Tundu Lissu amewasilisha Mpango wa Kujenga jengo la TLS kwa Tsh. 3 bill wakati CHADEMA haijajenga

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wakuu Mheshimiwa Tundu Lissu amewasilisha mpango wa Kujenga Jengo la TLS kwa Tshs. 3,000,000,000 huku Makao Makuu ya Chadema Wakishindwa Kujenga jengo jipya Muda wote Takribani Miaka 27. CCM ilivyokua na Miaka 27 ilikua tayari Imefanya Mengi na Inamiliki Majengo, Viwanja na Mali nyingine nyingi.

Hali Inasikitisha Makao Makuu ya Chadema iliyopo maeneo ya Uswahilini sana hivi ada za wananchama huwa mnapeleka wapi?

Mnashindwa Kununua Ardhi Mkajenga Jengo la Tshs.500,000,000 kama Moja Fleets za UDSM? Kwa Uwezo wa Mbowe tuu anaweza Kujenga Jengo la Chama kama Muhisani kwani hata Nyumba yake anayeishi ina gharama kubwa zaidi ya TShs .500,000,000.
makao makuu.jpg
 
huu sio muda wa mwafaka kwa chadema kwa kujenga majumba ya kifahari ili kushindana na ccm hizo zitakuwa ni kujitafutia sifa za kijinga.

hiyo ofisi kwa chadema kwangu nahesabu kama ni kambi tu. kwasababu saizi chadema ipo kwenye vita ya kupigania demokrasia.

na uzuri sisi wanachama wa chadema hatuangalii uzuri wa ofisi za chadema tunaanga malengo ya chadema ya kuikomboa tanzania.
 
Yani unataka kufananisha chama tawala kilichoshika dola zaidi ya miaka hamsini ndiyo ukilinganishe na chama pinzani Kwa mtazamo chadema inaangalia maslahi ya wananchi kwanza siyo ufujaji wa fedha.
Mfano viwanja vya mipira na majengo ya ccm ni mali walizotakiwa kurudisha serikali mara baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza kwa sababu ni mali zilizojengwa kwa kodi za wananchi. Madili wanayopiga serikalini ndio yanayowapa pesa za kujenga ofisi.
 
Kwanza mali nyingi za CCM ni za NCHI. Na siku upinzani wakichukua NCHI mjue hilo ni mojawapo ya ajenda. Kurudisha Mali
Siyo kweli kuwa mali NYINGI za CCM ni za nchi. Ukweli ni kwamba MALI ZOTE ZA CCM NI ZA nchi. Walizipata kwa kuchukua hela ya serikali, kuwachangisha wananchi wote kwa lazima, kukata mishahara ya wafanyakazi wote kwa lazima, na kuna wakati waliweka michango kwa kupitia vinywaji kama soda na bia.

Ni mpum.bavu pekee anayeweza kusimama hadharani kusifia CCM kuwa ina rasilimali.
 
Sisi tunawajengea wananchi uwezo wa kujitambua

Km majengo ccm anayo na opposition akiingia ataifishe majengo yote ya ccm kwani yamejengwa kwa kodi zetu
 
Hivi unadhani CDM wanashindwa kujenga ofisi yao ya kudumu?

Inawezekana sana, ila ile nyumba pale ni mradi wa mkubwa, anaendelea kula laki5 zake kila mwezi for the rest of his time. Si ndo kukamatia fursa au unataka agombee ubunge awanyime wengine nafasi?
 
mawazo yako hayana tofauti na viongozi wa dini wanaokaa kwenye mahekalu namagari ya kifahari wakati waumini wao hawana hata nauli ya kwenda ibadani wanategea lifti au kutembea kwa miguu
 
Tls siyo mali ya chadema halafu mali nyingi za ccm zilichumwa wakati wa chama kimoja ambapo kila mwananchi ilimlazimu kuchangia.
 
Mimi kama mdau wa sheria, NASHAURI PESA HIZO ZIKAJENGE MAKAO MAKUU YA TLS DODOMA.Siyo Dar tena. TLS lazima waangalie policy za nchi pia.DODOMA ndo katikati.
 
Back
Top Bottom