Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Apr 23, 2012.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Juzi nilikutana na rafiki yangu mmoja ambaye ni msomi wa shahada ya uzamili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam na ni mzaliwa wa Singida Mashariki, jimbo linaloongozwa na Lissu. Tukiwa safarini tulianza kusimuliana mambo mbalimbali yaliyokuwa yamejiri bungeni jana yeke. Nilimsimulia rafiki yangu juu ya muongozo uliokuwa umeombwa na Lissu kwa spika baada ya spika kubatilisha hoja ya zitto kabla hoja hiyo haijafika mezani kwake. Nilimsifu Lissu nikasema yule jamaa ni JEMBE kweli.

  Jamaa yangu aliniambia kweli Lissu ni jembe lakini haoneshi u-jembe wake jimboni kwake. Nilishtuka na kumwambia aache utani akaniambia habari ndo hiyo kwamba Lissu amekuwa moto bungeni lakini jimboni kwake ameshindwa kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni. Nilimuomba anithibitishie maneno hayo kwani sikuamini kama Lissu angewasaliti wapiga kura wake. Jamaa akaniambia wakati wa kampeni Lissu aliahidi visima 12 endapo angechaguliwa kuwa mbunge na kwamba chama chake cha CHADEMA kiliahidi kumuonezea nguvu ya kujenga visima hivyo, lakini takribani miaka miwili sasa Lissu hajachimba kisima hata kimoja na kwamba wananchi wengi wamekata tamaa na wameahidi kumuhukumu katika uchaguzi mkuu ujao kama hatatimiza ahadi zake.

  Zaidi ya hapo niliambiwa kitu ambacho Lissu amefanya ni kuwakingia kifua wananchi wake wasichangishwe michango mbalimbali kitu ambacho kimechangia halmashauri pia kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake kwa madai kwamba wananchi wake hawachangii kuwezesha kukamilika kwa miradi hiyo. Kilichowaumiza na kuwasikitisha zaidi wananchi wa singida mashariki ni pale Joshua Nassari alipoanza kuchimba visima siku moja tu baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo la arumeru mashariki.

  Nilisikitika sana baada ya kusikia habari hizo kwa kuwa mimi binafsi namuamini sana Lissu na uwepo wake bungeni una mchango mkubwa sana kwa ustawi wa upinzani na kwa kuiweka serikali katika msitari mnyoofu. Nililazimika kuziamini habari hizo kwa kuwa mtoa habari ni mfuasi wa mageuzi na kwa kuwa na mimi napenda harakati za CDM katika kulikomboa taifa nimeona ni vyema niliweke suala hili jamvini ili wahusika walione na wachukuwe hatua stahiki jimbo lisije likarudi kwa chama cha magamba mwaka 2015.

  Najua bado Lissu ana zaidi ya miaka miwili mbele ya kuweza kusimamia ahadi zake kwani ahadi ni deni. Wananchi wanahoji kama chadema walimwambia watamsaidia ajenge visima mbona mpaka leo hawajatimiza ahadi kama walivyofanya Arumeru mashariki? au kwa kuwa singida ni ngome ya CCM? Naomba chadema kama chama wachukuwe hatua kuhakikisha baadhi ya ahadi hizo zinatimizwa ili kulinda hadhi ya chama kuelekea mwaka 2015.

  Chadema wakumbuke kwamba singida na kanda ha kati kwa ujumla imekuwa ngome ya CCM kwa miaka mingi hivyo hawapaswi kuchezea bahati waliyoipata huko singida mashariki bali wanatakiwa watumie jimbo hilo kama chachu ya kupata mjimbo mengi zaidi mwaka 2015. Singida mashariki iwe mfano kwa majimbo mengine ya ukanda huo ili wananchi washawishike kuchagua chadema katika uchaguzi ujao. Daima mtu anayekupenda atakwambia ukweli.

  Nategemea michango yenye kujenga na sio kejeli wale kubeza, najua wengi tuna mapenzi binafsi na Lissu lakini kwenye ukweli lazima tuuseme kwa manufaa ya upinzani ambao naamini wengi tunaupenda.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah,ni deni kubwa sana.
  Naamini chadema 2015 watapata viti vingi sana vya ubunge (zaidi ya 100).
  Lakini naamini pia kwamba viti walivyo navyo saivi vingi wata poteza,(zaidi ya 10).
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  tusimbeze mleta mada... ana ujumbe mzito, Ndugu yangu Palalisote usiwe unabutua kila hoja

  Lets accept challenges to move forward... Hata mimi jimboni kwangu huwa napokea challenges
   
 4. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hao wananchi wa huko kwa Lissu mbona vilaza sana, walimchagua kama Mbunge au Mfadhili?? Kama mbunge tumesikia akitoa hoja kibao bungeni kutimiza wajibu wake lakini kama walimchagua awe mfadhili wamebugi wangemchagua Manji awe mbunge/mfadhili wao. Jukumu la kuchimba visima ni la serikali, mbunge anasimamia utekelezaji kupitia mfuko wa jimbo au halmashauri. Cha kushangaza wanamlaumu Lissu halafu wanasifia Mwigulu Nchemba...
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  una orodha ya ahadi za jk alizoahidi wakati wa kampeni? kama huna wala usizifuatilie maana kama unashtuka hiyo ya Lissu, za jk utazimia
   
 6. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tutamkumbusha asante kwa kutukumbusha
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hivi ahadi ya pinda aliyotoa kwa waandishi wa habari kwamba angetoa tamko Jumatatu imetimizwa?
   
 8. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli kuwa kuna ahadi alitoa, anatakiwa afanye juu chini azikamilishe. Na kwa wabunge wa chama kama Chadema naamini wakiwa wazi juu ya mahitaji kama ya visima katika majimbo yao, watapata usaidizi wa hali na mali kutoka kwa wapenda maendeleo ambao ni wengi sana.
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  You may call me whatever you wish lakini kama mambo yataendelea kama yalivyo tutakumbukana mwaka 2015 baada ya uchaguzi kumbukeni wananchi hawaangalii ni kwa kias gani una shine bungeni bali wanaangalia jinsi unavyowatatulia matatizo yao ndio maana kuna wabunge hawaongei bungeni lakini majimboni kwao wanatukuzwa.
   
 10. O

  OPORO Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe ni deni la visima!!!
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tundu Lissu achukue tahadhari kubwa na aanze kuzifanyia kazi ahadi zake kwa wananchi. Bahati mbaya kwa sasa wabunge wanageuzwa serikali/afisa miradi, na kama aliahidi basi ni vema afanye hivyo maana wabaya wake ni wengi mno na wanata kumtoa bungeni.
   
 12. K

  King kingo JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Angalizo zuri, sabodo si alitoa msaada wa kuchimba visima Tanzania yote apambane ahakikishe vinachimbwa kwa msaada wa sabodo.
   
 13. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu,mbona hamkukaa kujadili ahadi za kikwete ambaye ndie mtawala wa nchi?mpaka mkaanza jadili ahadi za lissu?na huyo unaemuita msomi ameshindwa kujua kwanini lissu mpaka sasa hajatimiza ahadi?majungu tu tena achana jembe wewe huyo unaemuita msomi hata asome vpi hatakaa aufikie uwezo wa lisu.jezea lissu nini
   
 14. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani mtoa mada hakuongelea werevu au ujinga wa hao wananchi bali ni utekelezaji wa ahadi zake.. hivyo basi

  Moja Kumbuka ni hao hao wajinga ndio watapiga kura 2015, kwahio kama wanategemea / walitegemea kupata jambo ambalo hawakulipata basi watakuwa dissapointed (vile vile kumbuka Lissu ni mwiba kwa CCM hivyo watafanya kila mbinu kumuondoa, hivyo lazima awe macho)

  Pili Kama alijua kujenga visima ni kazi ya serikali kwanini alitoa ahadi.., (kwahio kama alitoa ahadi, kusema sio kazi yake its no excuse). Hivyo ni vema kujipanga na kutekeleza angalau theluthi ya ahadi, kutokufanya kwa JK sio sababu ya kutokufanya kwa Chadema / Lissu, mafanikio ya hawa wabunge wachache wa sasa ndio itapelekea upatikanaji wa wabunge zaidi come 2015
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Makosa ya CCM hayawezi kurudiwa na CHADEMA. Tukumbuke CHADEMA wanasema CCM ni wazuri wa kuhubiri na kutoa ahadi lakini utekelezaji hakuna. Sasa kama Tundu Lissu alitoa ahadi ni vema akaitimiza vinginevyo hawezi kuisema CCM - na huu ndio mtihani walio nao CHADEMA wa kuhakikisha wanatenda tofauti na CCM.
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu,unajua kwa nini majimbo mengi yanayokaliwa na CHADEMA hayajawa na maendelo?serikali inafanya jitiada za maksudi kukwamisha mipango ya jimboni ili kuhakikisha mbunge aliyopo hafai.alafu huyu mleta mada alivyoeleza tu!ghafla nikakumbuka kesi ya lissu na jinsi anavyojituma kama mbunge wa taifa si jimbo moja.
   
 17. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Nawaonea huruma wabunge!!Inawezekana fedha zilizotakiwa kwenda jimboni kwa Lissu,zimeliwa na wajanja wizarani!!!
  Hata kama ungekuwa wewe,ungefanyeje kazi?Jukumu ni la wananchi kuwahukumu wanaotafuna fedha zetu wazi wazi!!!
   
 18. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  katiba mpya haitakuwa na majimbo ya uchaguzi, kutakuwa na proportional representation kama south africa kulingana na idadi ya kura chama ilvyopata kwa hiyo bungeni ni mwendo mdundo tu.
   
 19. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  M4C, POWER OF THE PEOPLE, Haitakuwa na maana kama hatuta sikiliza matatizo ya watu na kuya tatua, naomba tundu lissu apate ujumbe huu na kuuzungumzia.
   
 20. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ana udhuru, kesi hizi nazo zinapoteza muda kwahiyo hawawezi kumlaumu kwa lolote.
   
Loading...