Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,702
- 149,934
Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wabunge ndani ya Bunge letu,ni ukweli ulio wazi kuwa kuna wabunge wachache ambao wakisimama Bungeni na kutoa hoja,basi hoja zao mara nyingi hufanika hoja za wabunge wote walioachangia katika siku hiyo.
Mmoja wa wabunge hawa ni mh. Tundu Lissu.Spika,Naibu Spika au Mwenyekiti wa Bunge anaposoma oradhi ya wachangiaji na jina la Tundu Lissu likatajwa,basi ninaamini watu wengi wakiwemo hata wana-CCM husogea karibu na Luninga zao kusikiliza mh. huyu atasema nini.
Lissu ndani ya Bunge huwa ni mwiba kwa serikali na humtesa sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) katika maswala ya utungaji wa sheria na sidhani kama serikali huwa ina amani pale Lissu anapopata nafasi ya kuongea ndani ya Bunge.
Naamini kwa jinsi Lissu anavyoichachafya serikali Bungeni kwa hoja na hotuba zake ambazo huwa ni gumzo nchi nzima,leo hii Lissu akikoma kuwa mbunge kwasababu yoyote ile,basi Bunge linaweza kurudi live hata siku inayofuta.
Wabunge wengine ambao leo hii wakitoka Bungeni serikali inaweza kupumua ni mh.Godbless Lema na Zitto Zuberi Kabwe.
Wabunge hawa niliyowataja,kwa mtazamo wangu, wakitoka Bungeni leo hii,si ajabu figisufigisu zote hizi za Bunge kutokuwa live zikafikia kikomo.
Mkitaka kuthibitisha nachokisema,subiri muone magazeti ya kesho yatatawaliwa na hotuba ipi kati ya hotuba ya Lissu na ile ya Mwakyembe.