Tundu Lissu kurejea nchini

Tundu Lissu kurejea nchini

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,073
Kutokana na taarifa iliyotolewa asubuhi hii na shirika la utangazaji la BBC, amenukuliwa mwanasiasa maarufu wa Chama cha Chadema, Tundu Lissu, akisema kuwa hivi sasa ameshatoka hospitalini na anatarajia kurejea nchini wakati wowote kuanzia sasa

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi zisizopungua 30, mwezi September mwaka jana huko jijini Dodoma na watu wasiojulikana

Amekuwa akitibiwa nje ya nchi jijini Nairobi na baadaye nchini Ubelgiji kwa takribani miezi 11 hivi sasa

Alipoulizwa na mtangazaji Zuhura Yunus, kuhusu usalama wake akirejea nchini Tanzania kwa sasa, mwanasiasa huyo alijibu kuwa ni kweli analazimika kuchukua tahadhari kubwa sana ya usalama wake atakaporejea nchini kwa kuwa wale waliotaka kumwua hadi leo hawajapatikana

Akiongelea hali ya kisiasa hapa nchini, alijibu kuwa wapinzani nchini Tanzania, hususani wa chama kikuu cha upinzani nchni cha Chadema, kwa sasa wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana ambayo hayajawahi kutokea tangu turejee katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kwa kuwa viongozi wakuu wote wa Chadema wanasumbuliwa na kesi zisizo kuwa na mwisho karibu kila siku katika Mahakama zetu nchini, ambapo inawapa wakati mgumu sana kuwatumikia wananchi wao waliowachagua katika majimbo yao

Mwenyezi Mungu mjalie na umkinge na watesi wake Tundu Lissu, ambaye ndiye shujaa wa kisiasa nchini Tanzania hivi sasa
 
Kutokana na taarifa iliyotolewa asubuhi hii na shirika la utangazaji la BBC, amenukuliwa mwanasiasa maarufu wa Chama cha Chadema, Tundu Lissu, akisema kuwa hivi sasa ameshatoka hospitalini na anatarajia kurejea nchini wakati wowote kuanzia sasa

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi zisizopungua 30, mwezi September mwaka jana huko jijini Dodoma na watu wasiojulikana

Amekuwa akitibiwa nje ya nchi jijini Nairobi na baadaye nchini Ubelgiji kwa takribani miezi 11 hivi sasa

Alipoulizwa na mtangazaji Zuhura Yunus, kuhusu usalama wake akirejea nchini Tanzania kwa sasa, mwanasiasa huyo alijibu kuwa ni kweli analazimika kuchukua tahadhari kubwa sana ya usalama wake atakaporejea nchini kwa kuwa wale waliotaka kumwua hadi leo hawajapatikana

Akiongelea hali ya kisiasa hapa nchini, alijibu kuwa wapinzani nchini Tanzania, hususani wa chama cha Chadema, kwa sasa wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana ambayo hayajawahi kutokea tangu turejee katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kwa kuwa viongozi wakuu wote wa Chadema wanasumbuliwa na kesi zisizo kuwa na mwisho karibu kila siku katika Mahakama zetu nchini, ambapo inawapa wakati mgumu sana kuwatumikia wananchi wao waliowachagua katika majimbo yao

Mwenyezi Mungu mjalie Tundu Lissu ambaye ndiye shujaa wa kisiasa nchini Tanzania hivi sasa
Mmmmh bora abaki huko watammalizia
 
namshauri aishi kwa tahadhali sana maana wale jamaa mioyoni mwao wamesha jiwekea bango kama hili
images.jpeg
 
namshauri aishi kwa tahadhali sana maana wale jamaa mioyoni mwao wamesha jiwekea bango kama hili
View attachment 848999
Ni kweli inabidi achukue tahadhari ya maisha yake maradufu, kwa kuwa taarifa hii ya kurejea nchini haitawafurahisha wale wote waliopanga njama za kummaliza..........
 
Mmmmh bora abaki huko watammalizia
Hawezi kubaki ughaibuni......

Hata Mzee Mandela angeweza kubaki Tanzania kule Mazimbu Morogoro, wakati ule wa mapambano ya ukaburu kule Afrika Kusini, lakini aliamua kijasiri kurejea Afrika Kusini na Mahakama za kikaburu zikamuhukumu kifungo cha maisha jela.....

Akakaa Jela miaka 28 na hatimaye Makaburu wa Afrika Kusini wakaona bora yaishe na wakamtoa gerezani na akawa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuwa Rais wa Afrika Kusini na amekuwa ndiye "celebrity" maarufu zaidi duniani katika karne ya 20
 
Back
Top Bottom