ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Nawasalimu kwa salamu ya kizalendo.
Jana chama chetu cha ACT-Wazalendo kilizindua kampeni za urais, ubunge na udiwani katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala. Tunawashukuru Watanzania wote walijiotokeza katika mkutano wetu, waliofuatilia katika vyombo vya habari na hata kwenye mitandao ya kijamii. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaahidi kuwatumikia kwa nguvu zote na kwa maarifa yote na kwa ushirikiano mkubwa kati ya viongozi na wananchi.
Viongozi wamesema mengi, ila kwa ufupi Watanzania wameombwa kuchagua moja miongoni mwa mambo yafuatayo; mbwembwe zinazofanywa na CCM, ulaghai unaofanywa na UKAWA, na Utu, uadilifu na Uzalendo unaohubiriwa na ACT-Wazalendo.
CCM wanachofanya sasa ni mbwembwe ambazo kimsingi hazitamsaidia Mtanzania yeyote zaidi ya kuendelea kumdidimiza, CCM ni chama ambacho kimetufikisha hapa tulipo baada ya kuacha misingi iliyoasisiwa na waanzilishi wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume. Mgombea wake hafai kuaminiwa hata kidogo sababu hakerwi na RUSHWA wala UFISADI unaoendelea kulitafuna taifa hili. Hakusema lolote katika kashfa ya ESCROW na hata ile ya EPA. Sasa wanatulitea mbwembwe, Watanzania tuwakatae.
UKAWA ni walaghai kwa sababu kama wapinzani waliutangazia umma orodha ya mafisadi katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke. Katika orodha ya watu 11 namba tisa alikuwa Lowassa, na waliendelea kumtangaza hivyo kwa jina la ufisadi kwa miaka yote, ni mwezi uliopita tu ndipo walipoanza kumsafisha. Huu ni ulaghai kwa Watanzania na huku ni kucheza na tumaini la watanzania waliloliweka kwa vyama vya upinzani.
Imeshakua dhahiri sasa kuwa ndani ya CCM, UFISADI umekua mkubwa na sasa umezaa mtoto, na huyo ni UKAWA. Hotuba za viongozi wa UKAWA sasa zimebadilika, hawazungumzii UFISADI wala RUSHWA, na kwa kuwa huo ufisadi na rushwa ni matokeo ya uongozi mbovu wa CCM, na kwa kuwa mtuhumiwa mkubwa ufisadi ndiye mgombea wa UKAWA, hivyo basi si UKAWA na si CCM ambao wanaweza kuzungumzia na kuukemea UFISADI. Watanzania wanahitaji chama ambacho hakitauonea haya ufisadi na RUSHWA, chama ambacho kitaendeleza vita hii pale walipoishia CHADEMA, chama hicho si kingine isipokuwa ni ACT-Wazalendo.
Pamoja na kwamba chama chetu ndiyo chama pekee ambacho kina ubavu wa kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na rushwa, lakini pia chama chetu kina ILANI, sera na misingi yake ambayo yote haya kwa pamoja yanatoa majawabu kwa matatizo yanayolikabili taifa letu. Hifadhi ya jamii, uchumi shirikishi, afya na elimu ndiyo vipaumbele vyetu. Hivyo basi na kwa sababu hiyo tunakuomba ukichague chama cha ACT-Wazalendo.
Tunaomba Watanzania mtuunge mkono.