Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

Hakuna haja ya kumlaumu Lissu hata kidogo!

Wa kulaani ni ccm mpaka kiama chao kije na nafikiri haiko mbali hata kidogo!

Eti miaka 50 ya Uhuru! Uhuru ipi????

Na hata wale wanainchi wa Singida Mashariki ningeomba tu wawe waelewa na wajuwe nani kashikilia mpini wa sime!
 
sasa Lissu kazi yake ni kuwakilisha hoja za wananchi bungeni au ni kufadhili jimbo?kama wakisema hajawahi kusema chochote juu ya jimbo lake bungeni ni haki yao lakini hoja ya maendeleo Lissu hawezi kutoa pesa mfukoni mwake kwenda kuleta maendeleo unless afanye ubunifu namna ya kupata pesa kwa ajili ya kutekeleza baadhi ya ahadi.
 
Hoja ya mleta sred ni ya ukweli na lissu tushamwambia coz nipo jimbon kwake.....asante mkuu kwa kukumbushia napia kamanda ni memba humu jamvini atausoma huu uzi.
 
Hii haiwezi kuhalalisha kutotimiza ahadi ya yale CDM walioahidi wananchi. Kutekeleze kile ulichoahidi ni moja ya nyenzo muhimu kujiletea kuaminiwa na kuheshimika mbele ya wapiga kura na jamii kwa ujumla.

Kamwe tusiahidi tusiyoweza kutekeleza, vinginevyo hatutatofautishwa na yale tuyapingayo (ahadi hewa).
Kwani kazi ya mbunge ni nini? Nikuwakilisha wananchi na siyo kufadhili . Kwani CDM ndio wenye serikali? Kwani lissu amepiga kelele kwa serikali Mara ngapi? Na hasikilizwi kwanza hao wananchi wanatakiwa wasiichague ccm ili tuone Kama CDM kupitia lissu itashindwa kutekeleza hizo ahadi
 
Hoja ya mleta sred ni ya ukweli na lissu tushamwambia coz nipo jimbon kwake.....asante mkuu kwa kukumbushia napia kamanda ni memba humu jamvini atausoma huu uzi.

Kwamba Lissu aliahidi kujenga visima ina maana gani? achukue jembe achimbe au achukue fedha zake zigharimie uchimbaji visima? Au una maana ya kuisimamia serikali ili ijenge visima?Wachangiaji wamekumbusha wajibu wa mbunge, huu wa kujenga visima ukoje? Tukubali kwamba aliahidi na akashindwa kujenga, hivi kama angekuwa hajaahidi hamna lolote ambalo mnaona yeye kama mbunge ana deni kwenu?

Hata kama ameshindwa hilo kama ilivyosemwa lakini mbona kwa upande mwingine amefanya mengi hasa suala la kuiwajibisha serikali kwa kutumia vikao vya bunge?
 
Kwani kazi ya mbunge ni nini? Nikuwakilisha wananchi na siyo kufadhili . Kwani CDM ndio wenye serikali? Kwani lissu amepiga kelele kwa serikali Mara ngapi? Na hasikilizwi kwanza hao wananchi wanatakiwa wasiichague ccm ili tuone Kama CDM kupitia lissu itashindwa kutekeleza hizo ahadi
Mkuu unajua tatizo la Watanzania wengi ni wepesi sana wa kulaumu mambo bila kushirikisha ubongo hata kidogo katika kile tunacholalamikia,wengi tunashindwa kuelewa kua mbunge ni muwakilishi wa wananchi na si mtekelezaji mkuu,sasa wabunge waanze kutoa hela zao mifukoni kwa ajili ya maendeleo ya majimbo yao,je serikali inayokusanya kodi zetu ifanye nini na hizo kodi zetu?huku ni kutokua ni fikra na tutabaki kua taifa la walalamikaji tu maana wengi wetu tunashindwa kushirikisha ubongo katika kufikiri!
 
Mm! hii hoja imenigusa sana. Katika hili naomba mbunge wetu alichukulie kwa uzito stahili. Ni kweli serikali ndiyo inatakiwa kuchimba visima. lkni hofu yangu ni kwamba serikali ya magamba inaweza kukwamisha ili kumkwamisha Lissu. Hivyo naomba mbunge wetu ajaribu anather way round kwa ajili ya kutimiza ahadi zake ikiwamo na kutumia fedha za mfuko wa jimbo.
 
Hoja yako nitaijibu kwa pande mbili ya kwanza ni kukujibu wewe mwenyewe binafsi na wote wanaotarajia kuwa ni kazi ya mbunge kuchimba visima, barabara, kujenga barabara, kujenga shuke, kuleta maji n,k.

Ibara ya 63 (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

Hivyo basi ni vyema tutakatambua kuw anchi yetu inaendeshwa na mihimili mitatu ya Dola yaani SERIKALI yenye madaraka ya kukusanya kodi na kutumia raslimali ikiwemo madini, misitu, wanyama pori , mbuga za wanyama n.k zote za nchi kuwaletea maendeleo wananchi wa nchi hii. MAHAKAMA yenye madaraka ya kutafsiri sheria na BUNGE lenye madaraka ya kuisimamia Serikali kuhakikisha kwa niaba ya wananchi kuwa kodi, misaada, mikopo na raslimali zetu vinatumiwa vizuri ili kuwaletea watanzania wote maendeleo.

Hivyo mwenye kazi ya kuwachimbia wananchi visima, kuwajengea barabara, shule, kuwapatia maji, afya n,k. ni serikali na sio Bunge wala wabunge. Kwa muda mrefu sasa nimetafuta pasipo mafanikio mahali popote au nyaraka inayoeleza ni jukumu la mbunge kuchimba visima, barabara, kujenga barabara, kujenga shuke, kuleta maji n,k. pia nimeomba mara kadhaa wanajf wanionyeshe nyaraka ya aina hiyo pasipo mafanikio.

Serikali hufanya kazi zake kupitia mawaziri wanaoongoza wizara mbali mbali. Hivyo ili wabunge waweze kuisimamia Serikali hutakiwa kutumia Ibara ya 63 (3) ya Katiba Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bungelaweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

Je mbunge anawezaje kuisimamia Serikali ni kwa kupitia kuwahoji mawaziri wa Serikali maswali bungeni na katika kamati mbali mbali za bunge kama ilivyofanyika katika kikao cha saba cha Bunge kilichomalizika jana tar 23 Aprili 2012.

Hivyo kitendo chote chote cha Mhe Tundu Lissu au mbunbge mwingine yeyote mwenye kutaka kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa na vifungu vya Katiba hapo juu atajizuia kuwaomba mawaziri wa Serikali anayopaswa kuisimamia maombi yoyote kwa ajili ya jimbo lake. Na ndio wanavyofanya wabunge wengi wa upinzani. Swali la kujiuiliza hapa ni Je Mhe Tundu Lissu na wabunge wenzeke wa CDM wanatimiza wajibu wao kikatiba yaani kuisimamia na kuishauri Serikali? Nitaomba jibu kutoka kwako.

Je ni kwanini Tanzania ni nchi maskini licha ya kuwa na raslimali lukuki? Ni kutokana na chama cha CCM ambacho kimekuwa madarakani toka nchi hii ipata uhuru kufanikiwa kuwapumbaza watanzania wakiwemo wasomi eti ni jukumu la mbunge kuwaleta wananchi wa jimbo lake maendeleo kama vile kuwachimbia visima, kuwajengea barabara, shule kuwapatia maji n.k. Baada ya watanzania walio wengi kupumbazika, wabunge ili wachaguiliwe tena na wananchi katika majimbo watakayo wakalzimika kuzungumza zaidi mambo ya kijimbo na kuacha kuzungumza mambo ya kitaifa ikiwemo kuwabana mawaziri wa Serikali kisawasawa kuhusu utendaji wao. Kwa hali hiyo CCM ikafanikiwa kuiondolea Serikali zake usimamizi kutoka Bunge ambalo ndilo hutakiwa kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi.

Matokeo ni kushamiri kwa rushwa, ubadhirifu na ufisadi.

Tunatokaje hapo tulipo ni kwa watanzania kuelimishana wenyewe katika majimbo ili tuondoe ubinafsi tuliopandikiziwa na CCM wa kuthamini zaidi majimbo tutokayo badala ya kuthamini nchi yaani Tanzania na kuwaruhusu wawakilkishi wetu kufanya kazi ya kuisimamia Serikali bila ya kuingiza upendeleo kwa jimbo atokalo. Kwa maneno mengine kama tunataka kuondokana na umaskini watanzania katika majimbo mbali mbali tushindane kupeleka bungeni watu wenye uwezo mkubwa wa kuibana Serikali badala ya kutetea majimbo watokayo.

Jibu la Pili ni kwa CDM ili CHADEMA kuweze kushinda majimbo katika mazingira ya siasa za ghiliba zilizoasisiwa na CCM ililazimika kutumia ahadi ili wananchi wachague wagombea wao. Nashauri CDM ianze mara moja kutoa elimu kubwa sana ya uraia ili kuwaelimisha watanzania yale niliyoyataja hapo juu la sivyo watanzania wale wale na mawazo na yale yale waliowahukumu wagombea wa CCM mwaka 2010 watahukumu wabunge wa CDM 2015 kama walivyofanya kwa 2010 kwa kutokujua namna bora ya kuwapima wabunge wazuri kwa taifa na nchi.
 
Kama ni kweli kuwa kuna ahadi alitoa, anatakiwa afanye juu chini azikamilishe. Na kwa wabunge wa chama kama Chadema naamini wakiwa wazi juu ya mahitaji kama ya visima katika majimbo yao, watapata usaidizi wa hali na mali kutoka kwa wapenda maendeleo ambao ni wengi sana.

suala ni kuwa wazi. juzi hapa mwanza, wenje aliitisha harambee ya kuchangia miradi ya maendeleo jimboni kwake. takribani tsh. 50milion zilichangwa na wananchi. hivyo naamini hata lissu akiandaa mpango kama huo visima vitatengenezwa.

kitu kingine anachotakiwa kukifanya, ni kurudi kwa wananchi kuwajulisha, wapi amefikia katika kutekeleza ahadi zake, wapi amekwama na wananchi wampe ushirikiano gani katika kukamilisha ahadi zake.
 
Hao wananchi wa huko kwa Lissu mbona vilaza sana, walimchagua kama Mbunge au Mfadhili?? Kama mbunge tumesikia akitoa hoja kibao bungeni kutimiza wajibu wake lakini kama walimchagua awe mfadhili wamebugi wangemchagua Manji awe mbunge/mfadhili wao. Jukumu la kuchimba visima ni la serikali, mbunge anasimamia utekelezaji kupitia mfuko wa jimbo au halmashauri. Cha kushangaza wanamlaumu Lissu halafu wanasifia Mwigulu Nchemba...

hongera kwa maoni yako kazi ya mbunge ni kusimamia siyo ufaghili .
 
Naomba uongozi wa Chadema walifanyie kazi swala hili, na hizi ahadi zitimizwe sisi tukiwa kama wadau tusingependa kuona ahadi za chama hazitekelezwi bado tunasafari ndefu za kulikomboa taifa hili na kuanza kwa kushindwa kutekeleza ahadi kama hizi kitakichafua chama chetu.

Naomba sana kama hili litakuwa zito kwa chama naomba ifanyike harambee ya visima vya maji nchi nzima, tununue kabisa gari letu liwe linashughulika na kuchimba visima vya maji. ili kuwasaidia wananchi na matatizo haya.
 
Kwakuwa ni visima 12 sioni kama ni tatizo kubwa, kama bado hajachimba na aliahidi, basi mbinu hii hapa: Aombe CDM makao makuu wamuandalie Harambee, iitwe CDM timiza ahadi ya Visima kwa Tundu Lissu, hiyo pesa itapatikana haraka na ndani ya mwezi mmoja kila kitu kwisha. Lakini jambo lingine kama ameweza kuwakingia kifua pesa zilizokuwa zinaibwa na CCM kupitia hiyo michango ya maendeleo na wao basi waonyeshe moyo kwa kuanza kujipanga japo kuchimba hata kisima kimoja ili Lissu akichimba 12, baSI viwepo na vya ziada kwa nguvu zao, kwahela iliyopona kwenda magambani kwa kisingizio cha kuchangia maendeleo
 
Niliwahi kusema hapa(in relation to Mnyika) kuwa wakati wa kampeni mgombea ubunge hutoa ahadi kwa matuamini mawili:


  1. Yeye kushinda na hivyo kuwa mbunge
  2. Chama chake kushinda uchaguzi wa Rais na hivyo kutwaa dola

Pasi na shaka kwa Tindu ni hivyohivyo. Utekelezaji wa ahadi ni mzuri kama mtakuwa mmeshika na dola kwa vile inawapa uwezo wa kutekeleza sera zenu kwa kutumia mkate wa Taifa. Kwa kuwa CHADEMA haikuweza kutwaa dola ni vigumu kidogo kuweza kutekeleza ahadi kama zilivyotolewa kwa kuwa serikali ya CCM ilishatamka kuwa haitapeleka maendeleo katika majimbo ya wapinzani( refer Hotuba ya Pinda katika bunge la juzi juu ya kauli ya Maria Nagu kuhusu hili kule Arumeru Mashariki)
 
Mwacheni afanye kazi za kitaifa kwanza, hata sisi ambao sio wa singida tunamhitaji. Halafu uwe unasummarize habari zako.
 
samirnasri

Jambo hili ni tatizo kwa baadhi ya waliochaguliwa katika Chadema. Mfano. Diwani wa Rusahunga (CDM) hafanyi yale aliyowaahidi wananchi, wanamsubili 2015 wamhukumu. Na kila mwana CDM aliyechaguliwa na wananchi kuongoza katika nafasi ya vitongoji, vijiji, Udiwani au Ubunge kama hatimizi ahadi alizotoa, hatuwezi kuwa na uhakika kuwa 2015 ataendelea. Hivyo watimize wajibu kwa sababu tutawadondosha.

Zaidi ya hayo, wanaweza wakashindwa kupita hata katika chujio maana wakati wa kugombea tena, lazima uje na "evidance" kuwa ulichoahidi kimetekelezwa. hatuwezi kusimamia CCM tukashindwa kujisimamia sisi wenyewe. Toa kijiti katika jicho lako kisha...

Quality
 
Last edited by a moderator:
Kaka, nilikuwa Singida last week, hayo maneno uliyoambiwa kuwa Lissu anadaiwa na wananchi wa Singida Mashariki ni maneno yanayotoka kwa watu walio kambi ya CCM. Nakwambia hivyo kwa sababu Hotel niliyofikia nikiwa Singida ni Hotel ambayo jamaa hao wa CCM walifikia wakifuatilia kesi ya uchaguzi Dhidi ya Tundu Lissu. Hao jamaa usitegemee hata siku moja kuwa watasema Tundu Lissu anapendwa.

Jamaa hao wanachukia saana wananchi kutochangia. Cha ajabu ambacho huyo jamaa hajakisema ni ukweli kuwa hakuna wananchi wanamwamini Lisu zaidi kuliko hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa au Diwani. Diwani au mwenyekiti wa mtaa akiitisha mkutano, wananchi hawatoki, lakini TUNDU LISSU akiitisha mkutano viwanja vinajaa ile mbaya, ndio maana jamaa wanamchukia saana, lakini hakuna kitu kama hicho kuwa wananchi watamwadhibu Tundu Lissu 2015.
 
mtoa mada nae ni gamba,katumwa huyu na pia hajui wajibu na majukumu ya mbunge.sisiemu wanahubiri mpaka majukwaani kua hawatotoa fungu kwa majimbo ya wapinzani,sasa muanzisha mada inamaana hata radio au television na magezeti hayafiki huko??kweli penye wajinga mwerevu hana nafasi,LISU ni tunu ya taifa na ni kati ya bidhaa adimu duniani na tanzania kwa ujumla.acheni ujuha wana singida,mwigulu ndio mnamuona mjanjaa kwa kuwadanganya,sisiemu ni bora ya ukimwi.acheni ujinga jamani
 
inshu hapa naona huenda haina ukweli kwani hatujafahamu kama kweli Lissu aliahidi visima hivyo na hata kama aliahidi ni muda gani alitoa kutimiza ahadi hiyo.

Pia suala la kuzuia michango sio hoja kuna michango ipo kisheria na haiwezi kuzuirika na hii ndo iko kwenye bajeti ya serikali,kama huyo msomi wa huko Singida anaongelea michango ya hiari haina ulazima wa kutoa na wala haipo kwenye bajeti ya maendeleo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom