama Dr. Mollel wa Siha na ole Kalanga wa Monduli, waliingia CHADEMA na bungeni kutokana na wimbi la Lowassa la '15.

(ii) Baadhi, kama Waitara, Ryoba na ole Millya, wana muda mrefu CHADEMA lakini ni Wabunge wapya.

(iii) Ubunge wa upinzani wanaoujua hawa waliohama, ni ubunge wa upinzani wa Tanzania ya Magufuli na Bunge la Spika Ndugai, i.e. ubunge wa adha na mateso, sio ubunge wa heshima wa Bunge la Spika Sitta na Spika Makinda.

(b) Wabunge wenye historia ndefu kwenye CHADEMA au bungeni hawajajiuzulu hata mmoja.

(i) Tofauti na waliohama, hawa wana historia na uzoefu wa mapambano kisiasa ya upinzani nje na ndani ya Bunge.

(ii) Tofauti na waliohama, hawa wana historia na uzoefu wa kutiwa misukosuko mbali mbali na Serikali ya CCM kabla na baada ya kuwa wabunge.

(4) Mazingira ya kuhama hama yakoje??? Swali hili ni muhimu kwa sababu ya ubishani mkubwa uliopo kuhusu madai ya matumizi ya rushwa ili kuwarubuni wanaohama.

(a) Kila aliyehama amerudishwa na CCM kama mgombea wa nafasi ile ile aliyoiacha kwa kujiuzulu, bila hata kufuata utaratibu wa kawaida wa kichama wa kufanya vikao vya uteuzi, n.k.

(b) Viongozi wa CCM na Serikali yake, kuanzia Rais Magufuli mwenyewe na wa chini yake, wametangaza hadharani kwamba kila atakayejiuzulu ubunge au udiwani atarudishwa kugombea nafasi ile ile kwa kupitia CCM na atatangazwa mshindi kwa nguvu. Hata bila ushahidi wa malipo ya fedha, ahadi hizi ni rushwa kwa tafsiri ya rushwa ya sheria za nchi yetu.

(c) Kila aliyejiuzulu ubunge au udiwani na kuhamia CCM amefanya hivyo ili 'kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo'!!!

(i) Hata bila kuhoji ukweli wa sababu yenyewe, inawezekanaje hiyo ndio iwe sababu ya kila mmoja anayejiuzulu na kuhamia CCM???

(ii) Hata bila kuuliza maswali juu ya uhalali wa sababu hiyo, kwa nini wanaojiuzulu sasa wanarudishwa kugombea nafasi zile zile walizoziachia???

(iii) Kwani kujiuzulu ubunge au udiwani wa CHADEMA na baadae kugombea nafasi zile zile kwa CCM ni njia pekee ya kumuunga mkono Magufuli??? Kumbuka, John Shibuda wa CHADEMA na John Cheyo wa UDP walikuwa wakiunga mkono jitihada za Rais Kikwete lakini hawakuwahi kujiuzulu ubunge au uanachama wa vyama vyao.

(iv) Hivi inakuwaje wanaounga mkono jitihada za Rais Magufuli ni wanaCHADEMA peke yao??? Vipi akina Lyatonga Mrema, au Profesa Lipumba, au Dovutwa na wengineo wa vyama vingine??? Au ndio kusema hawa hawana madhara yoyote kwa CCM hata wakibaki kwenye vyama vyao???

(v) Hivi inakuwaje wanaounga mkono jitihada za Rais Magufuli ni Wabunge na Madiwani wa Majimbo na Kata peke yake???

Inawezekanaje Rais Magufuli asiungwe mkono na Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum ambao ndio wengi zaidi bungeni???

Au ndio kusema kujiuzulu kwa Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum hakuna faida yoyote kwa CCM kwa sababu hakupunguzi idadi ya Wabunge na Madiwani wa upinzani???

(vi) Katibu Mwenezi wa CCM, Polepole, amesema kwamba mwisho wa 'kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo' ni December, '18. Kwa nini zuio hilo la CCM linalingana ama kukaribiana na zuio la kikatiba na kisheria kwa chaguzi za marudio??? Je, hii ni bahati mbaya tu au kuna njama iliyofichwa kwenye hii ratiba ya CCM na ratiba iliyowekwa na Katiba na Sheria za Uchaguzi???

(c) Kila aliyehama 'ameshinda' uchaguzi katika mazingira ya matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi na mfumo wa usimamizi wa uchaguzi wenye upendeleo wa wazi wazi kwa CCM. Matokeo yote ya chaguzi za marudio za hivi karibuni ni matokeo ya kupika kati ya wasimamizi wa uchaguzi wanaCCM na vyombo vya usalama vya Serikali ya CCM. Hata Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ali amethibitisha hili in so many words.

(5) Je, tatizo ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe??? Hili nalo limeleta mjadala mkubwa.

(a) Wote waliojiuzulu ubunge na udiwani wa CHADEMA na kujiunga na CCM na wapambe wao wamedai tatizo ni Mwenyekiti Mbowe.

(i) Hata hivyo, waliingia CHADEMA na kuchaguliwa Wabunge au madiwani kwa kupitishwa na vikao vya Chama vilivyoongozwa na Mwenyekiti Mbowe huyo huyo. Baniani mbaya ila kiatu chake dawa!!!

(ii) Mwenyekiti Mbowe hajawahi kuwa kiongozi wa CHADEMA mzuri kwa CCM tangu angalau '05 alipogombea Urais hadi leo hii. Baadhi ya dhambi zake ni pamoja na kuwa Mchagga, mkwe wa Mzee Mtei, Mkaskazini, Mkristo na, sasa, mng'ang'ania madaraka.

(iii) Licha ya 'madhambi' haya makubwa, Mwenyekiti Mbowe ni kiongozi wa upinzani mwenye mafanikio makubwa katika historia ya vyama vingi vya siasa nchini kwetu.

(b) Mwenyekiti Mbowe amelipia mafanikio yake katika siasa za upinzani za Tanzania kwa gharama kubwa sana.

(i) Biashara zake, iwe ni Bilicanas, au uchapishaji magazeti au mashamba ya kilimo, zimeharibiwa na Serikali ya Magufuli ili kulipiza kisasi kwa sababu ya mafanikio yake ya kisiasa.

(ii) Mwenyekiti Mbowe amekamatwa na kushtakiwa kwa jinai kwa sababu za kisiasa kuliko pengine kiongozi mwingine mkuu wa Chama cha siasa katika Tanzania.

(c) Katika viongozi wote Wakuu wa upinzani katika historia ya Tanzania, ni Mwenyekiti Mbowe, na pengine Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF, ambaye amebaki na msimamo thabiti wa kisiasa licha ya mateso makubwa ambayo amepitishwa.

(6) Kujiuzulu kwa Wabunge na Madiwani wa upinzani, hasa CHADEMA, katika mazingira haya kuna madhara kwa CHADEMA na kwa siasa za upinzani kwa ujumla. Je, ni madhara gani hayo na ni makubwa kiasi gani kwa CHADEMA na kwa siasa za upinzani???

(a) Ni wazi wapo viongozi, wanachama, wafuasi na wananchi waliokatishwa, na watakaokatishwa, tamaa na matukio haya. Je, ni wengi kiasi gani???

(b) Kama hama hama hii ina madhara makubwa kwa upinzani kama inavyoelezwa na baadhi yetu, ni kwa nini kuna matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi na kila aina ya ubabe na hila kwenye chaguzi za marudio???

(c) Kama 'upinzani unakufa' kama inavyoelezwa, kwa nini Serikali ya Magufuli inaendelea kukataza uhuru wa vyama vya siasa vya upinzani kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria zetu??? Kwa nini bado kuna makatazo ya Bunge Live??? Kwa nini kuna ukandamizaji wa vyombo vya habari na uhuru wa maoni???

(d) Kama hama hama hii ina madhara makubwa kwa upinzani, kwa nini bado wananchi wetu wanahudhuria kwa maelfu katika mikutano ya hadhara michache inayoruhusiwa wakati wa kampeni za chaguzi za marudio???

Haya ni baadhi ya masuala yanayohitaji kujadiliwa kama sehemu ya mjadala wa hama hama ya Wabunge na Madiwani wa upinzani. Nawataka radhi kwa kuwasubirisha muda mrefu.
 
Lisu anajua kabisa kwamba katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama chochote muda wowote kama huko aliko haoni kama anatendewa haki .

Leo Lisu anakuja na bandiko refu kumshawishi rais Magufuli avunje katiba kwa kupiga marufuku watu kuhama chama , alafu ikitokea hivyo ,Lisu huyu huyu kesho yake atakuja na bandiko jingine refu akionyesha jinsi Magufuli alivyo dikteta wa kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia watu kuhama!!!

Hebu jiulize ni lini Lisu alitaka kufanya mkutano jimboni kwake akakatazwa?

Huyu Lisu ni kweli haoni wabunge wenzake, akina Heche, Ester Matiko, Msigwa wanavyofanya mikutano kwenye majimbo yao ?

Lisu acha kupotosha watu ,sema tu ukweli uongozi wa chadema umefeli kabisa hivyo wajihuzuru kupisha wengine.
 
Bandiko refu lakini limejaa pumba tupu za kumtetea Mbowe.

Lissu amezungumzia kuweka limitation ya kufanya siasa kwenye eneo ulilochaguliwa Katiba ya Tanzania inaruhusu kufanya siasa popote pale nchini je hilo swala unalizungumziaje? Pia watu wanafunguliwa kesi kwa kufanya siasa jimbo ambalo hawakichaguliwa wakati hakuna sheria inayokataza hivyo naona ujikite kwenye hayo maswali niliyouliza labda andiko la Lissu ni refu sana ukashindwa kulielewa..
 
Sisiem ni chama cha kilicho kufa kwahiyo wanategemea dola waonekana bado wapo hai ila teyari ni maiti.

Dola sasa wanakilinda na kukibeba hiki chama mfu ila harufu ikiwazidia, iko siku hata wao watautupa huu mzoga.

Ni swala la muda tu huu mzoga kila mtu utamshinda kwa harufu yake mbaya na kuamua kutupa.

Ni swala la muda tu.
 
Usitegemee akina Lissu kuandika mzizi wa tatizo Chadema zaidi ya kuzunguka na point zile zile. Zile sarakasi za 2015 ndio sehemu ya tstizo zilizoleta hadi hao wabunge na madiwani wa mafuriko.

Bandiko zima limeiacha chadema kama hawana doa wala kukiri wao kama viongozi ndio chanzo cha haya.

Alafu bila aibu mnasema utawala uliopita uliwapa uwanja wa kufanya siasa ikiwemo maandamano!! Mwangosi alikufaje? mmesahau yote au ndio siasa za matukio?

Mngesema utawala uliopita ulikuwa nafuu kidogo kwa demokrasia lakini struggle ilikuwa pale pale na umma ulikuwa nyuma ya chama kwelikweli.
 
Bandiko refu lakini limejaa pumba tupu za kumtetea Mbowe.

Lisu anajua kabisa kwamba katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama chochote muda wowote kama huko aliko haoni kama anatendewa haki .

Leo Lisu anakuja na bandiko refu kumshawishi rais Magufuli avunje katiba kwa kupiga marufuku watu kuhama chama , alafu ikitokea hivyo ,Lisu huyu huyu kesho yake atakuja na bandiko jingine refu akionyesha jinsi Magufuli alivyo dikteta wa kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia watu kuhama!!!

Hebu jiulize ni lini Lisu alitaka kufanya mkutano jimboni kwake akakatazwa?

Huyu Lisu ni kweli haoni wabunge wenzake, akina Heche, Ester Matiko, Msigwa wanavyofanya mikutano kwenye majimbo yao ?

Lisu acha kupotosha watu ,sema tu ukweli uongozi wa chadema umefeli kabisa hivyo wajihuzuru kupisha wengine.
Sauti na Maandiko ya TL ni ujumbe " kutoka kuzimu" (only God knows why he is alive). Vinagusa hisia na mioyo ya wanaomwamini Mungu.
 
Bandiko zima limeiacha chadema kama hawana doa wala kukiri wao kama viongozi ndio chanzo cha haya.
Soma vizuri hoja zako zote zimeelezwa kwenye hilo bandiko. Wengine mpaka sasa tunajua kwamba kuna makovu kati ya wafuasi wa Slaa ambao waliumia kwa kuachwa kwa mtu wao na tunajua pia kuna tatizo la kumpokea Lowassa bila ya kuweka utaratibu wa jinsi ya yeye kuishi CHADEMA.

Siasa ni matukio!!
 
Anaandika Wakili Msomi #TunduLissu wa CHADEMA, leo October 8, 2018 akitokea nchini Ubelgiji.

Huu mjadala wa hama hama ya Wabunge wa CHADEMA ni muhimu sana. Unahitaji kujadiliwa kwa tahadhari na kwa umakini, vitu ambavyo ni adimu katikati yann kelele na vumbi kubwa vilivyotokana na hama hama hii.

Napendekeza kutafakari mambo yafuatayo ya kufikirisha katika kujaribu kuelewa maana halisi ya hii hama hama:

(1) Kuhama kwa viongozi wa kisiasa kutokana na migogoro na tofauti za kisiasa ndani ya vyama vya siasa sio jambo geni katika historia ya vyama vingi nchi yetu. Hata hivyo, kuhama kwa Wabunge na Madiwani wa upinzani kwenda CCM ni jambo geni.

(a) Kati ya 1995, CHADEMA ilipopata Wabunge wake wa kwanza (walikuwa wanne), na 2015 ilipopata Wabunge 35 wa majimbo na 37 wa Viti Maalum, hakuna Mbunge au diwani hata mmoja aliyejiuzulu ubunge na kujiunga na CCM kwa sababu yoyote ile.

(b) Katika kipindi hicho cha '95 - '15, Wabunge na Madiwani walioondoka CHADEMA na vyama vingine vya upinzani na kuhamia CCM:

(i) ama walifukuzwa kwenye vyama vyao (mfano madiwani 5 wa CHADEMA Arusha, akina Danhi Makanga na Teddy Kasela Bantu wa UDP, n.k.),

(ii) ama walipoteza ubunge wao mahakamani (mfano Makongoro Nyerere, Dr. Lamwai, Kifu Gullamhussein Kifu wa NCCR-Mageuzi, n.k.)

(iii) au walisubiri washindwe ubunge ndio wakahamia CCM (mfano Dr. Amani Walid Kabourou, Saidi Arfi wa CHADEMA na wengineo wengi)

(c) Katika kipindi hicho hicho, waliokuwa wanahama chama wakiwa wabunge na kujiunga na vyama vingine walikuwa wanaCCM (mfano Freddie Mpendazoe).

(2) Katika kipindi hicho chote, licha ya matatizo mengi, hakukuwa na ukandamizaji wa haki za kisiasa na haki za binadamu kwa ujumla kama ilivyo sasa.

(a) Vyama vya siasa vilikuwa vinaendesha mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa.

(i) Leo shughuli za kawaida za kisiasa, kama mikutano ya hadhara, maandamano na hata vikao au semina za ndani, zimepigwa marufuku kabisa.

(b) Viongozi wa vyama vya upinzani hawakuwa walengwa wa moja kwa moja wa ukandamizaji unaoendeshwa na vyombo vya usalama.

(i) Leo karibu viongozi wote wa CHADEMA wa ngazi za juu, wakiwemo Wabunge wengi, na wa ngazi za kati na hata za chini wanakabiliwa na kesi za jinai mahakamani.

(ii) Wengi wa wale ambao bado hawana kesi angalau wameonja mahabusu au kipigo cha polisi kwa kufanya shughuli za kawaida za kisiasa zinazoruhusiwa na sheria zetu.

(iii) Wapo viongozi wameuawa kinyama lakini mauaji yao hayajachunguzwa wala hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

(iv) Wengine wamejeruhiwa vibaya katika mazingira hayo hayo ya kulenga kuwaua au kuwadhuru viongozi wa upinzani.

(c) Haki, hadhi na heshima ya Bunge na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge au katika shughuli za kibunge, zilikuwa zinaheshimiwa. Leo kuwa Mbunge, au diwani au hata Mwenyekiti wa Kijiji au Mtaa wa upinzani, hasa wa CHADEMA, ni adha kubwa.

(i) Leo Wabunge wa upinzani wanapigwa na kudhalilishwa na askari wenye sare za polisi ndani ya Ukumbi wa Bunge.

(ii) Wakitoka nje ya Bunge Wabunge wa upinzani wanatekwa nyara na mapolisi na kusafirishwa usiku kupelekwa Dar Es Salaam au Arusha au Morogoro au kwingineko.

(iii) Leo Wabunge wa upinzani wanakamatwa na kuwekwa mahabusu na baadae kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa kushiriki kwenye mikutano ya hadhara kwenye majimbo yasiyokuwa yao, ambalo halijawahi kuwa kosa la jinai katika nchi yetu.

(3) Ambao wanajiuzulu ubunge na udiwani na kuhamia CCM ni wanaCHADEMA wa aina gani hasa???

(a) Wabunge wote wa CHADEMA ambao wamejiuzulu ubunge na kuhamia CCM ni wanaCHADEMA na Wabunge wapya.

(i) Baadhi, kama Dr. Mollel wa Siha na ole Kalanga wa Monduli, waliingia CHADEMA na bungeni kutokana na wimbi la Lowassa la '15.

(ii) Baadhi, kama Waitara, Ryoba na ole Millya, wana muda mrefu CHADEMA lakini ni Wabunge wapya.

(iii) Ubunge wa upinzani wanaoujua hawa waliohama, ni ubunge wa upinzani wa Tanzania ya Magufuli na Bunge la Spika Ndugai, i.e. ubunge wa adha na mateso, sio ubunge wa heshima wa Bunge la Spika Sitta na Spika Makinda.

(b) Wabunge wenye historia ndefu kwenye CHADEMA au bungeni hawajajiuzulu hata mmoja.

(i) Tofauti na waliohama, hawa wana historia na uzoefu wa mapambano kisiasa ya upinzani nje na ndani ya Bunge.

(ii) Tofauti na waliohama, hawa wana historia na uzoefu wa kutiwa misukosuko mbali mbali na Serikali ya CCM kabla na baada ya kuwa wabunge.

(4) Mazingira ya kuhama hama yakoje??? Swali hili ni muhimu kwa sababu ya ubishani mkubwa uliopo kuhusu madai ya matumizi ya rushwa ili kuwarubuni wanaohama.

(a) Kila aliyehama amerudishwa na CCM kama mgombea wa nafasi ile ile aliyoiacha kwa kujiuzulu, bila hata kufuata utaratibu wa kawaida wa kichama wa kufanya vikao vya uteuzi, n.k.

(b) Viongozi wa CCM na Serikali yake, kuanzia Rais Magufuli mwenyewe na wa chini yake, wametangaza hadharani kwamba kila atakayejiuzulu ubunge au udiwani atarudishwa kugombea nafasi ile ile kwa kupitia CCM na atatangazwa mshindi kwa nguvu. Hata bila ushahidi wa malipo ya fedha, ahadi hizi ni rushwa kwa tafsiri ya rushwa ya sheria za nchi yetu.

(c) Kila aliyejiuzulu ubunge au udiwani na kuhamia CCM amefanya hivyo ili 'kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo'!!!

(i) Hata bila kuhoji ukweli wa sababu yenyewe, inawezekanaje hiyo ndio iwe sababu ya kila mmoja anayejiuzulu na kuhamia CCM???

(ii) Hata bila kuuliza maswali juu ya uhalali wa sababu hiyo, kwa nini wanaojiuzulu sasa wanarudishwa kugombea nafasi zile zile walizoziachia???

(iii) Kwani kujiuzulu ubunge au udiwani wa CHADEMA na baadae kugombea nafasi zile zile kwa CCM ni njia pekee ya kumuunga mkono Magufuli??? Kumbuka, John Shibuda wa CHADEMA na John Cheyo wa UDP walikuwa wakiunga mkono jitihada za Rais Kikwete lakini hawakuwahi kujiuzulu ubunge au uanachama wa vyama vyao.

(iv) Hivi inakuwaje wanaounga mkono jitihada za Rais Magufuli ni wanaCHADEMA peke yao??? Vipi akina Lyatonga Mrema, au Profesa Lipumba, au Dovutwa na wengineo wa vyama vingine??? Au ndio kusema hawa hawana madhara yoyote kwa CCM hata wakibaki kwenye vyama vyao???

(v) Hivi inakuwaje wanaounga mkono jitihada za Rais Magufuli ni Wabunge na Madiwani wa Majimbo na Kata peke yake???

Inawezekanaje Rais Magufuli asiungwe mkono na Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum ambao ndio wengi zaidi bungeni???

Au ndio kusema kujiuzulu kwa Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum hakuna faida yoyote kwa CCM kwa sababu hakupunguzi idadi ya Wabunge na Madiwani wa upinzani???

(vi) Katibu Mwenezi wa CCM, Polepole, amesema kwamba mwisho wa 'kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo' ni December, '18. Kwa nini zuio hilo la CCM linalingana ama kukaribiana na zuio la kikatiba na kisheria kwa chaguzi za marudio??? Je, hii ni bahati mbaya tu au kuna njama iliyofichwa kwenye hii ratiba ya CCM na ratiba iliyowekwa na Katiba na Sheria za Uchaguzi???

(c) Kila aliyehama 'ameshinda' uchaguzi katika mazingira ya matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi na mfumo wa usimamizi wa uchaguzi wenye upendeleo wa wazi wazi kwa CCM. Matokeo yote ya chaguzi za marudio za hivi karibuni ni matokeo ya kupika kati ya wasimamizi wa uchaguzi wanaCCM na vyombo vya usalama vya Serikali ya CCM. Hata Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ali amethibitisha hili in so many words.

(5) Je, tatizo ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe??? Hili nalo limeleta mjadala mkubwa.

(a) Wote waliojiuzulu ubunge na udiwani wa CHADEMA na kujiunga na CCM na wapambe wao wamedai tatizo ni Mwenyekiti Mbowe.

(i) Hata hivyo, waliingia CHADEMA na kuchaguliwa Wabunge au madiwani kwa kupitishwa na vikao vya Chama vilivyoongozwa na Mwenyekiti Mbowe huyo huyo. Baniani mbaya ila kiatu chake dawa!!!

(ii) Mwenyekiti Mbowe hajawahi kuwa kiongozi wa CHADEMA mzuri kwa CCM tangu angalau '05 alipogombea Urais hadi leo hii. Baadhi ya dhambi zake ni pamoja na kuwa Mchagga, mkwe wa Mzee Mtei, Mkaskazini, Mkristo na, sasa, mng'ang'ania madaraka.

(iii) Licha ya 'madhambi' haya makubwa, Mwenyekiti Mbowe ni kiongozi wa upinzani mwenye mafanikio makubwa katika historia ya vyama vingi vya siasa nchini kwetu.

(b) Mwenyekiti Mbowe amelipia mafanikio yake katika siasa za upinzani za Tanzania kwa gharama kubwa sana.

(i) Biashara zake, iwe ni Bilicanas, au uchapishaji magazeti au mashamba ya kilimo, zimeharibiwa na Serikali ya Magufuli ili kulipiza kisasi kwa sababu ya mafanikio yake ya kisiasa.

(ii) Mwenyekiti Mbowe amekamatwa na kushtakiwa kwa jinai kwa sababu za kisiasa kuliko pengine kiongozi mwingine mkuu wa Chama cha siasa katika Tanzania.

(c) Katika viongozi wote Wakuu wa upinzani katika historia ya Tanzania, ni Mwenyekiti Mbowe, na pengine Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF, ambaye amebaki na msimamo thabiti wa kisiasa licha ya mateso makubwa ambayo amepitishwa.

(6) Kujiuzulu kwa Wabunge na Madiwani wa upinzani, hasa CHADEMA, katika mazingira haya kuna madhara kwa CHADEMA na kwa siasa za upinzani kwa ujumla. Je, ni madhara gani hayo na ni makubwa kiasi gani kwa CHADEMA na kwa siasa za upinzani???

(a) Ni wazi wapo viongozi, wanachama, wafuasi na wananchi waliokatishwa, na watakaokatishwa, tamaa na matukio haya. Je, ni wengi kiasi gani???

(b) Kama hama hama hii ina madhara makubwa kwa upinzani kama inavyoelezwa na baadhi yetu, ni kwa nini kuna matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi na kila aina ya ubabe na hila kwenye chaguzi za marudio???

(c) Kama 'upinzani unakufa' kama inavyoelezwa, kwa nini Serikali ya Magufuli inaendelea kukataza uhuru wa vyama vya siasa vya upinzani kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria zetu??? Kwa nini bado kuna makatazo ya Bunge Live??? Kwa nini kuna ukandamizaji wa vyombo vya habari na uhuru wa maoni???

(d) Kama hama hama hii ina madhara makubwa kwa upinzani, kwa nini bado wananchi wetu wanahudhuria kwa maelfu katika mikutano ya hadhara michache inayoruhusiwa wakati wa kampeni za chaguzi za marudio???

Haya ni baadhi ya masuala yanayohitaji kujadiliwa kama sehemu ya mjadala wa hama hama ya Wabunge na Madiwani wa upinzani. Nawataka radhi kwa kuwasubirisha muda mrefu.
Umenena vyema
 
Bandiko refu lakini limejaa pumba tupu za kumtetea Mbowe.

Lisu anajua kabisa kwamba katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama chochote muda wowote kama huko aliko haoni kama anatendewa haki .

Leo Lisu anakuja na bandiko refu kumshawishi rais Magufuli avunje katiba kwa kupiga marufuku watu kuhama chama , alafu ikitokea hivyo ,Lisu huyu huyu kesho yake atakuja na bandiko jingine refu akionyesha jinsi Magufuli alivyo dikteta wa kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia watu kuhama!!!

Hebu jiulize ni lini Lisu alitaka kufanya mkutano jimboni kwake akakatazwa?

Huyu Lisu ni kweli haoni wabunge wenzake, akina Heche, Ester Matiko, Msigwa wanavyofanya mikutano kwenye majimbo yao ?

Lisu acha kupotosha watu ,sema tu ukweli uongozi wa chadema umefeli kabisa hivyo wajihuzuru kupisha wengine.

Nina uhakika hujasoma andiko lote kwa sababu huna akili ya kusoma na hata kama umesoma basi hujaelewa kwani mantiki anayozungumzia Lissu iko juu saaaana ya uwezo wako wa kuelewa kwani umebakishiwa akili ya kumshambulia Mbowe tu humu
 
Hivi Tundu Lisu hata ana watoto? Kwa maana anajipenda balaa, sijawahi kuona Binadamu anapenda kujiongelea kama Tundu Lisu, utafikiri yeye ndo wa kwanza kupigwa risasi Dunia hii!
 
Bado tunatatizo kubwa la ujinga na umasikini hasa wa fikira. Ni aibu leo hii mtu anatumia rasilimali za taifa kwa mtazamo mwepesi tu wa kijinga na kishamba kupoteza mabilioni na kubwa zaidi kuharibu umoja na ustawi wa taifa letu.
Waandishi Tumieni taaluma yenu wekeni clips Watz waliovitandani karibu kufa kwa kukosa huduma bora,elimu nk huku mfalme anafanya kufuru.
 
Bandiko refu lakini limejaa pumba tupu za kumtetea Mbowe.

Lisu anajua kabisa kwamba katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama chochote muda wowote kama huko aliko haoni kama anatendewa haki .

Leo Lisu anakuja na bandiko refu kumshawishi rais Magufuli avunje katiba kwa kupiga marufuku watu kuhama chama , alafu ikitokea hivyo ,Lisu huyu huyu kesho yake atakuja na bandiko jingine refu akionyesha jinsi Magufuli alivyo dikteta wa kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia watu kuhama!!!

Hebu jiulize ni lini Lisu alitaka kufanya mkutano jimboni kwake akakatazwa?

Huyu Lisu ni kweli haoni wabunge wenzake, akina Heche, Ester Matiko, Msigwa wanavyofanya mikutano kwenye majimbo yao ?

Lisu acha kupotosha watu ,sema tu ukweli uongozi wa chadema umefeli kabisa hivyo wajihuzuru kupisha wengine.
Hebu soma tena vizuri mkuu.. rudia tena
 
Usitegemee akina Lissu kuandika mzizi wa tatizo Chadema zaidi ya kuzunguka na point zile zile. Zile sarakasi za 2015 ndio sehemu ya tstizo zilizoleta hadi hao wabunge na madiwani wa mafuriko.

Bandiko zima limeiacha chadema kama hawana doa wala kukiri wao kama viongozi ndio chanzo cha haya.

Alafu bila aibu mnasema utawala uliopita uliwapa uwanja wa kufanya siasa ikiwemo maandamano!! Mwangosi alikufaje? mmesahau yote au ndio siasa za matukio?

Mngesema utawala uliopita ulikuwa nafuu kidogo kwa demokrasia lakini struggle ilikuwa pale pale na umma ulikuwa nyuma ya chama kwelikweli.

Kwani Mwangosi alikuwa Chadema au mwanahabari?!
 
Back
Top Bottom