Tundu Lissu hakujua kuwa wazungu kwa sasa hawaweki ''mayai yote'' katika kapu moja!

Upinzani haukushindwa kumshawishi watu kuandamana, bali serikali ilizuia maandamano. Viongozi wengi wa upinzani waliwekwa ndani, matamko ya serikali juu ya watakaojitokeza kuandamana yalijaa vitisho. Kwa Hali hiyo ni busara ilitumika kuacha kuandamana kuepusha shari na dola.
Sasa hii motto ya CHADEMA inayosema Peoples Power iliishia wapi?
 
Siasa za kimataifa zimebadilika sana tokea kuibuka kwa taifa la China kiuchumi na kutishia uchumi wa muungano wa nchi za Ulaya na Marekani.

Kuibuka kiuchumi kwa nchi ya China kumesababisha mzani wa maamuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani kwa nchi zenye uchumi wa chini na kati kama Tanzania yafanyike kwa uangalifu mkubwa.

Kuibuka kwa China kumewafanya wazungu wa nchi za Ulaya na Marekani waanza kufanya siasa za ''kutofungamana na upande wowote'' ndani ya vyama vya siasa katika nchi hasa za Afrika huku wakitumia muktadha wa kibiashara unaosema, ''usiweke mayai yote kwenye kapu moja''. Hii ina maana kwamba usiwekeze katika eneo moja pekee. Unatakiwa kutawanya uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti ili uwekezaji mmoja ukianguka mwingine utaendelea kukuzalishia.

Wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani kwa sasa wanajua dhana ya ''World Order'' haipo tena.

Wazungu walipomwambia Tundu Lissu wako nyuma yake na wakamsafirisha katika nchi mbali mbali za Ulaya na Marekani kutoa mihadhara inayohusu siasa za Tanzania ili apate uungwaji mkono, alidhani wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake!

Tundu Lissu kwa kutojua siasa za sasa za nchi za Ulaya na Marekani, alianza kutamba huku akiiambia dunia, ''Western world is done with Magufuli regime''! Magufuli regime has been isolated not only in EA and SADC but in all democratic world!

Kwa kuamini wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake, Tundu Lissu akaingia kwenye kampeni nchini akijua wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani watahakikisha utawala wa Rais Magufuli unaangamizwa kwa yeye kuwa Rais au kutokuwa Rais kwa sababu wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani wako nyuma yake.

Siku ya uapisho wa Rais Magufuli ilikuwa ni siku iliyotuma ujumbe kwa Lissu kuwa ''Western World is not done with Magufuli regime''. Mabalozi wote wa nchi za Ulaya na Marekani walihudhuria sherehe za uapisho wa Rais Magufuli kule Dodoma. Na kwa kutaka kuonyesha kuwa walihudhuria, walitoa official statement kuzieleza nchi zao.

Kwa sasa tunaona mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wakianza kufanya kazi na serikali ya Rais Magufuli kwa niaba ya serikali za nchi zao. Juzi tulimuona balozi wa nchi za Ufaransa akitoa pongezi kwa Rais Magufuli na kuahidi ushirikiano wa karibu.

Mabalozi wengine wameanza kutoa pongezi kwa vyama vya siasa vinavyoungana na serikali ya Tanzania ili kuwa sehemu ya serikali katika kuwatumikia wananchi.

Kwa maana nyingine, Kushindwa kwa Tundu Lissu hata kuwashawishi wananchi kuandamana, wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani walijua mayai waliyoweka kwenye kapu la Tundu Lissu yamevunjika yote na hapo hapo wakageukia biashara nyingine ya mayai waliyoweka kwenye kapu la Rais Magufuli.

Wazungu walichofanya ni kumrudisha Tundu Lissu kule ambako walimtoa (Ubelgiji) ili wasije wakapata lawama kama atapatwa na matatizo nchini yatakayowafanya wao kuhojiwa kwa nini walimleta Tanzania!

Kuna baadhi ya watu eti wameaminishwa na wanasubiri serikali ya Tanzania kuwekewa vikwazo na Rais Magufuli kufikiswa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)! Hawa wajinga watasubiri sana!

Yanayompata Tundu Lissu yalimpata pia Maalim Seif mwaka 2015 baada ya kuamini kuwa wazungu wameweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake! Maalim Seif akagomea Uchaguzi wa marudio akitegemea wazungu watakuwa nyuma yake. Baadaye alizunguka duniani akiwaomba wazungu watimize ahadi zao lakini wao wakamwambia hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu Zanzibar kwa sasa kuna amani.

Maalim Seif ametumia uzoefu alioupata mwaka 2015 kutatua tatizo ambalo lilijitokeza tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Wakati akihojiwa na Clouds TV baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif amesema uzoefu waliopata mwaka 2015 umewafunza kuwa huwezi kususia kila kitu kwa sababu kususia huko kuliwaathiri sana kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Wakati akihojiwa na Radio ya Sauti ya Amerika (VOA), Tundu alisema kwa sasa wazungu wanamuambia Tanzania kuna amani lakini yeye anawaambia hakuna amani. Wazungu wanachomwambia kwa sasa Tundu Lissu ndicho kile kile walichokuwa wanamwambia Maalim Seif baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliposusia uchaguzi.

Haishangazi kuona Tundu Lissu anawashambulia sana wale alidhani wako naye ambao wanaungana na serikali ya Tanzania au Serikali ya Mapinduzi, Kwake wanaofanya hivyo wanakuwa wanaua hoja zake kwa wazungu kuwa Tanzania hakuna amani.

Tundu Lissu ajiandae kisaikologia, Ninajua sio muda mrefu CHADEMA wataanza kupokea ruzuku ya serikali itokanayo na kura za wabunge ambazo Tundu Lissu anadai hazitambui! Hata wabunge wa viti maalum waliopitishwa na ''kamati kuu'' wataenda bungeni!

Niliwahi kusema, kwa hulka za Wazungu, Tundu Lissu atakuwa kama mwanasiasa za Venezuela, Juan Guaido. Ukitaka kusoma mada ya Juan Guaido, Gonga link hii;

Kadri siku zinavyoenda, Tundu Lissu atazidi kugombana na wanasiasa wengi anaodhani wanamsaliti bila kujua tatizo ni yeye kudhani kuwa wazungu waliweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake!

Lissu awarded IDU Award for Freedom 2020 - YouTube
 
Tundu Lissu kwa kutojua siasa za sasa za nchi za Ulaya na Marekani, alianza kutamba huku akiiambia dunia, ''Western world is done with Magufuli regime''! Magufuli regime has been isolated not only in EA and SADC but in all democratic world!
Mimi nilisema mahali fulani kuwa lissu hana uwezo mzuri wa kufikiri (nilitumia neno zezeta) nikapigwa ban; kwa kuwa sitaki kupigwa ban tena basi ngoja nisiseme kitu.
 
Uhuru na haki ya mpiga kura hauishii tu kwenye kupiga kura, wacha hoja za kitapeli; lazima na kura ya mpigaji iheshimiwe na pasiwepo makandokando yoyote kwenye zoezi zima la uhesabuji kura, hilo hapa kwetu halipo, kama hukubaliani na hili wewe ni mnafiki wa nafsi yako (refer kura kwenye mabox meusi zote zimewekwa tick wagombea wa CCM).

Composition ya Tume nayo ni tatizo, haiwezekani Mwenyekiti achaguliwe na Rais ambae kimsingi nae ni Mwenyekiti wa CCM, huyu tayari bosi wake anakuwa ni M/kiti wa CCM, hawezi kutimiza majukumu yake ya msingi bila kuwa na viashiria vya upendeleo, matamko mengi aliyotoa Mahera na wenzake yalikuwa yanawa favour CCM na mgombea wao, hili nalo halina mjadala, unless uwe mnafiki.

Kumchanganya Seif na Chadema kwenye maamuzi nalo ni tatizo jingine la uelewa mdogo ulilonalo, Seif yuko ACT, hivyo vikao vya chama chao ndivyo vilivyoamua waende kwenye hiyo serikali, Lissu kugombea urais sio kwasababu ya ubinafsi kama unavyosema, hilo ni takwa la sheria, usilete uongo wako hapa, hivyo suala la ubinafsi wa Lissu ni hoja mfu ya kitoto, au mlitaka Chadema isiweke mgombea?

Bandiko la huyu MsemajiUkweli ni hoja dhaifu za kufikirika na kujiliwaza tu, hazina mantiki yoyote, kusema wazungu wanamuogopa mchina ndio washindwe kuwashughulikia mkifanya ujinga wenu ni ufinyu wa kufikiri, mbona Makonda alishughulikiwa? na misaada mingapi mmenyimwa na wazungu mpaka mnatetemeka mnalazimisha kununua wapinzani waende bungeni mpate ile 1.6 trillion huku Ndugai akiwalinda kwa kuvunja sheria?

Kusifia hili bandiko na huu utawala usiofuata sheria ni ukosefu wa akili, na hicho kinaonekana kwa namna ulivyojenga hoja zako kwa 100% pale juu.

Mantiki ya hoja zako iko katika mkinzano wa kifikra ndani mwako. Pia hoja zako zimegubikwa katika madai ya siku zote ya wanasiasa wa upinzani ya demokrasia, na Tume huru ya Uchaguzi, kwamba kulikuwa na kura bandia kabla ya uchaguzi. Je,
√ kuna ushahidi wowote kuwa katika zoezi la kupiga na kuhesabu kura kulikuwa na udanganyifu? Kama kuna ushahidi wagombea husika watumie Sheria ya Uchaguzi kupata haki yao. Vinginevyo ni utoto kulialia kuibiwa kura;
√ kuna ushahidi wowote kuwa watumishi wa Tume, nchi nzima, ni wafuasi wa chama tawala kiasi cha kufumbia macho hayo matendo ya wizi wa kura (maboksi meusi kama unavyodai)? na
√ ni kweli uteuzi wa M/kiti wa Tume ya Uchaguzi hufanywa na Rais? Rejea mchakato wa uteuzi huo kama una dosari kabla ya kulaumu na kulalamika.

Seif wa ACT-Wazalendo alishiriki kikamilifu katika kampeni za Lissu kwa jinsi ileile. Kwa sababu hiyo kauli ya kususia matokeo ya uchaguzi na hivyo vyama, ilikuwa ya pamoja. Iweje mmoja wao awe kigeugeu? Ni yale yale ya UWAKA kujitokeza kwa staili nyingine. Tatizo jilo linaibua swali kuhusu UADILIFU wa wanasiasa wa upinzani.

Lissu kugombea Urais hakuna ubishi ni takwa la kisheria. Hoja yangu ni mazingira yaliyomwezesha kuwa mgombea kupitia CHADEMA. Kama wewe denooJ humo ndani ya hicho chama unalijua vizuri.

Hoja zilizomo kwenye bandiko kuu bado ni za msingi, iwapo viongozi wa CHADEMA wana nia ya dhati ya kushika Dola. Okotaokota ya wagombea Urais itaendelea kukigharimu chama.
 
Nilitarajia uandike hivyo hivyo kuanzia mwanzo mpaka mwisho ila mwisho ukaegemea upande mahabati.
Mkuu kwanini Uchaguzi wa Rais aupingwi mahakamani?
Mkuu,kwanini public media zilikua biased kwa kutangaza kampeini za CCM tu live ila kampeini za vyama vingine kama CHADEMA,CUF,ACT-Wazalendo hawakupewa haki au muda kufanya hivyo?
Mkuu ,kwanini mawakala wa vyama vya Upinzani walikua wanasumbuliwa na kutolewa nje ya vyumba vya kupigia kura?

Matokeo ya uchaguzi wa Rais hayapingwi mahakamani kwa takwa la Katiba ya JMT (1977).

Kwa nini vyombo vya habari havikuonesha mbhashara kampeni za vyama vya upinzani waulizwe wahusika.

Mawakala wa vyama vya upinzani kusumbiliwa na kutolewa nje pata ukweli kutoka kwa baadhi yao hao
 
Lisu bado ni Lulu kwa wazungu katika kufanikisha malengo yao. Wenzetu hawajali iwe ni CCM au chama kingine ilimradi wanapata wanachokihitaji hawana matatizo.

Ili wafikie hilo lazima wawe na mwali wa kujinadi naye ili mke wa kwanza awe na heshima na kupunguza makali yake. Usiponielewa hapo, nenda kwa mganga wa kienyeji.
Kwa hiyo unaamini waganga wa kienyeji wanatatua matatizo ya kifikra!

Hata Juan Guaido alikuwa lulu kwa wazungu lakini leo hii wamemtupa na kutafuta mwingine!
 
Sasa hii motto ya CHADEMA inayosema Peoples Power iliishia wapi?

Mheshimiwa nakushauri uende taratibu (take it easy) kwenye haya mambo. Usijeonekana wewe ndiye unaendekeza “school boy politics”.

Mheshimiwa Rais keshatutangazia “uchaguzi umekwisha” sasa tuchape kazi. CCM imepata ushindi wa kishindo na CHADEMA wameangukia pua. Bila shaka hiyo maana yake ni kwamba wananchi wanaikubali sana CCM ya Magufuli na wamewakataa CHADEMA na Lissu wao. Right?

Lissu kesharejea Ubelgiji baada ya kushindwa. Wapinzani wengine ama wameunga mkono juhudi au wametulia kuendelea na mistakabali yao. Kuna pia akina Mbatia, Zitto, Queen, Mrema, Rungwe, Cheyo, nk. Mchezo umeisha.

Sasa unapoleta bandiko la aina hii inaashiria dalili za kukosa kujiamini. Hivyo inabidi uendelee kumnanga mshindani wako uliyembwaga chini tayari ili upate maoni ya kukuinua “confidence” kwamba wewe ni “mshindi” kweli na mshindani wako “umemshinda vibaya sana” na “ni mtu wa ovyo sana”! Just like expending precious calories in a frenzy to flog a dead horse! To what end?

Take it easy boss. CHADEMA is no more and Tundu Lissu out! Uchaguzi umekwisha!
 
China haina uwezo wa kuwafanya wazungu waweke au watoe support kwenye vyama vya upinzani Tanzania na Afrika nzima. Ukitaka support ya wazungu, fanya kampeni na lobbying Washington DC siyo Brussels. Wazungu na nchi za magharibi, EU wanafanya wanachoambiwa na wamarekani.
 
Tatizo la hao jamaa uliowataja wanatanguliza emotion than critical reasoning!

Yaani matamanio yao wanadhani ndio matokeo!

Ukweli una tabia ya kuchelewa kumfikia mlengwa lakini lazima utamfikia kwa njia yoyote! Ukweli umewafikia na sasa wameamza kupotea hapa Jamiiforums! Najua watakuwa wamebadilisha ID na kuja na ID nyingine ili kuficha aibu!

Kuna mwingine nakumbuka nilisoma thread yake hapa akisema Rais Magufuli akiwa Rais wa Tanzania anahama nchi!

Walichokuwa wanakifanya hawa jamaa kinaitwa schoolboy politics!
Ni mpuuzi mwingine anajiita Prof Koboko na uzi ni huu
 
Kwa hiyo unaamini waganga wa kienyeji wanatatua matatizo ya kifikra!

Hata Juan Guaido alikuwa lulu kwa wazungu lakini leo hii wamemtupa na kutafuta mwingine!

Kesho yetu hatuijui, lakini kwa Leo Lisu bado ni Lulu ya Wazungu. Ya Juan Guaidaro muachie Juan Guaidaro.
 
Ila matatizo ya kisiasa kwa Tanzania ayajafia ata robo ya nchi Kama Rwanda na all East and Central Africa.Tundu Lissu atulie tuu.
 
Mzee Warioba kwanza kukinai ukiukwaji wa taratibu na katiba pia Mzee Msekwa Butiku alianza Zamani. Endeleeni kusifia mambo ya hovyo
 
Back
Top Bottom