Tunayathamini mapenzi..? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunayathamini mapenzi..?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by s.fm, Feb 2, 2011.

 1. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna sehemu nilisoma maneno flani hivi “mapenzi siku hizi ni kama magazeti”

  Haya maneno humanisha jinsi gani gazeti linavyotumika, sijui linaweza kusomwa na watu wangapi kwa siku. Lakini mwisho wa siku linakwisha kabisa na kupotelea mbali.

  Kwa upande mwingine mwenzenu kwa ule ukweli sijawahi hata siku moja kuona (kwa mfano) mtu fulani amekuja na mpenzi wake bar,beach hata kanisani n.k. wakiwa kwenye gari na mume akajaribu hata kumfungulia mlango mkewe anaposhuka ili kuonesha japo kale ka u-gentleman.

  Vitu vingine tunaviona kwenye sinema tu na kusoma kwenye novel, lakini kuona au kufanya live ni ndoto. Lakini natamani kama siku moja tungezijua faida za mambo haya pengine mapenzi tuliyonayo yange-improve kwa kiwango kikubwa.

  Hivi unamchukuliaje mpenzi wako? unapokua nae unahisi umekaa na nani na moyo wako unamfikiriaje?
  Hapa mara nyingi huwa ni tatizo kwa sababu tunashindwa kuelewa ndio maana mara nyingi umekaa na mpenzi wako unakuta mwenzio yuko bize mimeseji kibao anatuma na kupokea, mara afungue facebook n.k. na mwisho wake unaanza kuhisi mambo mengine.

  Ni mara ngapi umeonesha hali ya kumthamini mkeo/mume?
  Hapa pia kuna mambo mengi tu yanafanyika kama kujua anachopenda, kumletea zawadi, kumhusisha katika mambo mbali mbali, kumjali na kumuonesha upendo. Wengine kuambiana nakupenda mpaka wakati wa ku-do, baada ya hapo utaisikia hewani tu au wengine mpaka aandike sms lakini kuambiana face to face inakua ngumu sana! Ni vizuri kusema maneno hayo kila wakati ili kumjengea mazingira ya upendo mpenzi wako.

  Kusikilizana nalo ni tatizo sugu, je unamsikiliza mkeo/mumeo inavyopaswa?
  Unapomuonesha unajali na kuheshimu na kuyapenda mawazo yake ni dalili tosha za kuimarisha penzi!

  Watu hawataki kukubali kabisa kama mapenzi ni “commitment” mpenzi wako si sawa na mtu mwingine, ana nafasi yake maalumu katika moyo wako, kama watu hawatakubaliana na hili basi matatizo haya hayatakwisha

  Vurugu tupu kila kukicha, wengine wanaishi kwa machungu usiku na na mchana…usione watu barabarani hivi na majumba makubwa wanamoishi, utakuta baba analala chumba chake na mama chumba chake. Sasa hapo sijui watoto watajifunza nini

  Watu wengi siku hizi wanafunga ndoa ili kutimiza wajibu na ahadi walizojiwekea katika maisha tu, mapenzi ni kitandani lakini upendo na mapenzi ya kweli hakuna! Ndio maana ndoa zingine hazidumu kabisa na wengine wanaambulia magonjwa mfululizo.

  Kuna jamaa yangu kipindi fulani alikua ananiomba mchango wa harusi nikagoma kabisa, maana ulikua anaomba mchango kwa mara ya nne, yani yeye kila siku anafunga ndoa tu wanaenda honeymoon huko huko vurugu na kuchapana makofi. Hii yote ni kwa sababu ya kutothamini wapenzi wetu.

  Yafuatayo ni mambo yanayoweza kukufanya umthamini mpenzi wako kama ukiyazingatia

  Ukweli
  Uaminifu
  Uadilifu
  Kutambua umuhimu wako kwake
  Kufurahi pamoja
  Kupima/changanua mambo
  Kumpenda jinsi alivyo
  Kuwa na utu/utashi
  Kujifunza kusamehe
  Kujifunza kuwa na huruma na
  Mawasiliano mazuri


  Nawasilisha…
   
 2. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa kuna mambo wanaume huwa hatuyafanyi lakini ni madogo sana.

  Umesema kweli kabisa
   
Loading...