Tunayaishi maono ya hayati Mwalimu Nyerere?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Baada ya simulizi ya jana juu kifo Cha Mwalimu Nyerere tarehe 14/10/1999, simulizi iliyopambwa na ulikuwa wapi tarehe hiyo! Niliahidi kuendelea na Uchambuzi wa MAONO ya Mwalimu Kwa Taifa hili.

Jambo kubwa na la msingi sana HAYATI Julius Kambarage Nyerere ndiye kiongozi wa mstari wa mbele katika mapambano ya kudai Uhuru Kwa upande wa Tanganyika. Alijitoa sadaka kuongoza harakati hizo ambazo zimetufanya kuwa na uhuru fulani.

Baada ya kupata uhuru fulani, Mwalimu aliliongoza Taifa kupambana na maadui wakubwa watatu. Maadui hao ni Umaskini, Rushwa na Maradhi. Nyerere aliamini Taifa likiondokana na Umaskini, Rushwa na Maradhi litaondokana na Uhuru fulani na kuwa na uhuru kamili. Uhuru wa kimamlaka na kujitegemea. Uhuru wa kutokuyategemea makoloni yetu ya kale kuendesha nchi.

"Nimetumia neno UHURU FULANI kwa kuwa bado nchi yetu haijaweza kujitegemea Kwa 100".

Miaka zaidi ya 60 tangu Tanganyika kuwa huru na Miaka 58 tangu Tanganyika na Zanzibar kuungana bado tunapambana na vita dhidi ya Umaskini, Maradhi na Rushwa.

Ni wazi kuwa tangu uhuru na Kila awamu inapambana na maadui hawa ijapo siku hizi maadui wameongezeka.

Kwa mfano toka Mwalimu anga'atuke madarakani Mwaka 1985
kumekuwa na njia mbalimbali ambazo zimetumiwa ili kuzuia maradhi na hasa kwa kutoa elimu ya afya, usafishaji wa mazingira na elimu ya kutibu dalili za magonjwa badala ya magonjwa yenyewe. Na kumekuwa na hatua mbalimbali za kiuchumi zimekuwa zikichukuliwa ili kuondoa umaskini – hatua hizo zinahusisha kuwekeza katika uzalishaji wa watu binafsi na kuwafanya wajijengee uwezo wa kiuchumi. Ziko njia nyingi sana zimetumika kuhakikisha kwamba uchumi wa Taifa unakwenda juu.

Upande wa Rushwa nako kumekuwa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa, ijapo jana Mhe Rais Samia akiwa Kagera alisema nayo ijichunguze kama ipo salama.

Ukweli ni kuwa mtu akitoka nje ya Tanzania akaja hapa nchini akasikiliza hotuba za Viongozi wetu kutoka Chini mpaka juu atadhani ndo kwanza tunaanza kupigana na maadui hawa. Hawezi kujua kuwa maadui hawa wana miongo kadhaa wanapiganwa.

Kwa ufupi jitihada za kupigana na maadui hawa zinalegalega na kushindwa kuzaa matunda ambayo Mwalimu alitegemea. Maadui hawa wamegeuzwa Chrous kila mtu anawaamba lakini hawatokomei. Kizazi kinachozaliwa leo wanadhani ni wimbo.

Taifa linahitaji mjadala mzito juu ya Kupambana na maadui hawa. Taifa limejaa watu wanafiki. Jiulize kwani wanaopokea na kutoa Rushwa wanatoka kuzimu? Wanaopokea na kutoa Rushwa ni tofauti na wale wanaotuita kwenye mikutano ya hadhara kutukemea tusipokee au kutoa Rushwa? Umaskini unaoliandama Taifa unasababishwa na watu kutoka Mbinguni? Nani aliua viwanda AMBAVYO HAYATI aliweka kama DIRA? Mbeya mlikuwa na viwanda vingapi? Leo vipo? Walioviua walitoka Mbinguni au kuzimu? Mfumo wa elimu enzi za Mwalimu ulikuwa unamuandaa Mwanafunzi kuajiliwa na kujiajiri. Je mifumo ya siku hizi ambayo Kila mtu akiamka anabadilisha unamuandaa Mwanafunzi kujiajiri? Mifumo inayomuandaa Mwanafunzi kukariri inaweza kumsaidia Mwanafunzi kujiajiri?

Miaka 60 ya Uhuru Taifa linashindanisha Shule kufaulisha Wanafunzi badala ya kushindanisha kuibua vipaji vya Wanafunzi. Kushindanisha kufaulu watoto Kwa kuwaibia Wanafunzi Mitihani au kuwakaririsha majibu kunafaida Gani Kwa Taifa? Yaani Mwanafunzi akifaulu ambaye haelewi analisaidia nini Taifa? Kwa nini Shule zisishindane kuibua vipaji vya watoto? Miaka 60 ya Uhuru Bado watu wanaajiriwa Kwa Ufaulu na GPA bila kupima Competent ya huyo unayemwajiri. Yaani tunaamini wenye GPA ndio wenye UWEZO wa kufanya kazi. Hatuji kama Kuna watu Wana GPA za kukariri na wengine za kununua matokeo? Why tusiende kwenye Competent based?

Mwalim alilenga Competent based ndiyo maana alilenga kwenye elimu ya kujitegemea.

Kama Nyerere alichukia Rushwa na Umaskini basi hata sisi tuchukie haya Kwa dhati na vitendo. Tungekuwa tunachukia Kwa vitendo hizi ngonjera zingekuwa zilishafutika. Lakini Kwa kuwa tunakemea huku tukipokea Rushwa na kutoa ni ngumu kuumaliza mzizi huu. Nyerere huko aliko ninaamini anatucheka Kwa unafiki tulionao hasa tunapokemea vitu ambavyo tunaviishi. Anacheka Kwa kuwa anajua Watoa Rushwa na wapokea Rushwa hawatoki kuzimu. Walioua viwanda AMBAVYO vilikuwa vinatutengenezea ajira hawatoki Mbinguni. Wanaoharibu mfumo wa elimu Kila kukicha hawatoki PEPONI, tunao na wao pia wanauchukia mfumo huo.

Vita dhidi ya maadui hao watatu imepiganwa miaka yote 25 ya utawala wa Mwalimu Nyerere kupitia Tanu na CCM na kisha imeendelea kupiganwa kwa miaka yote zaidi ya 37 ya tawala za Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli na sasa Mhe Samia Suluhu Hasan.

Mapambano magumu

Ziko sababu kadhaa zinazosababisha mapambano kuendelea hadi leo na tena kwa mafanikio ya kusuasua.Leo sitazitaja. Labda Kwa ufafanuzi nitoe chache.

Sababu ya kwanza ni uwekezaji usio na mwendelezo katika mipango na utekelezaji wa hatua za kupambana na ujinga, maradhi na umaskini. Katika kila kipengele kwa miaka zaidi 60 tumekuwa tukiwekeza nguvu isiyo na uwiano wa wakati na mahitaji. Kila mtu anafanya anachoona kinatija kwake na siyo kama Taifa.

Unakuta tunajenga shule nyingi na zinakaa miaka 10 hazina walimu, vifaa wala miundombinu mahsusi. Siku tukipata walimu unagundua kuwa shule zilishachoka na kuchakaa kwa sababu hazikuwa na matunzo.

Msukumo wa kisheria,Tanzania haina msukumo wa kisheria ambao umeiweka Serikali katika jukumu la lazima la kupambana na umaskini, maradhi na ujinga. Masuala ya kupambana na maadui hao watatu yameguswa kwenye Katiba, tena kwa kutajwa kama “haki” za wananchi. Lakini, aina ya haki hizo haiwezi kusababisha Serikali ikafunguliwa mashtaka pale inapokosekana.

ITAENDELEA

Na ELIUS NDABILA
0768239284
 
Back
Top Bottom