Tundu Lissu aibuka kidedea!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu aibuka kidedea!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUKUTUKU, Mar 9, 2011.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mahakama kuu kanda ya Dodoma ,jana ilitupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu (CHADEMA) na kusema kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa kimakosa hivyo haiwezi kuendelea kusikilizwa.
  Jaji Sivangilwa Mwagesi,alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi kutokana na vifungu vya kisheria na akasema haiwezezi kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
  Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama wawili wa CCM,Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo Mbunge wa singida mashariki Tundu LISSU,msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa serikali.
  Hata hivyo wakati kesi hiyo ikifutwa jana,Lissu mwenyewe hakuwapo mahakamani baada ya kuelezwa kuwa aliharibikiwa na gari akiwa njiani kuja Dodoma ambapo aliwakilishwa na Ndugu yake Samson Mkotya ambaye alisema kuwa mbunge huyo alikuwa Morogoro baada ya juzi kuharibikiwa na gari lake.
  Kufutwa kwa kesi hiyo ni ushindi kwa Tundu lissu ambaye tangu mwanzo wa kesi hiyo alionekana kujiamini zaidi na kusema kuwa kesi hiyo ingeishia katika hatua za mwanzo bila ya kufika mbali.
  "Mimi nasema kuwa,kesi hii naisimamia mwenyewe na ninatambua kuwa haiwezi kufika mahali popote kwa kuwa imejaa makosa mengi ya kisheria ambayo kimsingi kama jaji ataamua kufuata haki hakuna kesi hapa,"alisema Lissu siku alipowasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo.
  Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwasilisha kumbukumbu za hukumu za kesi nyingi ambazo zilifunguliwa kwa mtindo huo ambazo alisema kuwa yeye(Lissu) alizisimamia lakini alishindwa.
  Baadhi ya kesi alizozinukuu Lissu ni pamoja na kesi ya John Mnyika na Charles Keenja,Joyce Chitende na Zainab Gama,John Jombi na Christopher Ole Sendeka ambazo alisema kuwa zote zilifunguliwa kwa mtindo huo lakini zilishindwa kuendelea.
  Jana Jaji Silivangira alisema licha ya kifungu cha 111(b) ambacho Lissu alisema kuwa kimekosewa kutokuwa na mapungufu ya moja kwa moja,lakini kwa kutumia sheria hiyo katika kifungu 112(a),(b) bado ufunguaji wa kesi hiyo ulionekana kuwa na makosa.(Chanzo cha habari:Mwananchi 9 machi 2011,pp3).

  Nawasilisha
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa ni kupotezeana muda tu, Bora wangeendelea na shughuli zao kuliko kushinda mahakamani kwa kitu kisichofaa
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hivyo vijamaa vinapinga matokeo vimetoka wapi? Vilale mbele hukoooo....:Lissu endelea na kazi yako kusaidia jimbo letu masikini la Singida Mashariki.
  Tuko pamoja, tulikuchagua wenyewe, tutakuunga mkono pia.....njaghamba iuhoma ilolo wang'u.........keep it up!
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sio bure watakuwa walitumwa na watu wakubwa!!
   
 5. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Siasa za bongo bana.. ndio maana mi napenda soccer
   
 6. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Comrade Lissu, pamoja sana!!
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  bravo!!!
   
Loading...