Tundu Lissu apambana dakika 125

Tundu Lissu apambana dakika 125

Ya tundu Lissu yamekushinda kujibu? na umeuona ukweli na alikinyanyua kitabu juu akasema yako humu na akataja ananukuu kutoka kitabu kipi, jee unakikumbuka "title" yake?

Wewe tuache wataalamu washeria tudadavue mambo humuwezi lissu hata mjikusanye Lumumba wote
 
Wewe tuache wataalamu washeria tudadavue mambo humuwezi lissu hata mjikusanye Lumumba wote

Kwa hakika hatumuwezi hata kiduchu, mtu asiyejuwa kutofautisha "state of emergency" na "disaster", huyo tutamuweza wapi?
 
Hii ndo michango ya great thinker! Tufikie muda watz tuongee ukweli kuliko kushabikia tu mambo ambayo yanatufanya kuwa low thinker. Daaaah nchi yangu tz.
 
Alipowapasha kuhusu mapungufu ya Nyerere live bungeni mbona hamkumshangilia?

Wengi wenu mkasema "kamtukana" Nyerere?

Hapo sasa!
 
Tundu Lissu juzi alitumia dakika 125 kupinga muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vipengele.

Lissu, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alikuwa na kazi ngumu ya kupambana na Naibu Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu na baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakijaribu kusaidia kupitishwa kwa muswada ambao hata hivyo ulikwama kutokana na idadi ndogo ya wabunge waliokuwa ukumbini.

amoja na uwingi huo wa wapinzani wake, Lissu hakuonekana kukata tamaa wala kuingia hasira zaidi ya kumwambia Mwanasheria Mkuu, George Masaju, “stoop!” kutokana na kuchukua jukumu la kulishauri Bunge, kitendo ambacho Lissu alisema kinamkera kwa kuwa AG ni mshauri wa Serikali na si Bunge.

Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na kaimu kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, alipinga vifungu vyote 44 vya muswada huo, akisema kuwa unamuondolea mamlaka Rais ya kutangaza hali ya hatari, sheria mpya kudurufishwa bila ya kuwa na upya wowote na kwamba inavunja Katiba ya nchi.

Mvutano huo ulianza saa 12:00 jioni, lakini ulishika kasi kuanzia saa 1:25 hadi 3:25 usiku baada ya Bunge zima kukaa kama kamati kwa ajili ya kupitisha kufungu kimoja kimoja cha muswada huo, huku Lissu akisimama mara 19 kupinga kupitishwa kwa vifungu hivyo, akieleza kasoro zake na kushauri jinsi vinavyotakiwa kuwekwa, huku vingine akitaka vifutwe kabisa.

Kutokana na kuibuka kwa ubishani mkali na mrefu kati ya mbunge huyo, Masaju, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Jenister Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia na kusababisha muda kuyoyoma jambo lililomfanya mwenyekiti wa Bunge, Musa Azzan Zungu kulazimika kulihoji Bunge ili kupitisha vifungu husika.

Hata baadhi ya wabunge waliosimama kupinga hoja za Lissu, akiwamo mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, Henry Shekifu (Lushoto, CCM) na kutoa ufafanuzi wa kisheria, hawakuweza kuzipangua hoja za mbunge huyo wa Singida Mashariki.

Wakati Lissu akianza kutoa ufafanuzi wa vifungu hivyo, mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali naye alikuwa ama akiunga mkono hoja za Lissu au kuja na hoja zake za kupinga muswada huo.

Hata hivyo, mbunge huyo baadaye alikata tamaa na kusema kuwa hana sababu ya kupoteza nguvu zake kutoa maoni ya msingi, mwisho wa siku yanapuuzwa na Serikali ambayo ilikataa kila pendekezo la wabunge hao.

“Nashangaa Mkosamali unakata tamaa,” alisema Lissu baada ya mbunge huyo kusema hawezi kuendelea kutoa hoja zaidi za kupinga muswada huo.

Wakati Mhagama akieleza kuwa sheria hiyo itasaidia wanaokumbwa na maafa na kukosa msaada, kutofautisha maafa na hatari ambazo kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Kudhibiti Maafa ya Mwaka 1990, zinatakiwa kushughulikiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Lissu alisema muswada huo hauna jipya.

Lissu ni hazina ya taifa
 
Nilimsifu sana pale aliposema ukweli kuhusu Nyerere na alipotumia kitabu kilichoandika na Dr. Ghassan na msaidizi Mohamed Said BMK kuonesha uovu wa Nyerere, mkasema kamtukana, umesahau? au ulikuwa bado hujaijuwa JF?

Kama ulikuwa bado kuijua JF jaribu kutumia search feature ya JF utazipata hizo habari.

Kwahiyo wewe sifa pekee unazotoa kwake ni pale anaposema ukweli kuhusu Nyerere pekee ?

Mbona una diverge hoja ya msingi,hoja ni kwamba Tundu lissu alitumia professional yake vizuri na kupambana vilivyo kuupinga mswaada wa kipuuzi uliowasilishwa bungeni na watu wasioweza kufikiri vizuri.Jibu hoja,hii ndiyo hoja ya msingi.
 
Huyo jamaa ni moja ya lulu tulionayo kama taifa kwenye tasnia nzima ya sheria!

majadiliano yale, hakika nilifurahishwa sana tena sana sana na wabunge wa upande wa pili kwa misumali waliyo jiandaa nayo dhidi ya walioleta Mswada ule na watetezi mbumbumbu ambao ulionekana hapakuwa na sababu ya kutungwa kwa sheria mpya kwani sheria tayali ipo wangefanya marekebisho kidogo sana katika sheria hiyo ya miaka ya 1990!

Good work guys, keep it up UKAWA!
 
Kwahiyo wewe sifa pekee unazotoa kwake ni pale anaposema ukweli kuhusu Nyerere pekee ?

Mbona una diverge hoja ya msingi,hoja ni kwamba Tundu lissu alitumia professional yake vizuri na kupambana vilivyo kuupinga mswaada wa kipuuzi uliowasilishwa bungeni na watu wasioweza kufikiri vizuri.Jibu hoja,hii ndiyo hoja ya msingi.

Rudia kunisoma nimeandika hivi:

Tundu Lissu juzi nilimsikiliza kidogo nikaona kichefu-chefu kwa ujinga wake aliokuwa anaudhihirisha nikaacha kumsikiliza.

Alikuwa amma hajui hata kutofautisha "State of Emergency" na "Disaster" au alikuwa anafanya makusudi kupotosha ili atimize mada yake ya kupinga tu hata pasipopingika.

Akanichafua roho na jisauti la kuiga wachungaji wa viwanja vya Jangwani, nikamuona ni punguani mwengine anahororoja na kubwabwaja bila mpango, nikasepa.
 
Mnyaturu a k a mnyampaa mkuu!

Mwigulu Nchemba ndio mnyaturu kaka, amini maneno yangu, hakunaga mnyaturu mjanja na hakunaga mnyiramba machepele ya aina ya Mwigulu, upuuzipuuzi huu unaouona wa mwigulu ni wa kinyaturu na kiukweli ana quality zote za kinyaturu.

Wazazi wa tundu ni wanyiramba, walikita kambi pale mahambe wakitoka ama kwenda kuuza karanga saranda (hakuna wa kubisha)
 
Last edited by a moderator:
Kuliko lisu awe mbunge nibora mninyime urais hahaaa wataisoma najivuniaga kumsikiliza huyu jembe Ila nae akihama chadema cimfuat ng'oooo
 
kwanza nakupongeza sana muheshimiwa lisu kwa uwelewa wako wa sheria umeweza kumkalisha Ag chini yani mwanasheria mkuu waserikali ameonyesha udhaifu mkubwa sana kana kwamba bado hajaiva kisheria kwa maana hoja alizozitoa zote zilikuwa mbovu na hazikuwa na tija kwa taifa.
 
Back
Top Bottom