Kila swali linahitaji jibu lake, plse!
Niwakumbushe Historia.
Mwaka 1979 katika Vita ya Uganda, Gadaffi aliisaidia Uganda kutushambulia kwa kuipatia vifaa. Nyerere akamchukia na wote tukaungana na Nyerere katika hilo.
Mwaka 2009 kuelekea miaka 10 bila mwalimu, mama Maria Nyerere akatuambia kule butiama kwamba Nyerere alimuomba Gadaffi fedha za kujengea shule mwaka 1996, Gadaffi akaleta za kujengea Msikiti uliopo butiama hadi leo.
Hii inaonesha katika mambo ya kukubaliana kupingana na adui tunaungana. Kama tunaaminiana tutalingana.
Unataka majibu matatu?
Rudia jibu hilo mara tatu uone kama halifai
Mtahaha sana na muungano wa UKAWA !! Mliita wenzenu wapenda maandamano mbona nyie tanzania one sijui kwanza mnaandaa ??
Rais wenu JK alisema 'sizitaki kura zenu' wafanyakazi mbona aliiruka kimanga kauli yake ???
Mlipoona CHADEMA na CUF wameenda Jangwani na mkasema hamna haja ya kwenda huko, mbona mlisomba mawaziri,non mizigo mkaenda pia ??
Sasa vichekesho jana nimemsikia mwenyekiti wa vyama vya siasa Peter Mziray akiponda UKAWwA hahahaha mtahahah sana mwaka huu
Mnatuonyesha jeshi kututishia sisi raia wa kawaida ??
Ngoja muungano uwatoe majasho
Tuliaminishwa na of course mimi niliamini kwa dhati kuwa CUF ni CCM B! Aliyenifanya niamini hivyo si mwingine ni mwanasiasa machachari na "mwanasheria nguli" Tundu Lissu!
Kwa kudhihirisha hilo CHADEMA ilikataa kabisa kata kata kuungana na CUF ili kuunda Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni!
Hata hivyo, hivi karibuni CUF kimeshikamana na CHADEMA wakiiponda CCM eti kupanga maandamano na mikutano ya hadhara kwa pamoja! Kweli hii ni ajabu sana!
Hebu tujiulize maswali yafuatayo:
1. Je, tuhuma za u-CCM B za CUF zilikuwa za kweli?
2. Kama zilikuwa za kweli, Je, kwa sasa CUF imeshakuwa "mtoto mzuri" na hatarudia tena utukutu wake?
3. Kama zilikuwa si za kweli, kuna sababu yoyote ya kuendelea kuiamini CDM?
4.......
Karibuni kwa mjadala, matusi, kejeli, nk si mahala pake, hata kama hatutakubaliana kila kitu, tuheshimiane!
Jibu moja kwa maswali yote.... CUF waliungana na ninyi walipowaamini, sasa Imani imetoweka.
Wagombanao ndio wapatanao, ushirika wa CHADEMA , NCCR na CUF hautaondolewa kwa propaganda nyepesi hizo, CCM imenyanyasa sana watanzania , huo mimi nauna ni kama mpango wa Mungu, mmetiwa upofu CCM, mnafikiri wingi wenu siku zote utawasaidia.
Msipo jitafakari kwa mikakati hii ya upinzani itawapa milage kubwa mno katika siasa za hapa nchini
Hivi Jussa sio miongoni mwa wana-UKAWA?
Orait, tuambie mkuu kama CUF imeacha kuwa CCM B! Msichukuliwe na upepo halafu baadaye muanze kutafutana hapa!
Kwani kupima kuwa chama fulani ni CCM B au la ni kutoka au kutotoka Bungeni?