GE2025 Tundu Lissu akifikishwa Mahakamani kuendelea na Kesi ya Uhaini leo Septemba 18,2025

GE2025 Tundu Lissu akifikishwa Mahakamani kuendelea na Kesi ya Uhaini leo Septemba 18,2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Leo, Alhamisi Septemba 18.2025 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu inaendelea tena kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Leo Jamhuri itaanza kujibu mapingamizi mawili yaliyowekwa na Tundu Lissu, ikiwemo pingamizi linalohusu uhalali wa hati ya mashtaka

Kutoka Mahakamani hapo, tunakusogezea kuona namna Tundu Lissu alivyofikishwa leo, kama ilivyo kawaida amefikishwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Jeshi la Magereza, huku viunga vya Mahakama hiyo kwa ujumla ulinzi wa maafisa wa Jeshi la Polisi nao ukiimarishwa.


 
Kwasasa kila mtu hana imani na mahakama zetu. Hili jambo si zuri kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Write your reply...atandikwe viboko haini dhurumaji huyu na mwenzie mnyika na thelathini
 
Kwasasa kila mtu hana imani na mahakama zetu. Hili jambo si zuri kwa mustakabali wa taifa letu.
Shida unakuta mto hukumu ameteuliwa na mshtaki! Hapa ndipo kwenye shida kubwa. Ukienda tofauti na Bosi wako, unakosa uteuzi.
 
Back
Top Bottom