Tundu Lissu: Hali ya nchi kiuchumi inazidi kuwa mbaya zaidi, viwanda vinafungwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Tundu Lissu

Kwanza, nawasalimu makamanda wote na wapenda Maendeleo wote. Nawapa somo (Elimu Elimu Elimu).

Ile Benki yenye picha ya ndege imewatangazia wafanyakazi wake kuwa ipo kwenye hali tete, wakae sawa kwa lolote litakalotokea hiyo ni kwa hapa kwetu tu, ila nchini kwao iko vizuri na kwenye nchi nyingine iko vizuri pia kutokana na mifumo mizuri ya huko.

Kumbuka kuna benki nyingine hivi karibuni, ile yenye jina la mnyama mwenye shingo ndefu ilitangazwa kuwa ipo kwenye hali tete, pamoja na hilo kuna Benki nyingine iliyokuwa kila mara inajitangaza kupata faida nayo imepata hasara mwaka huu tutegemee kupata wategemezi wengi sana kwenye familia kuanzia mwaka 2017.

Turudi tena kwenye point moja upende usipende wewe au mimi au wa kijani (rangi ya mboga mboga) mjue tunaenda kwenye hali mbaya sana ya kiuchumi, tunaenda kusoma namba, na Mzee wetu hataki kusikia hiki watu wanachokilalamikia, anaongeza sheria tu,
siri-kali hailipi madeni ya ndani ila inadai kodi tu, kama unadaiwa na Benki kwa kukopa hiyo ni shauri yako.

Na hivi karibuni mmemwona kada maarufu wa kijani (aliyekuwa anasisitiza ujasiriamali) anaidai siri-kali ila hajalipwa, izingatiwe amekopa benki na atafilisiwa muda si mrefu na ataisoma namba kwani mali zake zitapigwa mnada.

Nimetolea mfano mmoja tu kuna wananchi wengi tu mfano wahandisi, wafanyabiashara waliiuzia bidhaa siri-kali au kutengeneza miundo mbinu ya siri-kali hawajalipwa ila wanadaiwa kodi tu na vitisho chungu mbovu na makampuni yao wamekopa benki wanashindwa kurejesha mikopo hiyo, Vilevile yanashindwa kulipa kodi.

Sasa swali ni hili je?...
1. Mkifirisi mali zao na hamtaki kulipa madeni wanayowadai mtapata wapi kodi kama hizo kwa kiwango kile kile tena baada ya kufilisi?

2. Na je, wafanyakazi watakao achishwa kazi kwenye kampuni mtakazo filisi mali zao watapata wapi kazi tena katika kipindi hiki kigumu.

3. Na pia, jiulize kwa watakao maliza vyuoni na wenyewe watapata wapi tena kazi wakati wenzao waliopo kwenye kazi wanapunguzwa.

4. Na ukianzisha ujasiriamali kabla hujaanza biashara kodi unatakiwa ulipe kwanza, kwa makadirio watakayo kukadiria wao siri-kali.

a) Usilete ushabiki wa kijani jiulize wewe unayefanya kazi kama uko salama?

b) Pengine utasema tuvumilie mambo yatakuwa mazuri , tafakari ujue wengi watakuwa omba omba na uharifu utaongezeka, na uharifu ukiongezeka watu watapandwa na hasira, na wakipandwa na hasira watamgeukia nani?

c) Mfano wewe mmoja ukibahatisha kazi nzuri utawasaidia ndugu zako au zetu wangapi?

Usitumie hasira kujibu!
 
Baadhi ya maswali hayo hata mimi nimekuwa nikijiuliza na kwakweli sipati majibu.

Maswali mengine:

Mfanyabiashara gani hivi sasa atathubutu kwenda benki kuchukua mkopo wakati biashara zinadorora?

Mabenki haya bila kutoa mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara yata-survive?

Mabenki haya yaki-recover madeni huku hayakopeshi tena ndio suluhisho?

Kwanini serikali isitangaza kuwa uhakiki wa watumishi wa umma umekamilika ili mabenki sasa yaanze kutoa mikopo?

Viongozi wetu hawa kweli wanaitakia mema nchi hii?

Inafika hatua mtu unaanza kujiuliza hivi hawa watu ni watanzania kweli?Mbona hawashitushwi na hali hii?

Uchumi ukiharibika,viongozi hawa watakuwa na haki na uhalali wa kutuomba radhi watanzania kuwa walifanya makosa ya kibinadamu ili hali leo hii hawataki kusikia la mtu?

Inaumiza sana kwakweli!
 
Wangelipa madeni ya ndani maana hali ni ngumu sana.... kufanya kazi na sirikali na ukalipwa kwa muda inabidi ushukuru sana..... hata kama wanajipanga, walipe kazi za mwanzo hasa za wakandarasi na walio supply vitu kabla ya kuanzisha kazi nyingine, hali ni ngumu sana...
 
Kama anajiamini kwa kile anachokiandika kwa nini asitaje majina ya hizo benki?

Kama akitaja na wakampeleka mahakamani si tunaambiwa ni mwanasheria nguli na hushinda kila kesi? Hii tena itakuwa ni kesi eahisi sana kushinda kwa sababu ukweli anao mikononi.

The man is just playing politics!
 
Tundu Lissu

Kwanza, nawasalimu makamanda wote na wapenda Maendeleo wote. Nawapa somo (Elimu Elimu Elimu).

Ile Benki yenye picha ya ndege imewatangazia wafanyakazi wake kuwa ipo kwenye hali tete, wakae sawa kwa lolote litakalotokea hiyo ni kwa hapa kwetu tu, ila nchini kwao iko vizuri na kwenye nchi nyingine iko vizuri pia kutokana na mifumo mizuri ya huko.

Kumbuka kuna benki nyingine hivi karibuni, ile yenye jina la mnyama mwenye shingo ndefu ilitangazwa kuwa ipo kwenye hali tete, pamoja na hilo kuna Benki nyingine iliyokuwa kila mara inajitangaza kupata faida nayo imepata hasara mwaka huu tutegemee kupata wategemezi wengi sana kwenye familia kuanzia mwaka 2017.

Turudi tena kwenye point moja upende usipende wewe au mimi au wa kijani (rangi ya mboga mboga) mjue tunaenda kwenye hali mbaya sana ya kiuchumi, tunaenda kusoma namba, na Mzee wetu hataki kusikia hiki watu wanachokilalamikia, anaongeza sheria tu,
siri-kali hailipi madeni ya ndani ila inadai kodi tu, kama unadaiwa na Benki kwa kukopa hiyo ni shauri yako.

Na hivi karibuni mmemwona kada maarufu wa kijani (aliyekuwa anasisitiza ujasiriamali) anaidai siri-kali ila hajalipwa, izingatiwe amekopa benki na atafilisiwa muda si mrefu na ataisoma namba kwani mali zake zitapigwa mnada.

Nimetolea mfano mmoja tu kuna wananchi wengi tu mfano wahandisi, wafanyabiashara waliiuzia bidhaa siri-kali au kutengeneza miundo mbinu ya siri-kali hawajalipwa ila wanadaiwa kodi tu na vitisho chungu mbovu na makampuni yao wamekopa benki wanashindwa kurejesha mikopo hiyo, Vilevile yanashindwa kulipa kodi.

Sasa swali ni hili je?...
1. Mkifirisi mali zao na hamtaki kulipa madeni wanayowadai mtapata wapi kodi kama hizo kwa kiwango kile kile tena baada ya kufilisi?

2. Na je, wafanyakazi watakao achishwa kazi kwenye kampuni mtakazo filisi mali zao watapata wapi kazi tena katika kipindi hiki kigumu.

3. Na pia, jiulize kwa watakao maliza vyuoni na wenyewe watapata wapi tena kazi wakati wenzao waliopo kwenye kazi wanapunguzwa.

4. Na ukianzisha ujasiriamali kabla hujaanza biashara kodi unatakiwa ulipe kwanza, kwa makadirio watakayo kukadiria wao siri-kali.

a) Usilete ushabiki wa kijani jiulize wewe unayefanya kazi kama uko salama?

b) Pengine utasema tuvumilie mambo yatakuwa mazuri , tafakari ujue wengi watakuwa omba omba na uharifu utaongezeka, na uharifu ukiongezeka watu watapandwa na hasira, na wakipandwa na hasira watamgeukia nani?

c) Mfano wewe mmoja ukibahatisha kazi nzuri utawasaidia ndugu zako au zetu wangapi?

Usitumie hasira kujibu!
Mbowe ni miongono mwa wadaiwa wa ile benki ya mnyama mwenye shingo ndefu!
Sasa shida ni kwa wakopaji bila kulipa? Au Mr President?
 
Ni Kweli hata mbadilisha gia za angani Mbowe amefunga pale billicanas
Lissu mwanasheria si mchumi lakini anaisikia harufu ya uchumi kutingishika kwa lugha ya kiuchumi aisee
Tundu Lissu

Kwanza, nawasalimu makamanda wote na wapenda Maendeleo wote. Nawapa somo (Elimu Elimu Elimu).

Ile Benki yenye picha ya ndege imewatangazia wafanyakazi wake kuwa ipo kwenye hali tete, wakae sawa kwa lolote litakalotokea hiyo ni kwa hapa kwetu tu, ila nchini kwao iko vizuri na kwenye nchi nyingine iko vizuri pia kutokana na mifumo mizuri ya huko.

Kumbuka kuna benki nyingine hivi karibuni, ile yenye jina la mnyama mwenye shingo ndefu ilitangazwa kuwa ipo kwenye hali tete, pamoja na hilo kuna Benki nyingine iliyokuwa kila mara inajitangaza kupata faida nayo imepata hasara mwaka huu tutegemee kupata wategemezi wengi sana kwenye familia kuanzia mwaka 2017.

Turudi tena kwenye point moja upende usipende wewe au mimi au wa kijani (rangi ya mboga mboga) mjue tunaenda kwenye hali mbaya sana ya kiuchumi, tunaenda kusoma namba, na Mzee wetu hataki kusikia hiki watu wanachokilalamikia, anaongeza sheria tu,
siri-kali hailipi madeni ya ndani ila inadai kodi tu, kama unadaiwa na Benki kwa kukopa hiyo ni shauri yako.

Na hivi karibuni mmemwona kada maarufu wa kijani (aliyekuwa anasisitiza ujasiriamali) anaidai siri-kali ila hajalipwa, izingatiwe amekopa benki na atafilisiwa muda si mrefu na ataisoma namba kwani mali zake zitapigwa mnada.

Nimetolea mfano mmoja tu kuna wananchi wengi tu mfano wahandisi, wafanyabiashara waliiuzia bidhaa siri-kali au kutengeneza miundo mbinu ya siri-kali hawajalipwa ila wanadaiwa kodi tu na vitisho chungu mbovu na makampuni yao wamekopa benki wanashindwa kurejesha mikopo hiyo, Vilevile yanashindwa kulipa kodi.

Sasa swali ni hili je?...
1. Mkifirisi mali zao na hamtaki kulipa madeni wanayowadai mtapata wapi kodi kama hizo kwa kiwango kile kile tena baada ya kufilisi?

2. Na je, wafanyakazi watakao achishwa kazi kwenye kampuni mtakazo filisi mali zao watapata wapi kazi tena katika kipindi hiki kigumu.

3. Na pia, jiulize kwa watakao maliza vyuoni na wenyewe watapata wapi tena kazi wakati wenzao waliopo kwenye kazi wanapunguzwa.

4. Na ukianzisha ujasiriamali kabla hujaanza biashara kodi unatakiwa ulipe kwanza, kwa makadirio watakayo kukadiria wao siri-kali.

a) Usilete ushabiki wa kijani jiulize wewe unayefanya kazi kama uko salama?

b) Pengine utasema tuvumilie mambo yatakuwa mazuri , tafakari ujue wengi watakuwa omba omba na uharifu utaongezeka, na uharifu ukiongezeka watu watapandwa na hasira, na wakipandwa na hasira watamgeukia nani?

c) Mfano wewe mmoja ukibahatisha kazi nzuri utawasaidia ndugu zako au zetu wangapi?

Usitumie hasira kujibu!
 
Giza nene sana miaka ijayo, kutakuwa na vilio vya kusaga na meno au vilio vya mbwa mdomo juu. Kauli ya Mwinyi ya kwamba nchi inaenda kama gari bovu bado ni very valid na siyo kauli yake ya jana ya kinafiki eti jamaa kaleta tsunami la kupambana na rushwa na ufisadi.

Angeulizwa kuhusu Wabunge kupokea milioni 10, Lugumi, escrow, IPTL, MV ufisadi etc angeishia kung'aa macho.

Baadhi ya maswali hayo hata mimi nimekuwa nikijiuliza na kwakweli sipati majibu.
 
Mambo mazito. Tufanyeje sasa maana hata huyo Mungu tunayemuomba wakati hatujabadilika atatuchoka na wala hatatusikia wala hatatusaidia kabisa
 
Number doesn't.........najua utamalizia.!
Wote niwatanzania tunakaa wote nchi moja
Basi tusubiri tujionee
Tutakuwa kama Ivory cost wakati huo
 
Back
Top Bottom