Tundu Lissu: 'Bunge la Bajeti' is another silly season!

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
Lissu: This is another silly season!

Nitajaribu kuandika kadri ya alivyosema. Nitamnukuu kadri ya alivyosema, lakini ni wazi sitaweza kuaandika yote (ya muhimu) aliyoyasema na kwa namna ile ile aliyoisema, maana nilikuwa nikitype kwa wakati ule ule aliokuwa akizungumza. Ni moja ya hansard nzuri kuifutilia, kuipata na kuisoma.

Of-course baada ya mchango wake bungeni pametifuka kweli kweli. Alifuata Mwigulu Nchemba, looh! Badala ya kuzungumzia bajeti in details akaanza kumsakama Lissu, wapinzani na bajeti yao. Akatupa hata kitabu cha bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni ilyosomwa leo na Ndugu Kabwe Zitto Zuberi.

Jamaa kama alivyokurupuka kujibu tamko la Zitto juu ya kufilisika hazina kama ambavyo taarifa za Benki Kuu (BoT) kwenye mtandao zilikuwa zinaonekana kuonesha, ndivyo ilivyokuwa leo. Anatanguliza mbele sana kujisema juu ya uchumi grade gani vile...na kuwa aliwahi kufanya kazi BoT. Tumsaidie. Sifa za uwezo wa mtu, kitaaluma, huwa hazisemwi mdomoni. Zinapaswa kuonekana. People have to feel it, have to ssen it...it has to be felt, heard not to be said with merely words.

Mmoja wa wafanyakazi wenzangu hapa, dereva, ananiambia hapa kuwa jamaa pressure ilikuwa juu kutokana na mchango wa Lissu na Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani ilivyoichana chane ile ya serikali. He is another completely affected with CHADEMAphobia (or CHADEMAhegemony) akimfuatia kwa ukaribu sana Stephen Masatu Wassira.

Baada ya hapo pia alifuatia John Komba, oohpps. I have nothing to quote from him. Angalizo kwao; wasipokuwa makini watajikuta katika hali iliyowasibu mwaka jana wakati wa mjadala wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, ambapo baada ya KUTIFULIWA kwa hoja kabambe, wakaacha kujadili hoja mbele yao, wakaanza kumjadili mtu (Lissu), watu (CHADEMA). Complete out of point, out of touch. Wakaliwa kwenye mahakama kubwa ya watu, nje ya bunge.

Anyway turudi kwenye 'headline'. Ndugu Tundu Lissu alikuwa mmoja wa wachangiaji wa mjadala wa bajeti leo bungeni. Session ya jioni hii. Katifua. Amesema wazi wazi kuwa wakati wa bunge la bajeti ni majira mengine kwa ajili ya masuala ya kipuuzi. Ameita it is silly season. Na hivyo Mkutano huu wa bajeti it is another silly season kwa sababu ni wakati wa kujadili mambo ambayo hayatekelezeki.


Wabunge wengi (ofcoz mnawajua) wanasimama wanasema wanaunga mkono bajeti mia kwa mia kisha wakianza kuchangia wanapinga kila kitu walichosema awali wanaunga mkono. It is another silly season.

It is another silly season kwa sababu serikali inaleta vitu bungeni na wabunge wanajadili na wengine wanaunga mkono wakati inajulikana wazi kuwa vitu hivyo havitekelezwi.

Amesema kujadili vitu ambavyo havitekelezwi ni kujidanganya wenyewe, kudanganya watoto wetu na kuidanganya nchi hii. Ni aibu kwa kwetu kwa wabunge wote (bunge zima).

Ametolea mfano wa namna serikali ilivyoahidi katika mkutano wa bunge la bajeti uliopita kuwa wataweka trilioni 8.6 kila mwaka kwa ajili ya bajeti ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Anasema kwa sababu ya kuwa ni silly season, wabunge waliitwa Saint Gasper na Rais, wakalishwa, wakanyweshwa juu ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Lakini katika bajeti ya mwaka jana mpango huo ukatengewa trilioni 4. (something), walipohoji wakajibiwa kuwa ni mwaka wa mpito lakini itaanza rasmi mwaka huu.

Lakini mwaka huu tena mpango huo umetengewa trilioni 4.5 badala ya trilioni 8.6 kama ilivyoahidiwa. “They knew they were lying, we knew they were lying, we should be ashamed to this government, ashamed to this budget…ashamed to these Members of Parliament kwa sababu ndiyo wanaopitisha bajeti hii…(hapa Lukuvi akaingilia juu ya matumizi ya lugha za kuudhi kwa kutumia kanuni ya 64 kuwa inakataza matumizi ya lugha za matumizi na Mwenyekiti Mabumba akasisitiza).

“Mara kadhaa wamekuja hapa na kuahidi kuwa wataziba mianya ya ukwepaji kodi, watapunguza misamaha ya kodi. Lugha hizi zimekuwa za siku nyingi sana. Viongozi wa dini wamefanya utafiti na kuja na ripoti waliyoiita The 1 billlion Dollar Question…hii ni disaster ya CCM and nobody else. Mwaka 1998 Kigoda waziri wa madini, sheria ya madini ya mwaka 1998.


“Mwaka 1998 katika bunge hili wakati huo Waziri wa Nishati na Madini alikuwa Kigoda, alisema kuwa sekta ya madini itakuwa ikichangia asilimia 52 ya revenue yote inayotokana na madini. Lakini mpaka sasa tunapata on average dola milioni 100 tena katika utafiti huu wa viongozi wa dini wanasema asilimia 65 zinatokana na kodi za wafanyakazi.

“Na sasa tumepata miungu wapya wanaitwa wawekezaji…our new gods, the untouchable, kila ukigusa aah wawekezaji, ukigusa aah wawekezaji…what have they done for us? Tunaambiwa kuwa eskta ya madini ndiyo inayotoa more foreign exchange than any other…hizo fedha hizo ziko wapi…

 
Kweli wanaojua nchi yetu inavyoliwa na ulongo ulongo tunaoambiwa na watawala lazima wawe na hasira kama Mh. Lissu alivyokuwa bungeni leo wakati anachangia jioni
 
Nimefuatilia mjadala wa wizara ya fedha kuhusu bajeti kuu. Ninajiuliza hivi kama serikali ilikusanya mapato kwa asilimia 106, Wafadhili na mikopo ni 80% kwa juu juu ni kwamba mapungufu kwenye bajeti iliyopita ilitakiwa roughly 14% cha kushangaza wizara na idara za serikali zimepewa kiduchu kwenye maendeleo.

Naambiwa ardhi walipangiwa bil 20 wameishia kupewa bil 3 halafu tunategemea viwanja. Kama serikali inajiamulia inavyotaka ridhaa ya bunge juu ya bajeti ni ya nini? Na bado mwaka huu hela zinaelekezwa kulipa madeni. Kuna EPA nyingine imezaliwa bado hatujashtuka huko hazina lazima mfuko wetu umetoboka.
 
Hayo ndo maneno ambayo Mh. lissu ameiambia serikali na wabunge wa ccm.huyu jamaa ana uchungu sana na hiyo bajeti yao iliyojaa uongo kwa wananchi wa Tz.
Hahahahahahahaaa.....chezea Lissu wewe.
 
Anapiga ikulu , shame on you du! Nouma kweli Huyu lissu balaa
 
weken habari nzima,mnaweka habari kana kwambo wote tunaangalie bunge bana!achen hizo.ghaaaa!
 
Kweli wanaojua nchi yetu inavyoliwa na ulongo ulongo tunaoambiwa na watawala lazima wawe na hasira kama Mh. Lissu alivyokuwa bungeni leo wakati anachangia jioni

Bora slaa aingie ikulu kuliko lissu kuingia bungeni....
 
Lukuvi kaona ni lugha ya kuudh!!!i; kweli ukweli mchungu jamani, Mwigulu anasema Lissu ni Muigizaji, 2015 sio mbali.
 
Tundu lisu katoka kuchangia hoja muda si mrefu akaanza kuiponda na kusema serikali yetu ni silly government,chama ni silly na akafika mbali kuomba wananchi wasitishe muda wa chama kuongoza tena hii nchi,Mheshimiwa lukuvi akasimama kuomba mwenyekiti amzuie Tundu lisu apunguze maneno yake makali maana yanakera,big up tundu lisu

Saa hizi anaongea mbunge wa CCM kasema wabunge wengine ni wasanii (akimponda Tundu lisu)mwenyekiti kasimama kasema afute kauri yake na akaifuta naye kaponda kuwa kuna wanasheria waliosema uchawi,kuna waenda madisco humu ndani(nahisi mbowe anamponda),Patachimbika leo



Nawakilisha!
 
hawa watu wakutuonjesha asali siwapendi!si ulete habari kamili,mnafukuzwa?
 
Tujuzeni rasmi jembe letu amechangia yapi jamani wengine hatujashuhudia tupeni utamu wote basi.
 
kuweni fair jamani, sio mnaweka vipande vya habari kama vile wote tuna access ya kusikiliza bunge
 
Kuna huyu jamaa anaitwa Mwigulu, nadhani anapaswa kuombewa, he is just there!!!
 
Back
Top Bottom