Tunaweza kutokomeza urasimu

Tunaweza kutokomeza urasimu

masomo

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Posts
208
Reaction score
46
Kama viongozi mbali mbali katika idara mbali mbali wangekuwa na dhamira ya kweli kuongeza ufanisi na kupunguza rushwa kwa nini wasingetoa namba zao za simu ili mtu anayehitaji huduma akizungushwa zaidi ya mara mbili basi aweze kupiga simu kwake ili kuingilia kati.tunaona urasimu mwingi katika idara mbali mbali kama hapa nchini kama vile tanesco,mashirika ya hifadhi ya jamii kama vile NCCF,mahakamani,mawizarani,wilayani,halmashauri,hazina,na sehemu nyingine.pia mtu akiona na kuwa na ushahidi wa wizi na rushwa aweze kutoa taarifa kama wananchi wanavyofanya katika jeshi la polis.madhalani,wizi wa rasilimali za taifa,meno ya tembo nk.leo kama ingeahidiwa ahadi ya bakshishi kwa atakayetoa taarifa ya majangili nadhani wengi sana wangekamatwa tena wakiwa kwenye ujangili au hata wakiwa na meno ya tembo.naomba wakubwa watoe mamba zao za simu na ahadi ya pesa kiasi fulani ili wananchi watoe taarifa za uzembe,wizi,rushwa na urasimu katika serikali na maeneo mengine.kama hakuna ushirika katika ujangili huu watatoa namba zao ili tusaidiane kazi,na pia kama wanataka ufanisi.
 
Urasimu sio kitu kibaya (kwa maana ya bureaucracy) umewekwa kama namna ya kudhibiti kivunjwa/kupindishwa kwa sheria kwa ujumla wake. Sasa huku kwetu tunatumia vibaya na inakuwa kama channel ya kuwawezesha watu kudai rushwa. Kwa hiyo mi nadhani Urasimu acha uwepo tupigane na rushwa. Fikiria chaos ambayo ingekuwepo kama utaratibu wa kupata kiwanja usingekuwa na urasimu! Na urasimu uliopo tu, Kiwanja kimoja wanamilikishwa watu watatu au zaidi. Au pale mtu akiomba kitu ofisini, mtu mmoja tu ndio angekuwa anaidhinisha. Yaani macho yake tu ndio yanashuhudia alichoidhinisha! Kungebaki na kitu kweli?
 
Back
Top Bottom