KXY
JF-Expert Member
- Dec 31, 2011
- 880
- 327
Salaam kwenu!
Jioni ilipokuwa ikikaribia wengi hawakuwa na habari na maandalizi ya kitakachofuata baada ya jua kuzama. Wachache sana waliandaa nyenzo ya kuwafanya waweze kuendelea na kazi giza litakapoingia, hawa waliandaa mshumaa.
Kati ya wale wengi baadhi yao walikejeli walipoona mshumaa, hawajazoea na waliona hawaendani nao, wao sio wa kutegemea mshumaa. Zimepita siku nyingi na kwao hawakuwahi kutatizwa na kuzama kwa jua, kwao ni kama jua liliwaka kwa saa 24.
Taratibu giza likaingia, hamaki nayo ikaanza japo hakuna aliyekuwa na hakika nini kitafuata. Dalili ya mvua ni mawingu na kama itaonekana usiku ni wazi vingine vinakuwa havionekani, si nyota wala mwezi unaotustahi mara kwa mara. Giza totoro!
Umuhimu wa mshumaa upo wazi kwa sasa, wengi wametambua wanahitaji huo mwanga kwa usiku huu. Wabishi hawakosekani wao kuliko mwanga wa mshumaa ni bora kukaa gizani. Wachche hawa wanataka wawaaminishe wengi kwamba bora giza kuliko mwanga 'hafifu' na kwamba mshumaa huo hautadumu muda wowote utazimika.
Kuna hoja kutoka kwa hawa wachache, kwanza mshumaa unapowaka wenyewe unaungua kwahiyo mwisho wa siku utaisha. Pili ukipita upepo kama mshumaa huu upo wazi ni lazima utazimika.
Badala ya kutetea umuhimu wa mshumaa na kuwakejeli kwasababu wao walikejeli, inabidi kupima hoja zao. Mshumaa huu utatufikisha asubuhi? Je upepo ukivuma mshumaa utapona?
Ni vyema tukauhifadhi vyema mshumaa huu ili usizimwe kwa upepo, tuulinde, tuufunike kwa glasi kubwa itakayopunguza nguvu za upepo.
Kubwa zaidi tutambue mshumaa huu hautawaka milele hivyo muda huu tunavyofaidi mwanga wake tufanye maandalizi ya chanzo cha kudumu cha kutupatia mwanga. Isionekane kama kufanya hivyo ni kutotambua umuhimu wa mshumaa huu bali ni kutokana na mshumaa huu ndio maana tunaweza dhubutu kufanya hivyo.
Sasa hivi kuna mwanga, ni vyema kujiandaa na vita wakati wa amani. Kuna hatari ya kujisahau na kuona kwamba sisi wenye mshumaa tuna mwanga basi na tukae tukusanyike kama vifaranga tufaidi joto la mshumaa. Tuna jukumu la kuulinda kwanza na pia kuutumia mwanga huu kwa manufaa. Tukumbuke mshumaa unateketea lazima tujitahidi kujitoa huku kusiende bure.
Usiku bado mrefu, kitakachotokea kati ya sasa na asubuhi ndio kitaamua kama tutaamka salama au tutashtuka usiku wa manane baada ya ndoto mbaya tukikuta giza nene.
Asanteni!