MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,432
Wakuu,
Kampeni za uchaguzi zinaendelea na kwasababu ya mabadiliko makubwa ya kiushawishi ya Tundu Lissu yanayomfanya ajipatie mashabiki kwa kasi ambayo wengi (ikiwemo mimi) hatukutegemea, nimeona niandike machache kwanini anafanikiwa;
1) Lissu alianza vibaya kampeni kwa hotuba zake kujaa hoja za kiharakati ambazo haziongezi kura. Mashambulizi binafsi kwa mgombea wa CCM yalijaa jeuri isiyojenga wala kuongeza kura hivyo kuonekana na umma kama mwanaharakati zaidi ya amri jeshi mkuu mtarajiwa.
2) Hoja namba moja ndio kiini cha Lissu kujirekebisha na kubadili upepo wa kampeni. Lissu akaanza kuacha kumzungumzia sana mgombea wa CCM na kujikita kwenye shida za watu.
3) Chadema wametafiti na kutambua maeneo ambayo hayajafanyiwa kazi na kujikita huko kuliko kuponda tu miradi ambayo hoja yao imekuwa haieleweki na wananchi wengi. Sasa Lissu anazungumza habari za bei ya Cement, kupandisha mishahara, Fao la kujitoa n.k
4) Lissu ameanza kuheshimu vyombo vya dola na hata leo amewasifia. Hii ni mbinu ya kuwachota kisaikolojia askari na watumishi wengine ili wapate ushirikiano wao kikamilifu. Nafikiri hii itazidi kumuongezea wafuasi maana anajipambanua kama Amri Jeshi mkuu mtarajiwa.
5) Pamoja na ukubwa wa CCM lakini uchaguzi huu wana tatizo kubwa kupangua hoja kwenye maeneo ambayo hawakufanya vizuri. Kwanza wanaonesha hawajui vision ya mgombea wao toka alipoingia madarakani. JPM amefanya kazi nzuri sana lakini kuna maeneo hakufanya vizuri na lazima wajipange kutoa majibu ya wazi maana Chadema wamejikita huko.
6) Kwa ujumla tulitegemea kampeni zitazotawaliwa na CCM kutokana na upinzani kuwa nusu kaputi kwa muda mrefu lakini Lissu amebadili upepo na kufanya tushuhudie moja ya uchaguzi ambao hoja ndio zitazotawala na kutoa fursa kwa wananchi kuamua yupi atawafaa.
7) Pia mnyonge mnyongeni haki yake apewe. JPM anakwenda kuandika historia ya kuendesha uchaguzi kistaarabu bila vurugu tulizoshuhudia chaguzi zilizopita. Kwasababu wengi tunasahau lakini chaguzi zilizopita ziligubikwa na mengi. Pamoja na mapungufu machache lakini kampeni zinakwenda vyema na tuendelee kuomba hali ibaki hivi hadi mwisho.
Hakika Tundu A. Lissu amebadili upepo na kuleta ladha halisi ya kampeni za ushindani kihoja.
Asanteni,
MTAZAMO.