johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 86,491
- 147,265
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu amesema Jukumu kubwa lililo mbele ya Watanzania wote wakati huu tunapoisaka Katiba Mpya ni Kufuta Ujinga, kwa sababu Ujinga wa Taifa unawarahisishia Watawala kutenda wapendavyo
Lisu anasema Tanzania imegeuka kuwa Taifa linaloabudu miungu Watu ambao ndio huwapangia wengine maisha yao yaweje
Akihutubia maelfu ya Wananchi kwenye Viwanja Vya Mwembeyanga Tundu Lisu amesema miaka 17 iliyopita walitangaza orodha ya Mafisadi Uwanjani Hapo wakiwemo Marais wawili na Waziri mkuu mmoja ambaye alijiuzulu baadae, lakini Ufisadi uliopo sasa unazidi mara mia ya Ule
Lisu ametoa mfano wa vifo vya Watu waliokufa Rufiji kwa Mafuriko na kuhoji ni nani aliyeruhusu bwawa lifunguliwe?
Aidha Lisu amesema kuna Wizi wa kutisha kwenye Halmashauri zetu lakini kwa sababu Taifa limemwacha Mungu wa Mbinguni na Kuabudu miungu Watu hakuna anayehoji na badala yake wanajinyenyekeza kwa Wezi Ili nao waonekane wa maana mtaani
Katika mkutano huo Wananchi wameazimia Tundu Lisu anunuliwe Gari Imara litakalomwezesha kuzunguka Nchi nzima kuwafuta Tongotongo Wananchi Ili macho yao yaweze kuona tena kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere
Tundu Lisu amezungumza mambo mengi lakini kama mjuavyo mimi siyo Mwandishi wa Gazeti kama Lucas
Ahsanteni na Pokeeni Baraka za Mungu wa Mbinguni 😀😀
Kwako Erythrocyte pale Kajunjumele - Kyela 😂😂🔥