Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA , ameondoka nchini humo leo Jumanne kwenda Ubelgiji huku akisema “sikimbii mapambano, ila nakwenda uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.”

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam (JNIA), Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), amesindikizwa na maofisa wa Ubalozi wa Ujerumani, Marekani, ndugu, jamaa na marafiki.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Lissu amesema, ameamua kuondoka nchini, pamoja na mambo mengi, kunusuru maisha yake na “kujipanga upya kisiasa.”

Lissu anasema, amekuwa akitishiwa maisha yake, mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi mkuu wa Oktoba, hali iliyomfanya yeye na wasaidizi wake watatu, kukimbilia kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani, jijini Dar es Salaam, ili kuomba hifadhi.

Mwanasiasa huyo amekuwa nyumbani kwa Balozi huyo tangu Jumatano ya tarehe 4 Novemba 2020.

Katika Uchaguzi huo, Lissu alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 1.9 milioni, huku Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitangazwa mshindi kwa kupata kura 12 milioni kati kura 15 milioni zilizopigwa.

Kupatikana kwa taarifa kuwa maisha ya mwanasiasa huyo machachari wa Upinzani nchini Tanzania yako hatarini, kunakuja miaka mitatu, tangu aliposhambuliwa kwa risasi na wanaoitwa, “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma

Shambulio dhidi ya Lissu, lilifanyika mchana wa tarehe 7 Septemba 2017, wakati alipokuwa akirejea nyumbani, akitokea viwanja vya Bunge, kuhudhuria mkutano wa Bunge la asubuhi.

Mara baada ya tukio hilo ambalo lilimjeruhi vibaya, mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisafirishwa hadi nchini Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye nchini Ubelgiji.

Lissu alirejea nchini Jumatatu, tarehe 27 Julai 2020, kutokea nchini Ubelgiji na kujitumbukiza moja kwa moja kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, mke wa Lissu, Alicia Magabe, ameondoka Tanzania kuelekea nchini Ubelgiji. Magabe aliondoka nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ameongeza, “mimi siyo mtu wa kukimbia vita. Maisha yangu yote, nimekuwa mtu wa mapambano,” amesema mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Alipoulizwa anatoa wito gani kwa wananchi waliompigia kura na Watanzania wengine, Lissu amesema, “ujumbe wangu kwao, ni kwamba mimi sikimbii mapambano. Nakwenda kufungua uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.”



2.jpg
6.JPG
3.JPG
1.jpg
4.jpg
 
Panya ukimuona nyumbani ukimkimbiza angalia shimo anakokimbilia huko ndio Kwao Lema na Lissu wamekimbizwa Tanzania wamekimbilia mashimo ya Kenya na Kutaka kwenda USA kwa Lema ukimbizi kwa Lema na Lissu katimukia Ubalozi wa Ujerumani na Ubelgiji huko ndiko shimo lake alikotokokea.

Mungu mwema katuonyesha watanzania panya hawa tuliowakimbiza wametokea mashimo yepi.

Toka mwanzo tuliambiwa CHADEMA wamiliki ni Wakenya ,Wazungu na Wamarekani tumeshadhibitisha wanaenda kwenye mashimo yao.
 
Back
Top Bottom