Tundu lissu kurudi nchini mwakani

Tundu lissu kurudi nchini mwakani

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
26,597
Reaction score
29,530
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu hatafanyiwa upasuaji mwingine na ataendelea kubaki na risasi moja kwenye uti wa mgongo.

Hayo yameelezwa leo Agosti 29 na kaka yake Lissu, Wakili Alute Lissu, alipozungumza na wanahabari.

Amesema Lissu hatafanyiwa upasuaji mwingine baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara nne akiwa Ubelgiji ingawa kuna risasi moja ambayo bado imebaki nyuma ya uti wa mgongo.

“Wakijaribu kuitoa huenda ikaathiri uti wa mgogo na hivyo kupata tatizo la kupooza,"amesema.

Lissu alihamishiwa hospitali ya Leuven iliyopo Ulelgiji akitokea hospitali ya Nairobi, baada ya kushambuliwa kwa risasi kadhaa na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka jana.

Alute ambaye amerejea nchini, wiki hii akitokea Ubelgiji kumjulia hali Lissu, amesema huenda mwanasiasa huyo akarejea nchini mwakani, hasa kutokana na mfupa wa mguu wa kulia kuwa bado haujaunga vizuri.

"Hali ya Lissu inaendelea vizuri, lakini napenda kukanusha taarifa kuwa kuna kamati ya mapokezi yake kwani, Lissu kwa hali yake hawezi kurejea nchini hivi karibuni, kutokana na kuendelea na matibabu nje ya hospitali,’’ amesema.

Wakili Mughwai amesema bado Lissu hajapata ruhusa ya moja kwa moja kutoka kwa daktari wake hivyo atakuwa akipatiwa huduma kwenye nyumba aliyopanga jirani na hospitali hiyo ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.

"Haiwezekani kurudi karibuni, mimi nadhani labda mwakani hasa kutokana na kuhitaji uangalizi wa daktari wake, ingawa yeye binafsi na hata sisi wanafamilia tungependa arudi mapema,"amesema.

Amesema risasi hiyo imeachwa kwa sababu haina athari kwa maisha ya Lissu, kwani si mara ya kwanza, wagonjwa kubaki na risasi mwilini kwani itasababisha madhara makubwa zaidi kama ikitolewa.

Hata hivyo, Wakili Mughwai amesema wanashukuru sana Watanzania wote wakiwepo wanaoishi Ubelgiji kutokana na michango wanayotoa kumsaidia Lissu na kwenda kumjulia hali nchini Ubelgiji.
 
Kupona kwake na kubaki na bila ulemavu ni kitendawili na muujiza wenye maono makubwa ndani yake.... Ama kweli kama zako bado kutimia, utakiponyoka kifo kwa namna ya kushangaza mno...
Kiroho tafsiri yake ni pana zaidi ya tafsiri za kibinadamu kwenye mijadala rahisi

Jr[emoji769]
 
Hela za kupanga hiyo nyumba anatoa wapi?

Mkewe anabeba boksi huko Ubelgiji?
 
Mungu amfanyie wepesi,apone na arejee kuwakilisha waliomchagua.
Hao waliojipa kazi ya kumtoa uhai,angali wanapumua,waonje adha ya dhambi ya mauaji na familia zao.
 
Hela za kupanga hiyo nyumba anatoa wapi?

Mkewe anabeba boksi huko Ubelgiji?

Camarada;
mbona umekimbilia kwenye malipo zaidi kuliko kumtakia uhai zaidi hata wa siku moja tu?? Usijali, ila ka huyo mkewe amekuambia amejiuza mno huko, basi uguswe moyo umsaidie angalao $ 2 zitamsaidia pia.
Tuwe na ubinadamu zaidi kuliko uchu
 
Back
Top Bottom