Nawe Nyani Ngabu, umebugi kwa kujichanganya. Unasema siasa ni propaganda. Kwa hilo nami nakubaliana na wewe, lakini kilichofuatia, na ufafanuzi wako, kinakinzana na unachotaka tuelewe (rejea maandishi mazito katika bandiko lako).
Maudhui na jinsi ya kuendesha propaganda ndiko hutofautiana kati ya mtu na mtu, au kikundi kwa kikundi. Utofauti huo unatokana na lengo la hiyo propaganda.
Nikirejea mada yako, Mh Lissu na Serikali, kisiasa wote wamekuwa wakiendesha propaganda. Kwa kuwa serikali ina madaraka, imekuwa ikitumia, silaha yake hiyo, kuhakikisha propaganda yake inafanikiwa.
Labda tu tujadili ni aina gani ya propaganda hizo na usahihi wa jinsi zinavyoendeshwa. Je, matokeo yake ni hasi au chanya kwa wahusika?