Tunatamani kuishauri serikali tatizo haishauriki

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,012
1,522
Tunapenda nchi iendelee lakini wenye madaraka hawapendi iendelee kwa kuwa hawapo tayarhi kupokea ushauri,mwaka 2016, 17 nilifanya kazi hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kujitolea kitengo cha damu,kuna kipindi mashine ya kutengenezea blood components (PACKED RBCs,FFP, Plateletes nk) injinia alishindwa kurekebisha,ikabidi aitwe injinia kutoka kampuni iliyotengeneza hiyo machine toka India, ilichukua takribani miezi 9,na hospital ndio iligharamia kila kitu, je kuna ulazima gani wa ishu kama hizi kuingia gharama badala yakufanya leasing?

KATIKA KIPINDI hicho chote MNH ilikuwa inategemea damu salama na kuna wakati walikuwa wanakosa kabisa,WIZARA YA AFYA WATUMIENI THINK TANKS WAWAPE MAARIFA ,SIO KILA SIKU MARA MLOGANZILA CT-SCAN MACHINE HAIFANYI KAZI,MARA UPS YA THEATRE IMEFAIL,TAABU TUPU NA UREKEBISHWAJI UNACHUKUA MUDA.

Kuna Hospitali na vituo vya afya vya serikali havina kabisa baadhi ya mashine na vifaa muhimu,mfano Wilaya ya Ludewa ina Haematogy analyser moja tu na ipo ktk hospital ya wilaya, yaani kata 26, CBC test ya kupimwa dk 1 majibu yanapatikana baada ya siku 3, kipimo kinasafirishwa km kenda.

Sikilizeni watu,kuna watu wapo huku mtaani wanamaarifa kuzidi wenye nyadhifa.
 
Back
Top Bottom