Lamkyeku
JF-Expert Member
- Apr 18, 2014
- 494
- 661
Anaandika Lissu,
Fedha gani za Mzungu nilizopigia kampeni mwaka 2015?
Fedha zote nilizotumia kwenye uchaguzi wa mwaka jana zilitokana na malipo ya kiinua mgongo tulizolipwa wabunge wote.
Niliondoka LEAT mwezi February 2009, zaidi ya mwaka na nusu kabla sijawa mbunge.
Kazi ya ushauri wa kisheria niliyoifanya kati ya mwaka 2007 na '09 haikuhusu wananchi wa vijiji vitano vya Bagamoyo kunyang'anywa ardhi zao.
Ilihusu kampuni ya SEKAB Bio-Energy kupewa hekta 22,000 za Shamba la RAZABA (Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo) ambalo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliipatia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika miaka ya '60 kwa ajili ya ufugaji ng'ombe.
SEKAB Bio-Energy walipewa shamba hilo kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2007.
Barua ya Wazungu hao kupewa shamba hilo iliandikwa na Dkt. Jumanne Ngasongwa, wakati huo Waziri wa Uchumi, Mipango na Uwezeshaji.
Mimi nilipewa kazi ya ushauri wa kisheria juu ya taratibu za utathmini wa shamba hilo kwa ajili ya ulipaji fidia na masuala yanayohusiana nayo.
Kwa kuwa mimi sio wakili magumashi, nyaraka zote nilizoziandaa kwa ajili hiyo ninazo na nimezipitia tena baada ya maCCM wa humu ndani na/au mawakala wao kuleta uzushi huu.
Hakuna hata moja inayohusu mwanakijiji hata mmoja kunyang'anywa ardhi yake. And believe you me, I was paid handsomely for my legal advice.
Mimi ninajulikana kimataifa kwa kupigania haki za ardhi za wanavijiji katika nchi hii zilizoporwa kwa mabavu na maCCM na kukabidhiwa wawekezaji wa nje.
Whether ni Rufiji Delta au kwenye hifadhi za taifa za Umasaini au kwenye Goldfields za Kanda ya Ziwa, nimetetea wananchi dhidi ya makampuni ya kigeni na mawakala wao wa Serikali za maCCM.
Nimeifanya kazi hiyo tangu ujana wangu. I'm proud to say I've fought tirelessly and consistently for my people.