Tundu Antipas Lissu

Kwani tuhuma huthibishwa na nani? Mbona dr slaa alitowaga tuhuma nzito kwa ccm

hasa viongozi wake waandamizi kwani kilitokea nini?

Mbona the list of shame aliyoitoa hadi leo haijafanyiwa kazi?

Hizo ni propaganda za ccm kama kawaida yao
 
povu.
risasi yenu ya mwisho kwe bunduki yenu ilikuwa slaa
sasa mmeishiwa risasi subirini vichapo tu
 
Nyie endelezeni tu matusi...

Kwenye kura ndo mtapata takwimu halisi bodaboda na waliokosa ajira Tanzania mnaowaita mizigo wako wangapi...

Kule kwetu wanasema mtajua mchanga na mawe kipi kingi...

Msamiati kama wa 2010 Mwaka huu hatutaki kusikia eti kura Zimeibiwa. ataetangazwa Mshindi tuamini ndo Mshindi. 5 Years later Gwajima leo ndo anakuja kusema 2010 Slaa alishindwa kweli na alistahili kushindwa.
 

Ndiyo umeandika nini rubbish. ungekua unajitambua usingetaka watu wawaze kama wewe, bure tena bure kabisa.
 

Yeye Slaa anataka wananchi wamchague nani? Aliyepo chooni ama aliyetoka chooni? Umesoma nilichoandika kweli? Nilisema it's too late kwa maana kwamba Lowassa ameshapitishwa kugombea kupitia Chadema na kelele za Slaa kwa sasa ni za kinafiki. Angeshitaki kwa wanaChadema toka kipindi hicho angalau angeeleweka. Sasa hivi anafanya kampeni ya CCM pamoja na kuwafananisha CCM na choo.
 
Kiukweli hapo Tundu Lissu amebugi kabisa, badala ya kijibu hoja anaenda kumtaja Josephine, HAKUKUWA na huo ulazima!! Sasa nimeanza kuona ukosefu wake wa busara!
 
UMENENA MKUU...MATUSI YA VIJANA WA VIROBA WA CHADEMA YASIKUSUMBUE! #HapaKaziTu

Mtakapojibiwa officially ndo mtakapo haha kumtafuta mchawi kati yenu stay tuned no one is guilty until proven guilty so enjoy your day while waiting for more and more discouraged news
 
Kwanini kama kweli ni mteteaji...lowasa alipoingia chadema yeye katoka.....busara angebaki ili asaidie kumtubisha ufisadi huo ausemao...otherwise inakuwa kamkimbia ....maana yeye lowasa alijua kuwa anakoenda kuna Dk ambae amekuwa mwiba akiwa ccm still aliingia chadema....
 
Aliulizwa nanukuu "unafikiri kwa nini slaa ameachana na siasa/chadema?"......sasa ukiliangalia hilo swali vzr linaruhusu mtu kujibu kulingana na anachokijua...hakuna tatizo katika majibu ya lisu ila kuna tatizo katika fikra zako kuwa lazima ajibu kama unavyotaka.....tunaheshimu mchango wa dr.slaa lakini pia watu tunaamini ccm ni chafu zaid ya lowasa,tutamshughulikia lowasa yeye kama yeye ila tunachokitaka sasa hivi hili genge la escrow,epa na mikataba ya gas na petrol ya dharura liondoke kwanza...
 
Ni vyema Chadema wajibu hoja za Dr.Slaa badala ya kutukana,haitasaidia kitu kumkashifu mtu aliyekijenga chama kwa nguvu zake zote
 

Huwezi kumshughulikia Lowassa yeye kama yeye baada ya kuwa rais.
Sio kwa katiba ya sasa.
Labda useme kuwa Lowassa anatumika tu kama njia ya kuingia ikulu afu mtamfanyia impeachment.
Kwa katiba ya Tanzania kumtoa rais madarakani au kumdhibiti ni kazi ngumu.
Na hasa akiwa na udhibiti wa vyombo vya dola
 
Nafarijika sana nikipitia mitandao ya kijamii kwani 90% ya wadau wanamuunga mkono Eddo sasa sijui kura zipigwe humu humu afu ma admn ndo wewe wasimamizi
 

kura yangu ni kwa lowasa.tena mmenipa hasira zaidi.mimi ni msukule wa ukawa.
 

Ndio kitachofanyika na ndio maana wanaitwa ukawa
 
Ndio kitachofanyika na ndio maana wanaitwa ukawa

Sasa hivi tu kumtoa JK imewatoa Ukawa jasho mbali na skendo zote zilizoitikisa serikali.
Hiyo ukawa wameshindwa hata kuisajili kwa "merger of political parties" ambayo inaruhusiwa kisheria na ni rahisi sana kwa sababu viongozi wangepoteza nyadhifa zao.
Hata makubaliano ya ukawa hayajasajiliwa rasmi chini ya sheria.
Ukawa sio chombo kilichosajiliwa kisheria. Ukawa hakitakuwa chama kinachoongoza serikali. Kikatiba Chadema ndo chama..
Kwengine wote Rais akishatangazwa na serikali kuundwa vinakuwa vyama vya upinzani.
Rais atatakiwa kuendesha nchi kwa kufuata katiba (ambayo haijabadilishwa) na rais hana mamlaka ya kuibadilisha. Rais anatumia katiba kutawala na sio makubaliano ya ukawa.
Tamu sana hii.
 
sasa huoni yey kachafua.! Na yeye anatakiwa kuchafuliwa bila kumchagulia uchafu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…