Tunda hili mimi sili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunda hili mimi sili!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 5, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ninaapa kwa mababu, na mizimu ya kikwetu,
  Natoa leo sababu, roho yangu iwe kwatu,
  Ni hili lilonisibu, kunifedhehesha utu,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili!

  Nimepewa tunda hili, la bure sikununua,
  Ni moja siyo mawili, hilo nililichukua,
  Nina hamu kwelikweli, alonipa kang'amua,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili!

  Alonipa kasifia, kasema tunda ni tamu,
  Kanipa kaniambia, wengine wanalo hamu,
  Hakuna alowahia, kulila tunda adhimu,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili!

  Ndipo nikashangilia, wakijiji nina ngeke,
  Tunda nililoshikia, kama vile libeneke,
  Hamu nikalishakia, nyumba hima nifike,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili.

  Kufika pale nyumbani, sahani nikaandaa,
  Kulitoa mfukoni, na kisu kukiandaa,
  Nikapigwa tafurani, nikabaki kushangaa,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili!

  Tayari limeshang'atwa, upande huu na ule,
  Kwa kisu lilishakatwa, ati na miye nilile,
  Wanadhani wa kuletwa, kumbe nami yule yule,
  Walilokula wengine, tunda hili mimi sili!

  Tunda hili sasa chungu, kuonja miye sitaki,
  Nataka lililolangu, si tunda la kinafiki,
  La kwangu la peke yangu, lenye utamu wa haki,
  Walilokula wengine tunda hili mimi sili!
   
 2. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Burudani na kukesha zina raha yake...

  Shukurani kwako mkuu...mazito hayo.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  naona magwiji bado wamechoka na furaha ya Obama au ya kina Jeetu!
   
 4. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Nadhani ni zaidi hayo.

  Mkkj uko juu,kama Air bus A380.

  Najitahidi kukusanya mistari,lakini inakataa.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nile nimepewa nile,
  Nile wakijiji nile,
  Nile alivyokula yule,
  Nile tunda lile lile?

  Nilile au nisile,
  Nilile au nilale,
  Nisilile au nile,
  Nile tunda lile lile?

  Nile kama vile yule,
  Nile nami vilevile,
  Nile hapa au pale,
  Nile tunda lile lile?

  Nile bila ya simile,
  Nile lile kama Chale,
  Nilile hapa si pale,
  Nile tunda lile lile?

  Nilile mwana wa yule,
  Nile walokula wale,
  Nile hilo pole pole,
  Nile tunda lile lile?

  Nile au sote tule,
  Nile au tukalile,
  Nile au nisilile,
  Nile tunda lile lile?

  Nile jingine nilile
  Nile hilo siyo lile,
  Nile la kwangu nilile,
  Nile tunda lile lile?

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 6. S

  Sunshine OLD Member

  #6
  Nov 6, 2008
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This is super!
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji waapa, kwa tunda uliloonja,
  Eti we utalikwepa, kisa wameshalionja,
  Kilipata hutoepa, utakula hutoonja,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!

  Utamu wa tunda mwana, ulile na uridhike,
  Liwe limemenywa jana, ile ile ladha yake,
  Hata ulile mchana, utasema mwake mwake,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!

  Tunda ale Amani, au Joni halihusu,
  Awe kala Jakisoni, asojuwa shika kisu,
  Aonje naye Hasani, haondoi hata nusu,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!

  Tunda lataka matunzo, tautunza utamuwe,
  Tunda la toka mwanzo, linakifu na ujuwe,
  Ka we mtu kwa vikwazo, utakufa kwa kiwewe,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!

  Midhali umeridhia, tafaidi utamuwe,
  Wako wanolililia, waomba walikamuwe,
  Hawajali mabakia, wanataka warushiwe,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!

  Tunda ule kwa nafasi, wewe ni mwenye haraka,
  Usiwe na wasiwasi, kama tunda walitaka,
  Uache huo ukwasi, tunda halina viraka,
  Mlaji ni mla leo, mla jana kala nini?!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  .... standing ovation!!!!....
   
 9. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mama uko juu sanaa........!

  Waarabu wa Pemba,mnajuana kwa viremba.
  Chamoto au baridi,mihogo au sambusa.
  Tunda lako malidhia,na mama kakuhusia.
  Ulile bila yakukonda,japo wamelimega.
  Huku na kule,tayari limeshamegwa....!!!???
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hahahahaha.. unajua watu wenye njaa utawaona tu..
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mimi ndege wa tunduni,Kwa ukweli nimechoka
  Wakijiji upewe nini,Sambusa hukuitaka
  Haya tunda mdomoni,Bado wanyata nyata
  Ndege miye nina njaa,Nipeni lo tunda nile

  Waki tano zimepita,Tangu nione tunda
  Nilinyakua kashata,Numbani kwa dada Rinda
  Utamu sikuupata,Ufananao na tunda
  Ndege miye nina njaa,Nipeni lo tunda nile

  Sisi ndege wa angani,Kazi yetu kunyakua
  Wakijiji wa shambani,Kwa huba unaletewa?
  Wajenzi sio mitini,Wahenga nimeelewa
  Ndege miye nina njaa,Nipeni lo tunda nile

  Mimi hua sichagui,Liloiva au bichi
  Lilotandwa buibui,Balungi na parachichi
  Lenye maji lenye tui,Baharini kavu nchi
  Ndege miye ina njaa,Nipeni lo tunda nile

  Liloliwa ndilo zuri,Au wewe unabisha
  Lilo zima la kiburi,Muda kula chelewesha
  Halijajua uturi,Harufuye yachekesha
  Ndege miye nina njaa,Nipeni lo tunda nile

  Kweli yote nayapenda,Ila bichi lina kazi
  Midomo itakupinda,Meno yapata ganzi
  Ukicheza tavurunda,Muulize hata Dazi
  Ndege miye nina njaa,Nipeni lo tunda nile
   
 12. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Mzee Mwanakijiji, achana na chako kinyaa,
  Wameonja wanamji, Tunda bado kusinyaa,
  Kwanza likoshe kwa maji, sijifiche Kwenye minyaa'
  limeonjwa upande huu, wewe geuza kungine.
   
 13. K

  Kwaminchi Senior Member

  #13
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji, u mtu wa kushangaza!
  Lini liingia jiji, mchana au mkesha?
  Tunda hilo lafariji, mbona we linakutisha?
  Tunda nimelila juzi, na leo nalitafuta.

  Tunda limejaa maji, Zam Zam yakumbusha.
  Kwa kuukosa mtaji, kipato kuniangusha.
  Tunda likahama mji, kwako likajidondosha.
  Tunda nimelila juzi, na leo nalitafuta.

  Tunda hilo la Ujiji, hima wewe harakisha
  Latafutwa kila mji, latamaniwa Arusha.
  Lilikuwa kwa Somji, wewe lakubabaisha?
  Tunda nimelila juzi, na leo nalitafuta.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  matunda bado bora,anga hizi eehh!
  Heko Wakijiji
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hilo tunda kula tuu,
  Ushamba wa ukijiji, utakutokea juu,
  Hilo tunda la kijiji, utamuwe uko juu,
  Tunda hilo kama tende,huwa halina makombo.

  Huwa halina makombo, tunda hilo kama tende,
  Jahazi lisende kombo, ukaja vimba matende,
  Tena kwa Mzee Kombo, kuna mti wa Mtende.
  Tunda hilo kama tende, huwa halina makombo.

  Wataka la peke yako, peke yako utaweza?
  Muulize ndugu yako, peke yake ameweza?
  Jilie kinyako vyako, ni wangapi wameweza?
  Tunda hilo kama tende, huwa halima makombo.

  Afadhali lilomegwa. Utamuwe julikana,
  Kuliko lililo bwagwa, utakuja kulikana,
  Nawe wajibwagabwagwa, mwishowe utajikana,
  Tunda hilo kama tenda, huwa halina makombo.

  Suma Gii aliimba, katika wimbo wa chungwa,
  Ni kweli alijiimba, tunda chenza kama chungwa,
  Mduara kama dimba, la machenza na machungwa,
  Tunda hilo kama tende, makombo huwa halina.

  Jee wee hula vya watu? Jua na vyako huliwa,
  Kwa kila mla vya watu, jua na vyake huliwa,
  Tundalo memega watu, matunda yote huliwa,
  Tunda hilo kama tende, huwa halina makombo.

  Weza lila wima wima, na hata ukiinama,
  Weza onja kwa kupima, utamue mesimama,
  Natena ukijipima, tajiona mesimama,
  Tunda hilo kama tende, huwa halina makombo.

  Tamati nimemaliza, kwa ushauri mwanana,
  Usije kujimaliza, kwa usingizi mwanana,
  Ukila ukimaliza, ni kwa utamu mwanana,
  Tunda hilo kama tende, huwa halina makombo.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16

 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17

 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18

 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Sorry na samahani, repy yangu ili stuck na mimi nikawa na resend kumbe it was going through. Natafuta pa kuifutia sipaoni.
  Moderator please do the needful, mistakes highly regratable.
   
 20. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Una kipaji
   
Loading...