- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye anakabiliwa na makosa ya uhaini na uchochezi. Tarehe 09 Aprili, 2025 Lissu alikamatwa na jeshi la polisi mara baada ya mkutano wa hadhara alioufanya Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.
Kupitia ukurasa unaotumia jina la 'siasatz' katika mtandao wa TikTok ilichapishwa video inayomuonesha Tundu Lissu akisema chama chake ni CCM (Chama Cha Mapinduzi).
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search, pamoja na marejeo ya video, umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kutoka kwenye video iliyochapishwa na Global TV katika mtandao wa YouTube.
Video hiyo imehaririwa kwa kukata vipande na kuunganisha isivyo stahili hatimaye kupotosha ujumbe wa Lissu.
Katika video halisi, Lissu alikuwa akieleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho kilikuwa chama cha kwanza ambacho alijiunga nacho.
"Mimi mwanachama chama changu cha kwanza cha siasa, ni Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu nilikuwa CCM, ilikuwa ni lazima iwe hivyo, unataka kujiendeleza, hakuna namna"
Rejea hapa.
View: https://www.youtube.com/shorts/lMHFUBZ6VVI