Tundu Lissu kurindima mkoa wa Songwe leo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mgombea Urais wa Tanzania Tundu Lissu leo anaingia mkoani Songwe kuendeleza harakati zake za kuingia Ikulu.Kabla ya kuingia Songwe atamalizia mkutano saa 5 asubuhi mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini

Mgombea huyo wa Chadema mwenye ushawishi mkubwa na ambaye kila dalili zinaonyesha atashinda Urais amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu kokote kule anakopita.

Mikutano yote ya shujaa huyo wa #UhuruHakiNaMaendeleoyawatu imekuwa ikifurika watu majiani wenye bashasha na Shangwe za Ukombozi wa Mara ya Pili.

Imekuwa ni Tofauti kubwa na mpinzani wake ambaye watu wamemchoka kutokana na kuonyeshwa na Televisheni ya Taifa kila mkutano anaofanya huku ikiwa imejaa watoto wa shule , wanamuziki zaidi ya mia moja na kusombwa watu kwa malori.

Lissu amekuwa Tumaini la watu wote wakiwemo wafanyabiashara ambao amesema ataondoa Kodi za manyanyaso, wakulima ambao atawapa Uhuru wa kuuza mazao yao wanakotaka na Wafanyakazi ambao ameahidi kuwaongezea mshahara wote walionyimwa kinyume Cha Sheria kwa miaka mitano na pia kuwarejeshea Fao la Kujitoa wanaoacha kazi kabla ya muda wa kustaafu na kufutilia mbali Sheria Kandamizi ya watu kusubiri mpaka miaka 60 ndiyo mtu apate Mafao yake kutoka mifuko ya Jamii.

Molemo Media Tutakuwa Live hapa kuwaletea kila kitakachojiri

IMG-20200915-WA0131.jpg

Mbalizi
Tundu Lissu amelakiwa na umati mkubwa wa watu mjini Mbalizi huku akina mama wakitandika kanga zao chini na kumshsngilia kwa kupeperusha majani ya miti.

Lissu amelaani vikali Sana kauli ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba itawapa adhabu wagombea wanaotoa kauli za kuvunja Amani ikiwemo kuzuiwa kufanua kampeni.

Lissu amemtaka Mkurugenzi wa Uchaguzi na Tume yake kuuleza umma wamefanya Nini kuhusu mgombea wa CCM kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.

Lissu amesema mgombea wa CCM amekuwa akitisha watu watakaochagua Upinzani kwamba hawatapelekewa Maendeleo lakini Tume imekaa kimya.

Pia Lissu amesema ni marufuku kabisa kutumia madaraka yako kutoa ahadi na akasema mgombea wa CCM akiwa Sengerema alimpigia simu Mkurugenzi mkuu wa Tanroads aende kujenga Barabara katikati ya mkutano wa kampeni kinyume na kanuni za uchaguzi.

Pia Lissu amesema kokote anakopita mgombea wa CCM shule zinafungwa na watoto wanashurutishwa kwenda kwenye mikutano ya kampeni kinyume kabisa na kanuni za maadili lakini Tume ya Uchaguzi imekaa kimya.

Lissu amesisitiza kwamba hakuwezi kuwa na Amani mahali penye wizi wa kura na Chadema inasisitiza ili Amani itawale kwenye uchaguzi mkuu huu isiibiwe kura hata moja.Vinginevyo kamwe Chadema haitakubali upumbavu wa wizi wa kura ama kumtangaza asiyeshinda.
 
Attachments

  • VID-20200916-WA0034.mp4
    7.9 MB
  • VID-20200916-WA0090.mp4
    8.9 MB
  • VID-20200916-WA0092.mp4
    11.6 MB
  • VID-20200916-WA0091.mp4
    5.4 MB
Mgombea Urais wa Tanzania Tundu Lissu leo anaingia mkoani Songwe kuendeleza harakati zake za kuingia Ikulu.

Mgombea huyo wa Chadema mwenye ushawishi mkubwa na ambaye kila dalili zinaonyesha atashinda Urais amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu kokote kule anakopita.

Mikutano yote ya shujaa huyo wa #UhuruHakiNaMaendeleoyawatu imekuwa ikifurika watu majiani wenye bashasha na Shangwe za Ukombozi wa Mara ya Pili.

Imekuwa ni Tofauti kubwa na mpinzani wake ambaye watu wamemchoka kutokana na kuonyeshwa na Televisheni ya Taifa kila mkutano anaofanya huku ikiwa imejaa watoto wa shule , wanamuziki zaidi ya mia moja na kusombwa watu kwa malori.

Lissu amekuwa Tumaini la watu wote wakiwemo wafanyabiashara ambao amesema ataondoa Kodi za manyanyaso, wakulima ambao atawapa Uhuru wa kuuza mazao yao wanakotaka na Wafanyakazi ambao ameahidi kuwaongezea mshahara wote walionyimwa kinyume Cha Sheria kwa miaka mitano na pia kuwarejeshea Fao la Kujitoa wanaoacha kazi kabla ya muda wa kustaafu na kufutilia mbali Sheria Kandamizi ya watu kusubiri mpaka miaka 60 ndiyo mtu apate Mafao yake kutoka mifuko ya Jamii.

Molemo Media Tutakuwa Live hapa kuwaletea kila kitakachojiri
Mlowo kwa kamanda Haonga! Safi sana! Na Tunduma kwa Mwakajoka akimnyunyizia Silinde moto utawaka!
 
Bunge zima!
Ila wakuu mwambieni jamaa yenu alikosea sana kufuta fao la kujitoa. Inaonyesha wazi kuwa jamaa hana uchungu na walala hoi. Hilo fao ndio mtaji wa maskini. Unapomzuia kuchukua hela yake mpaka afikishe umri wa kustaafu lengo lako si ni kumharibia kabisa maisha. Huyo jamaa yenu alikosea sana kusema ukweli. Huo ni zaidi ya unyama.
 
Wafanyakazi wa Serikali kwa awamu hii wamefutiwa fao la kujitoa na pia hawakupandishiwa mishahara, CCM hapa ina kazi ya kuwajibu Wafanyakazi ili kuwarejeshea matumaini!
 
Mgombea Urais wa Tanzania Tundu Lissu leo anaingia mkoani Songwe kuendeleza harakati zake za kuingia Ikulu.

Mgombea huyo wa Chadema mwenye ushawishi mkubwa na ambaye kila dalili zinaonyesha atashinda Urais amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu kokote kule anakopita.

Mikutano yote ya shujaa huyo wa #UhuruHakiNaMaendeleoyawatu imekuwa ikifurika watu majiani wenye bashasha na Shangwe za Ukombozi wa Mara ya Pili.

Imekuwa ni Tofauti kubwa na mpinzani wake ambaye watu wamemchoka kutokana na kuonyeshwa na Televisheni ya Taifa kila mkutano anaofanya huku ikiwa imejaa watoto wa shule , wanamuziki zaidi ya mia moja na kusombwa watu kwa malori.

Lissu amekuwa Tumaini la watu wote wakiwemo wafanyabiashara ambao amesema ataondoa Kodi za manyanyaso, wakulima ambao atawapa Uhuru wa kuuza mazao yao wanakotaka na Wafanyakazi ambao ameahidi kuwaongezea mshahara wote walionyimwa kinyume Cha Sheria kwa miaka mitano na pia kuwarejeshea Fao la Kujitoa wanaoacha kazi kabla ya muda wa kustaafu na kufutilia mbali Sheria Kandamizi ya watu kusubiri mpaka miaka 60 ndiyo mtu apate Mafao yake kutoka mifuko ya Jamii.

Molemo Media Tutakuwa Live hapa kuwaletea kila kitakachojiri
Anarindima amekuwa Lori?
 
Hivi!! Kwa kawaida mtu humchukua siku ngapi kujua kwamba, kitu anachokitafuta hakitawezekana kukipata ili pengine aachane nacho na aanze kujishughurisha na mambo mengine?

MMbona anapoteza muda huyu Kijana na mjuvi wa Sheria za Tz?
 
Back
Top Bottom