Tundu 'Frankenstein' Lissu

K
Kweli kabisa mkuu,Ndugai hastahili heshima yoyote.
Uliona wapi spika akaramba miguu ya Rais hapa duniani.
Huyu Ni spika wa hovyo kabisa hapa duniani halafu fisadi.
Nimeona Tanzania spika alipokuwa Job Ndugai mzee wa kujipendekeza kwa Rais
 
Ni kweli kabisa sometime watuulize hata wengine namna ya kumsoften mpinzani wako pasipo madhara ya mwili wake ,uhai au kumpatia umaarufu.

Washukuru tu kuwa baada ya 2020 1. Atakuwa sio Rais wa nchi
2. Si mbunge wa jimbo au kuteuliwa
3. Sio rais wa TLS
Hivyo atapiga kelele huko uchochoroni tuuuuu No impact
Wakicheza vzr atakuwa kimya
 
Hatimaye muda ndio unaongea Sasa.
 
Hivi wewe unadhani kuwa kiongozi wa Juu ndio kuwa na busara? Hivi Ndugai Ana busara gani na nanhii naye Ana busara gani,anashinda mwaka mzima anaongea matusi tu jukwaani na mabarabarani.
Lissu anaongea ukweli mtupu.
Mtazoea tu,najua hamkuzoea.
Nilitegemea jibu kama hilo kwa kuwa niliamini, na ukathibitisha, kuwa unawakilisha kundi (lugha ya matusi) la wasiojua maana ya busara.
 
Tatizo hao unowaita viongozi wa juu, wewe unawachukulia kama miungu fulani inayotakiwa kutukuzwa.

Kwenye nchi zilizoendelea hao watu wanachukuliwa kama watumishi wa umma, hivyo wako subjected to demands of their people

Hayo uliyosema ni kweli. Je, ni sahihi kukebehi binadamu mwenzio, kwa mila za kiafrika? Au ndiyo itikadi ya chama chake? Je, akipata madaraka itakuaje?
 
Hayo uliyosema ni kweli. Je, ni sahihi kukebehi binadamu mwenzio, kwa mila za kiafrika? Au ndiyo itikadi ya chama chake? Je, akipata madaraka itakuaje?
Mchuma janga hula na wa kwao, hao ccm unaowatetea wangekuwa hawapendi kejeli wasingekuwa na utamaduni wa kuwakejeli wapinzani wao

Ila kwa kuwa wao wakiongozwa na mwenyekiti (Rais) huwa wanakejeli wenzao, acha na wao wakejeliwe.

Hili game gumu mwaka huu.
 
Hahahaha!!! Kumbe yule mama naye mwamba sana!
 
Mkuu Tundu Lissu anakusalimia sana, na anakutakia usiku mwema.
 
Game la mwaka huu limeanzia mitandaoni na litaishia mitandaoni kama yalivyo mapenzi ya mitandaoni.

Nje ya mitandao hali ni tofauti kabisa. Nafasi finyu CHADEMA kilikuwa nayo kinachafuliwa na mteule wake wa Urais. Mikusanyiko ya watu (nyomi) imemwondoa kwenye busara za kiuongozi na kuwa mzee wa kijiweni wa MIPASHO. Anacheza ngoma ya Magufuli pasipo kujitambua
 
Dah!

CCM nadhani mna majuto mengi sana!

Maana mmeumba dubwana [sisemi hivyo kwa ubaya] ambalo halidhibitiki tena.

Sasa hivi hata kumkamata na kumfungulia vi kesi uchwara hamuwezi tena.

Mkuu, nakuhakikishia Lisu anajaribu kuchangamsha genge tu, kitu ambacho ni kizuri sana kwa afya ya democrasia

Lakini hawezi kupata zaidi ya 20%
 
Mkuu, nakuhakikishia Lisu anajaribu kuchangamsha genge tu, kitu ambacho ni kizuri sana kwa afya ya democrasia

Lakini hawezi kupata zaidi ya 20%
Hilo la kupata hata 20% sina uhakika nalo kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi.

Hivyo ni vigumu kusema atapata kiasi gani cha kura.

Ila binafsi naamini kabisa kama uwanja wa mapambano ungekuwa uko sawa, basi Lissu angeshinda huu uchaguzi by a landslide.
 
Mkuu Ngabu!! Kwa ninavyoona uchaguzi uwe huru au usiwe huru Lissu anaenda kumshinda magufuli vibaya sana!! Sioni mtumishi wa umma kwenye sekta yeyote iwe vyombo vya ulinzi na usalama au taasisi za serikali ambayo consciousness yake itamwambia ambebe magufuli dhidi ya Lissu. Sijaona
 
Kipi Lisu kinamfanya amshinde Magu? Kuzunguka kwenye mitaa kadhaa hapa dar?
 
Objectively speaking, Lissu ni presidential candidate mzuri sana.

Ana uwezo mkubwa wa kuelezea changamoto zinazowakabili watu.

Lakini bado sioni ni jinsi gani anaweza kukivuka kizingiti cha tume ya uchaguzi isiyo huru....
 
Mkuu, hata kura zihesabiwe hadharani Lisu hashindi!

Sijui mnaosema Lisu anashinda mnakuwa mko mitaa gani yani
 
Kipi Lisu kinamfanya amshinde Magu? Kuzunguka kwenye mitaa kadhaa hapa dar?
Lissu anapendwa, Lissu anakubalika. Akili yake, sera zake na maono yake juu ya a Tanzania si ya kawaida.
kubwa zaidi ni exposure yake anayoitumia kwenye mazingira yetu inamuweka mbali zaidi kwenye kukubalika dhidi ya wagombea wote!

Mbaya zaidi matendo ya Magufuli dhidi yake Lissu na Chama chake Lissu bila kusahau dhidi ya wafanyakazi, wakulima, vijana na wafanyabiashara inamfanya pia Lissu kuwa hazuiliki vyovyote vile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…