Tundu Lissu: Mamlaka ya Rais yana ukomo

Tundu Lissu: Mamlaka ya Rais yana ukomo

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,694
Reaction score
58,737
Mwanasheria wa Mkuu CHADEMA, Tundu Lissu amesema Katiba ya mwaka 1965 ilifuta vyama vingi ikabaki TANU hali iliyoondoa uwezekano kikatiba wa kupinga au kukosoa utawala wa Awamu ya Kwanza bila kukabiliwa na nguvu za dola na kushtakiwa.

Lakini marekebisho ya mwaka 1992 yaliyotokana na Waraka Na 1 wa Serikali, yalirejesha mfumo wa vyama vingi ambamo ndani kuna uhuru na haki kisheria na kikatiba kuipinga na kuikosoa Serikali.

Mwanasheria huyo amesema kwa kuzingatia Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, kuipinga na kuikosoa Serikali si uhaini wala kosa kwani vyama vya upinzani vimepata uhalali huo kisheria na ndiyo maana vinasema haviwezi kuona Serikali ya Rais John Magufuli ikitumia mamlaka isiyokuwa nayo kwa kusigina Katiba na sheria.

Amesema tofauti kubwa kati ya utawala wa Mwalimu Nyerere na Rais Magufuli ni mamlaka waliyonayo kikatiba.

Chanzo: Mwananchi
 
Attachments

  • 1472454139738.jpg
    1472454139738.jpg
    58 KB · Views: 80
Lissu endelea kutufunua macho wengi walidhani anachokisema Rais wa nchi hakuna mamlaka yeyote inaweza kupinga, kuhoji wala kunon'gona kufanya hivyo ni kosa, tulidhani madaraka yake hayana ukomo!! Bado watu wengi hatujajua pia madaraka ya Mahakama, Bunge na Serikali kuu, muingiliano wa mihimili hii ya nchi na uhuru wa kila kimoja wakati wa kutekeleza majukumu yake kikatiba.
 
Hata mamlaka ya wakosoaji/ upinzani pia yana ukomo. Mnapaswa kuelewa sheria ni upanga ukatao kuwili.
 
Tundu Lisu anaingea vitu hewa sana. Hebu mwambieni ataja ni kifungu kipi kinaongelea ukomo wa rais.
 
Mwanasheria wa Mkuu CHADEMA, Tundu Lissu amesema Katiba ya mwaka 1965 ilifuta vyama vingi ikabaki TANU hali iliyoondoa uwezekano kikatiba wa kupinga au kukosoa utawala wa Awamu ya Kwanza bila kukabiliwa na nguvu za dola na kushtakiwa.

Lakini marekebisho ya mwaka 1992 yaliyotokana na Waraka Na 1 wa Serikali, yalirejesha mfumo wa vyama vingi ambamo ndani kuna uhuru na haki kisheria na kikatiba kuipinga na kuikosoa Serikali.

Mwanasheria huyo amesema kwa kuzingatia Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, kuipinga na kuikosoa Serikali si uhaini wala kosa kwani vyama vya upinzani vimepata uhalali huo kisheria na ndiyo maana vinasema haviwezi kuona Serikali ya Rais John Magufuli ikitumia mamlaka isiyokuwa nayo kwa kusigina Katiba na sheria.

Amesema tofauti kubwa kati ya utawala wa Mwalimu Nyerere na Rais Magufuli ni mamlaka waliyonayo kikatiba.

Chanzo: Mwananchi
Sasa mbona mwanasheria mkuu wa hii serikali anajichanganya?
 
Lisu ni mwanasheria uchwala, au hajui kusoma, au akisoma haelewi, katiba yetu imempa Rais mamlaka mkubwa hadi kumweka mtu kizuizini! Na kukosa kuna mpaka, na si lazima ukosoe kwa maandamano
 
Lissu ndiyo baba wa taaluma ya sheria hapa Tanzania, si yule wanayemwita sijui Mchecheto Masajuuu.
 
Pinga kwa hoja acha mambo ya kike kike!

Jipeleke huko piga zako...na zijasoma sababu mwanzoni ilikuwa kupande cha ukurasa wa gazeti tu. So kama sitaki kusoma yaliyowekwa sasa hayo maandishi na kuandika kitu ni uamuzi wangu na sisukumwi hata kachu
 
Ujue kunamagonjwa mengine huwa hayaponi ila hutulia tu ndiyo maana watu kama LISU hajapona kivile baada ya mda hupanda na kushuka.
 
Back
Top Bottom